Rais Magufuli amteua Brigedia Jenerali Charles Mbuge kuwa Mkuu wa JKT, aliyekuwepo apelekwa Mgambo

D

Doncy monco

Member
Joined
Jul 26, 2019
Messages
36
Points
125
D

Doncy monco

Member
Joined Jul 26, 2019
36 125
Rais wa Tanzania, John Magufuli amefanya mabadiliko ndani ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa kumteua bosi mpya wa jeshi hilo na kumhamisha aliyekuwepo.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Septemba 10, 2019 jijini Dar es Salaam amesema Rais Magufuli amemteua Brigedia Jenerali Charles Mbuge kuwa Mkuu wa JKT.

Jenerali Mabeyo amesema aliyekuwa Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Martin Busungu ameteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi la akiba (mgambo).

Busungu aliyeteuliwa kushika wadhifa wa juu ndani ya JKT, Februari 16 mwaka 2018 alichukua nafasi ya Meja Jenerali Michael Isamuhyo ambaye alistaafu.

Aprili 13, 2019 wakati Rais Magufuli akizindua mji wa kiserikali wa Ihumwa Dodoma, alitangaza kumpandisha cheo Mbuge kutoka Kanali na kuwa Brigedia Jenerali kutokana na kazi nzuri aliyoionyesha ya kusimamia ujenzi huo.

Mara baada ya kumtangaza, alimuita mbele Brigedia Mbuge kwenda kukaa kwenye jukwaa kuu sehemu inayotengwa kwa ajili ya viongozi wakuu na siku hiyo hiyo eneo hilo, Mbunge alivalishwa vyeo vya Brigedia Jenerali.

Chanzo - Mwananchi
 
I

Idofi

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2010
Messages
1,784
Points
2,000
I

Idofi

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2010
1,784 2,000
mgambo ni jeshi kubwa jamni lipo nchi nzima, nikiwa nafanya kazi Halmashauri huko Mbeya mshauri wa mgambo wa wilaya alikua Luteni Kanali
 
G

gataca

Member
Joined
Aug 15, 2015
Messages
83
Points
150
G

gataca

Member
Joined Aug 15, 2015
83 150
Ingekuwa Busungu ndo kapanda halafu Mbuge kashuka then upepo wa mjadala ungevuma tofauti kabisa na sasa.
wangesema kamuweka msukuma mwenzie ila sasa kamtoa msukuma story tofauti ila mimi naona poa haivutii mkuu wa majeshi na jkt wote wawe jamii moja ...pia .inawezekana kapelelekwa huko mgambo kuliimarisha jeshi hilo la akiba mambo yao wanayajua wenyewe sisi hapa ni ni speculation tu
 
stephot

stephot

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2012
Messages
8,582
Points
2,000
stephot

stephot

JF-Expert Member
Joined Mar 1, 2012
8,582 2,000
Ni kweli ila all in all jamaa alifanya kazi nzuri sana katika majukumu yote machache aliyokua anapangiwa natena kwa muda mfupi
Hii inatia moyo hata kwa wengine,kuwa ukijituma kuna mtu wa kukuangalia na kuweza kukupa haki inayostahili kwa ufanyaji bora wa kazi,sio tu watu wanapandishwa vyeo kwa kujuana hii inakatisha tamaa sana,Big up Raisi wetu Magufuli...
 
Renegade

Renegade

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2009
Messages
4,819
Points
2,000
Renegade

Renegade

JF-Expert Member
Joined Mar 18, 2009
4,819 2,000
Kuna mkuu wa mgambo na mshauri wa mgambo ni vitu viwili tofauti! Wengi wa washauri wa mgambo ni wanajeshi wastaafu kama maColonel
Washauri wa Mgambo wanatoka kwenye idara ya Mgambo ya jeshi.
 
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2007
Messages
31,018
Points
2,000
Chakaza

Chakaza

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2007
31,018 2,000
Kumbuka aliyekuwa Inspector General wa Police miaka 90 Mahundi aliteuliwa kuwa IGP kutoka RPC Arusha na cheo cha SSP wakati kulikuwa na makamishna wakubwa makao makuu ya jeshi hilo. Kuteuliwa kwa mtu ni kutokana na utendaji wake mzuri
Ili uone ukubwa wa jeshi la polisi wakati huo, angalia SSP anakuwa RPC! Miaka ya 90 maofisa wa juu walikuwa wachache sana kulingana na ukubwa wajeshi la polisi. Hata JW nako ilikuwa hivyo, 1978 tunaingia vitani mkuu wa Majeshi alikuwa Major general tuu, na maofisa wa juu jeshini walikuwa mabrigedia na makanali tuu.
 
N

ngakotecture

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2014
Messages
1,182
Points
2,000
N

ngakotecture

JF-Expert Member
Joined Dec 30, 2014
1,182 2,000
Huwa ni mmoja tu kwa jeshi zima?!
No mkuu wapo ata watano ila mmoja wapo ndio huteuliwa kuwa mnadhimu mkuuu na kwa uelewa wangu mm mdogo mnadhimu mkuu ambaye ndo lt jeneral ndio boss na mtendaji mkuu general ambaye ni mkuu hupelekew ripoti tu
 
Easy Chair Mark III

Easy Chair Mark III

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2019
Messages
566
Points
1,000
Easy Chair Mark III

Easy Chair Mark III

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2019
566 1,000
Lakini pia mnatakiwa muelewe ya kwamba kabla Rais wa nchi hajamteua MTU yoyote yule ili ashike wadhifa wa juu kabisa namna hii, ni lazima kwanza upite mchakato Fulani wa mchujo pamoja na kufanya kwanza consultantations mbalimbali na watu wake wa karibu/washauri wake. Vile vile, ikumbukwe kuwa viongozi wote muda wote wako under constant and continious vetting, KWA hiyo siyo ajabu kuona kuwa MTU wa seniority ya chini akapanda au kuteuliwa kwenye cheo cha juu zaidi, NA yule mwenye seniority ya juu akaachwa. Huwezi kujua ameachwa KWA sababu gani, yawezekana pengine kwenye vetting ameonekana kuwa na dosari, you never know!!
 
F

FUSO

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2010
Messages
16,382
Points
2,000
F

FUSO

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2010
16,382 2,000
Kwa hiyo jamaa aliyekuwepo kapewa ukuu wa Mgambo...duh!!
 
Jay One

Jay One

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2010
Messages
13,108
Points
2,000
Jay One

Jay One

JF-Expert Member
Joined Nov 12, 2010
13,108 2,000
Lieutenant General ni wangapi Tanzania.. Maana nasikiaga tu Major General, ila Lt. General sijawasikia na ni cheo kikubwa, kutoka Major General unaenda Lt. General alafu unaenda General..!!
 
wa kupuliza

wa kupuliza

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2012
Messages
2,283
Points
2,000
wa kupuliza

wa kupuliza

JF-Expert Member
Joined Jun 15, 2012
2,283 2,000
Hii inatia moyo hata kwa wengine,kuwa ukijituma kuna mtu wa kukuangalia na kuweza kukupa haki inayostahili kwa ufanyaji bora wa kazi,sio tu watu wanapandishwa vyeo kwa kujuana hii inakatisha tamaa sana,Big up Raisi wetu Magufuli...
Kweli mkuu hata yule mkuu wa wilaya aliyeharibu shamba la mbowe fasta tu akawa Rc,yule hakimu wa case ya Sugu nae alipandishwa chap chap.

Nadhani hao walifanya kazi inayostahili mkuu.
 
Mmexico

Mmexico

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2016
Messages
354
Points
500
Mmexico

Mmexico

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2016
354 500
Nafasi za uteuzi mkuu ni hatari sana inakufanya uwe mtumwa na unyenyekevu balaaa! Unaweza kuta alionyesha msimamo kidogo akaonekana hafai!! Au alifanya kosa kidogo tuu akaliwa kichwa
Jeshi linakutaka hivyo, ndio siri ya wao kuheshimiwa na kuweza ongoza Askal.

Nidhamu na utii wa hali ya juu.
 
Mmexico

Mmexico

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2016
Messages
354
Points
500
Mmexico

Mmexico

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2016
354 500
mgambo ni jeshi kubwa jamni lipo nchi nzima, nikiwa nafanya kazi Halmashauri huko Mbeya mshauri wa mgambo wa wilaya alikua Luteni Kanali
sema upendavyo ila hiyo ni bonge la Demotion.
Kabla ya huyu Msukuma anayetoka JKT, aliyekuwa akiongoza ni Mgambo ni Luten Kanali.
 
KIM KARDASH

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Messages
5,119
Points
1,250
KIM KARDASH

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2011
5,119 1,250
Huyu kuna tetesi ni mtutsi...anaejua historia yake atuwekee tumfahamu vizuri tusije kujiingiza kwenye matatizo yanayompata mzee m7 na uganda yake dhidi ya rwanda
1568311723185-png.1205820
 

Forum statistics

Threads 1,336,675
Members 512,696
Posts 32,547,468
Top