Rais Magufuli amteua Brigedia Jenerali Charles Mbuge kuwa Mkuu wa JKT, aliyekuwepo apelekwa Mgambo

D

Doncy monco

Member
Joined
Jul 26, 2019
Messages
36
Points
125
D

Doncy monco

Member
Joined Jul 26, 2019
36 125
Rais wa Tanzania, John Magufuli amefanya mabadiliko ndani ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa kumteua bosi mpya wa jeshi hilo na kumhamisha aliyekuwepo.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi wa Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Septemba 10, 2019 jijini Dar es Salaam amesema Rais Magufuli amemteua Brigedia Jenerali Charles Mbuge kuwa Mkuu wa JKT.

Jenerali Mabeyo amesema aliyekuwa Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Martin Busungu ameteuliwa kuwa Mkuu wa Jeshi la akiba (mgambo).

Busungu aliyeteuliwa kushika wadhifa wa juu ndani ya JKT, Februari 16 mwaka 2018 alichukua nafasi ya Meja Jenerali Michael Isamuhyo ambaye alistaafu.

Aprili 13, 2019 wakati Rais Magufuli akizindua mji wa kiserikali wa Ihumwa Dodoma, alitangaza kumpandisha cheo Mbuge kutoka Kanali na kuwa Brigedia Jenerali kutokana na kazi nzuri aliyoionyesha ya kusimamia ujenzi huo.

Mara baada ya kumtangaza, alimuita mbele Brigedia Mbuge kwenda kukaa kwenye jukwaa kuu sehemu inayotengwa kwa ajili ya viongozi wakuu na siku hiyo hiyo eneo hilo, Mbunge alivalishwa vyeo vya Brigedia Jenerali.

Chanzo - Mwananchi
 
macho_mdiliko

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2008
Messages
10,009
Points
2,000
macho_mdiliko

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2008
10,009 2,000
Duuh kutoka mkuu wa JKT mpaka mkuu wa migambo hii ni hatari aisee, itakuwa amefanya kosa kubwa sana
Inawezekana ni jambo dogo tu amefanya. Hizi nafasi za uteuzi wakati mwingine zinategemea damu za mteauji na mteuliwa zinavyoiviana. Mbona Makonda anafanya madudu lakini yupo tu!
 
ng'wanamangilingili

ng'wanamangilingili

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2015
Messages
1,541
Points
2,000
ng'wanamangilingili

ng'wanamangilingili

JF-Expert Member
Joined Aug 22, 2015
1,541 2,000
Inawezekana ni jambo dogo tu amefanya. Hizi nafasi za uteuzi wakati mwingine zinategemea damu za mteauji na mteuliwa zinavyoiviana. Mbona Makonda anafanya madudu lakini yupo tu!
Ni kweli ila all in all jamaa alifanya kazi nzuri sana katika majukumu yote machache aliyokua anapangiwa natena kwa muda mfupi
 
kidadari

kidadari

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Messages
5,596
Points
2,000
kidadari

kidadari

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2012
5,596 2,000
Duuh kutoka mkuu wa JKT mpaka mkuu wa migambo hii ni hatari aisee, itakuwa amefanya kosa kubwa sana
Nafasi za uteuzi mkuu ni hatari sana inakufanya uwe mtumwa na unyenyekevu balaaa! Unaweza kuta alionyesha msimamo kidogo akaonekana hafai!! Au alifanya kosa kidogo tuu akaliwa kichwa
 

Forum statistics

Threads 1,336,689
Members 512,697
Posts 32,547,763
Top