Rais Magufuli amteua Dkt. Sophia Kongela kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC)

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Uteuzi Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Sophia Kongela kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC)

Wakati huo huo Dkt. Maulid Banyani ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa NHC


index.jpeg
 
Mkulu anawaamini sana Ma Dr. na Prof. kama kuna mtu anaweza kupata uteuzi ni bora atafute sponsorship akasome PhD
 
RAIS MAGUFULI NA WAZIRI LUKUVI WAFANYA UTEUZI

Rais Magufuli amemteua Dkt. Sophia Kongela kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC)

Kabla ya uteuzi Dkt. Kongela alikuwa Mhadhiri katika Chuo Kikuu Ardhi(ARU)

Aidha, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amemteua Dkt. Maulid Banyani kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa(NHC)

Dkt. Banyani anayechukua nafasi ya Nehemia Mchechu ambaye alisimamishwa kabla alikuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu Ardhi(ARU)

index.jpeg
 
Ningekua mkuu wa juu nisingechagua mtu bila kujua vision yake juu ya ile nafasi ninayotaka akaitumikie.

Mfano; Kama nataka Mkurugenzi wa wa Idara au shirika fulani la umma ningetoa nafasi hiyo kwa watu watano ninaowaamini kwa sharti la kuniandikia kwa maandanishi mpango wao na maono yao juu ya kampuni / Shirika jinsi watakavyoweza kuliendesha kampuni au shirika hilo kwa faida na sio kutegemea ruzuku ya serikali muda wote. Hapo ningefanya mchujo na kumpata mmoja mwenye uzoefu mkubwa.
Kwa sasa watu wengi wana CV kubwa sana za Darasani lakini akipewa nafasi za kusimamia makampuni / Mashirika yetu wanabaki na blabala nyingi na maneno mengi kuliko vitendo. Mashirika mengi yanaingiza fedha nyingi sana lakini bado yanachukuliwa kama vile ni sehemu ya huduma tu na kuwafanya wasimamizi wake kupata kichaka cha kukwapua fedha za umma na kupiga madili . Ndio maana watu wakiteuliwa wanajihesabu kuwa wameshatoka wao binafsi kimaisha kwa sababu huenda hawakuwahi kuwaza kufanya kazi au majukumu kama hayo waliyopangiwa. Wanachojua ni kukiwakilisha chama kinachotawala hata kama serikali inapata hasara. Wanajua bunge lenye wingi wa kura za chama kimoja watapitisha ruzuku tena.
Mashirika Mengi yanakufa na kushindwa kujiendesha kutokana na teuzi kujaa siasa na ukada.

Ni rahisi kumsikia mhadhiri wa Chuo kikuu wa Sayansi ya Siasa akijipambanua kuwa yeye ni muumini wa Ubepari au Udikteta au ujamaa. Ikiwa na maana zao lake litakua kama alivyojipambanua. Kama ni muumini wa utawala wa kiimla tunategemea atakua anaandaa wanasiasa madikteta wasomi.
Kama ni muumini wa mawazo ya kumwandaa mwanafunzi kusoma ili apate kazi nzuri ya kuajiriwa ,na akawa muda wote anasifia walioajiriwa na kuwaona kuwa ni watu wenye bahati na wenye maisha mazuri basi tutegemee kuwa na wahitimu wanaowaza kuajiriwa tuu.

Labda ingereheshwa dhana ya kuwa nyuturo kwa wakuu wa idara mbalimbali ili waweze kuwaza ndani na nje ya box. Ndipo maarifa yanapoanzia.
 
Shirika la nyumba halitakaa limpate mkurugenzi atakae linyanyua kama Mchechu, story ya mchechu na serikali hii naifananisha kama kocha wa timu ya leicester city kutoka ziro to hero ilipoanza kuharibu kidogo wakamtimua kocha.
 
Shirika la nyumba halitakaa limpate mkurugenzi atakae linyanyua kama Mchechu, story ya mchechu na serikali hii naifananisha kama kocha wa timu ya leicester city kutoka ziro to hero ilipoanza kuharibu kidogo wakamtimua kocha.

Mchechu kaifanyia Makubwa Sana NHC lakin ndio hivyo Tena
 
Chuo kimoja unachomoa madaktari wawili, sio fare kabisa. Ila anahamasisha watu wasome sana...wale wapenda nafasi za kuteuliwa
 
Shirika la nyumba halitakaa limpate mkurugenzi atakae linyanyua kama Mchechu, story ya mchechu na serikali hii naifananisha kama kocha wa timu ya leicester city kutoka ziro to hero ilipoanza kuharibu kidogo wakamtimua kocha.

Mchechu ni mchapakazi nammbunifu.. shida yake ni moja tu.. ambayo ni Mwizi.. na hajui kuiba... anauzia NHC viwanja vya kampuni yake mwenyewe kwa bei juu.. hata kuzuga hawezi
 
mchechu ndio kwa heri?
Mchechu alijisahau sana kiasi cha kudhani kila mtu ni tajiri;
Nakumbuka siku moja alishangaa nyumba ya Tshs 72 mil watu kulalamika kwamba ni ghali badala ya kubuni mbinu za kuteremsha bei;
Aidha alikuwa anashirikiana na W/biashara binafsi ktk kujenga (kama lile ghorofa liliporomoka Kisutu) na kuuza nyumba!
 
Back
Top Bottom