Rais Magufuli amteua Dkt. Willibrod Peter Slaa kuwa Balozi

Nakumbuka kwenye kampeni 2015,Magufuli alipofika karatu alimsifia sana Slaa kwamba ni mkweli ana nondo hatukani mtu wala kutoa povu
Hatuwezi kuacha kumtumia galacha kama Slaa akifanya kazi za kawaida kabisa wakati taifa lipo kwenye vita kali ya uchumi
 
...naona jpm ana tafuta watu wa kumpigia kampeni hapo 2020 kwa kila njia..amesoma upepo ameona atakuwa na wakati ngumu 2020.....huu ni mkakati mpya... Maana anajua huko ccm hakuna anayeweza kusimama kwenye kampeni na wapinzani hapo 2020 kumpigania kwa umma...anatafuta team ya kampeni toka walioasi upinzani ili azunguke nao nchini mwaka 2020....hii haitasaidia.....watanzania wa leo si mazuzu.....watu wameamka...hata awape vyeo waasi wote waganga njaa hawa.....ni rahisi sana kumsoma JPM....hadi ifike 2020 tutaona mengi ya ajabu utawala huu dhalimu...
 
Kuuza chama kwa MAFISADI wakati wa uchaguzi mkuu pia sio mchezo mkuu.
Jamani CCM mnayo bahati na weledi wa propoganda. Hilo halina ubishi mnapata A+. Dhana ya UFISADI mmefanikiwa sana kuipigia propoganda. Mahakama ya MAFISADI imeanzishwa rasmi leo ni zaidi ya mwaka. Nyie ndie wenye vyombo vyote vya dola (polisi, TAKUKRU, DCI, JWTZ, USALAMA wa Taifa, pamoja na 'wasiojulikana'). Ni kitu gani kimewashinda kuyapeleka mbele ya mahakama ya MAFISADI hayo 'MAFISADI' yaliyouziwa/yaliyonunua chama wakati wa uchaguzi mkuu?
 
Kama mapolisi, wanasiasa wanapewa ubalozi, na wana diplomasia wanaachwa, kijana atashindwa nini?
 
Kwahiyo ulitaka hao vijana waajiriwe kwenye nafasi za ubalozi. Yaani unamaliza chuo mara paap unapewa ubalozi. Kweli siyo mchezo
Mapolisi, wanasiasa wanapewa ubalozi, kijana atashindwa nini. Maana ubalozi imegeuzwa wadhifa wa kila mtu na sio wanadiplomasia
 
Kwa watu wanaochukulia vitu juu juu wanaweza wasielewe maana ya huu uteuzi!!! Hapa ni kuwaambia wapinzani kuwa mkitusaidia kitu fulani hatutowaacha hivi hivi!!! Watu walikuwa wanalalamika sana na walikuwa wanatolea mifano wapinzani walioisaidia CCM kuwa hawathaminiwi na ikawa ni ngumu sana kuwanunua so leo wameonyeshwa au kudanganywa kuwa ukikubali tutakupa ulaji!!! heeeee wajinga ndio wali wao.
 
..kweli.

..kama vile Mzee anavyosema anapiga vita rushwa huku chama chake kinanunua madiwani toka chama kingine.

..hata ukijikita kwenye "maandishi" sera au dira nako hauko salama. Hebu nieleze chato international airport ilikuwepo ktk dira au ilani?

Hakuna ushahidi wa waziwazi kuonyesha kwamba CCM inanunua madiwani.

Pili, kuhusu Chato International Airport anaefadhili mradi ni World Bank hivyo ni rahisi kuamua kuelekeza fedha za mradi huko, kwani ni kwa manufaa kwa wilaya ya Chato na taifa kwa jumla.

Nafikiri hata mfadhili aliombwa fedha za kuujenga uwanja wa Chatio ili uwe na hadhi ya kimataifa.

Hiyo si kwa mheshimiwa raisi John Magufuli pekee bali hata wewe kama ungekuwa na mamlaka kama yake basi ungeamua kutumia fedha za ufadhili kuzielekeza katika mradi fulani wenye tija kwa taifa.

Tukumbushane tu kwamba wazungu wanakupa otions unataka kuwekzza wapi fedha za mradi na wewe unaamua ziende mahala Fulani.

Huko nyuma tuliona fedha zinatumika kwenye mambo yasiyo na tija angalau sasa hata huko Chato kutakuwa na hadhi yake.
 
And hopefully atabaki kuwa HC of Tanzania to Canada ili asaidie mapambanobya bombadier. Mark my words.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom