Rais Magufuli amteua Brigedia Jenerali Charles Mbuge kuwa Mkuu wa JKT, aliyekuwepo apelekwa Mgambo

D

Doncy monco

Member
Joined
Jul 26, 2019
Messages
36
Points
125
D

Doncy monco

Member
Joined Jul 26, 2019
36 125
Rais wa Tanzania, John Magufuli amefanya mabadiliko ndani ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa kumteua bosi mpya wa jeshi hilo na kumhamisha aliyekuwepo.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Septemba 10, 2019 jijini Dar es Salaam amesema Rais Magufuli amemteua Brigedia Jenerali Charles Mbuge kuwa Mkuu wa JKT.

Jenerali Mabeyo amesema aliyekuwa Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Martin Busungu ameteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi la akiba (mgambo).

Busungu aliyeteuliwa kushika wadhifa wa juu ndani ya JKT, Februari 16 mwaka 2018 alichukua nafasi ya Meja Jenerali Michael Isamuhyo ambaye alistaafu.

Aprili 13, 2019 wakati Rais Magufuli akizindua mji wa kiserikali wa Ihumwa Dodoma, alitangaza kumpandisha cheo Mbuge kutoka Kanali na kuwa Brigedia Jenerali kutokana na kazi nzuri aliyoionyesha ya kusimamia ujenzi huo.

Mara baada ya kumtangaza, alimuita mbele Brigedia Mbuge kwenda kukaa kwenye jukwaa kuu sehemu inayotengwa kwa ajili ya viongozi wakuu na siku hiyo hiyo eneo hilo, Mbunge alivalishwa vyeo vya Brigedia Jenerali.

Chanzo - Mwananchi
 
kidadari

kidadari

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Messages
5,594
Points
2,000
kidadari

kidadari

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2012
5,594 2,000
Inawezekana ni jambo dogo tu amefanya. Hizi nafasi za uteuzi wakati mwingine zinategemea damu za mteauji na mteuliwa zinavyoiviana. Mbona Makonda anafanya madudu lakini yupo tu!
Muda mwingine ukionyesha msimamo tuu hata kama upo sahihi unaonekana mkaidi... So inahitaji moyo.
 
Mromboo

Mromboo

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Messages
1,476
Points
2,000
Mromboo

Mromboo

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2012
1,476 2,000
Nafasi za uteuzi mkuu ni hatari sana inakufanya uwe mtumwa na unyenyekevu balaaa! Unaweza kuta alionyesha msimamo kidogo akaonekana hafai!! Au alifanya kosa kidogo tuu akaliwa kichwa
Kigwangala ni mfano hai
 
S

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2017
Messages
7,343
Points
2,000
S

Sesten Zakazaka

JF-Expert Member
Joined Sep 10, 2017
7,343 2,000
Mmmmh hii tumbua hamisha imefikia kwa hawa jamaa daàh, ila historia ya Mbuge ndo ujue bahati ipo duniani
Kwanini unasema bahati mkuu? Kwani jamaa hakustahili cheo na nafasi hiyo?
 
MtamaMchungu

MtamaMchungu

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2011
Messages
4,501
Points
2,000
MtamaMchungu

MtamaMchungu

JF-Expert Member
Joined Apr 10, 2011
4,501 2,000
"Cheo ni kama koti la kuazima, usiringie"
 
General Mangi

General Mangi

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Messages
14,283
Points
2,000
General Mangi

General Mangi

JF-Expert Member
Joined Dec 21, 2013
14,283 2,000
Hizi dharau sasa....
Magu kashakamata huku uraiani....
Bado anataka kushikisha adabu na kuwanyamazisha hao mabakabaka??

Tukajifiche wapi?
 
TUJITEGEMEE

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2010
Messages
14,270
Points
2,000
TUJITEGEMEE

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2010
14,270 2,000
Busungu aliyeuliwa kushika wadhifa wa juu ndani ya JKT, Februari 16 mwaka 2018 alichukua nafasi ya Meja Jenerali Michael Isamuhyo ambaye alistaafu.
Angalieni maandishi yenu kabla na baada ya kuweka bandiko. Hasa mnapoelezea vitu 'sensitive'
 
A

Ad majorem

Member
Joined
Aug 11, 2018
Messages
90
Points
150
A

Ad majorem

Member
Joined Aug 11, 2018
90 150
Vikundi vya JKT vya kwaya havijatunga nyimbo za kusifu! Chunguza utalijua hilo. Na ni kosa kubwa sana, muulize Nape

Vikundi vya JKT vya kwaya havijatunga nyimbo za kusifu! Chunguza utalijua hilo. Na ni kosa kubwa sana, muulize Nape
Afande Mbughe ni mtu wa hamasa, anapenda sana vikundi vya muziki na kazi. Hajakaa sana Kibattle. Wale waliopita kwenye mikono yake enzi za Ruvu jkt watakuwa wanalijua hilo. Kipaumbele chake yeye ni kazi tuu hata kama mazoezi mpo shallow. Nilikuwa napenda tabia yake ya Kupenda kuja kucheza Disco la jeshi na Makuruta. Anafaa sana, Mungu azidi kumuinua.
 

Forum statistics

Threads 1,336,678
Members 512,696
Posts 32,547,530
Top