Rais Magufuli amsimamisha kazi Mkurugenzi Muhimbili

Baba safi sana mzee. Nakuaminia jembe letu. Kweli sikukosea. Baba nenda na pale customer care vodacom mlimani city kuna vijana wanafanyiwa uhuni sana. Wanalipwa 246'000 badala ya 861,000. Hebu nenda hapo hata kwa baadae mzee
 
Ni kweli hatutaki maelezo, Kama machine hazifanyi kazi akitoa maelezo ndio zitafanya kazi?! The damage has been done hivyo lazima mtu atolewe kafara kutuliza mizimu ya wagonjwa waliofariki kwa kukosa huduma hiyo!

Mi nashangaa watu walivyo kua negative hapa, au labda hawafahamu hela iliyo tengwa kwa ajili ya huduma za hapo muhimbili, na hawajaona maisha anayo ishi huyo mkurugenzi ukilinganisha na mshahara Wake. Lazima tumpongeze raisi wetu ili nayey apate moyo wakupambana na hao mafisadi
 
Dah kuna genge la mafisadi lilitaka kutukosesha Raisi mwenye kasi ya ajabu kama huyu! asante sana JK kutuletea JP
 
Huu ni upuuzi mwingine. Hivi taratibu za kumfukuza kazi zimefuatwa? Bajeti je? Utawala bora na demokrasia vinafika mwisho

Kwa uzembe huu bado unawatetea? Kwanza hakuna aliyefukuzwa hao walipewa vyeo wameshindwa hivyo wamevuliwa (cheo ni dhamana) unarudishwa kwenye ajira yako ya awali.
 
amesimamishwa nafikiri taratibu nyingine za utumishi zinaendelea ukweli huwa kuna ka mchezo kanafanyika au uzembe unafanyika haiwezekani kifaa kikubwa kama kile kimeharibika miezi 2 bila kufanyiwa matengenezo wakati muhimbili inaingiza mamilioni ya pesa sababu sasa hivi haitoi tena huduma za bure
 
Hivyo sio fesh ni sawa je kama tatizo amesharipoti kukawa hakuna fungu la kutengeneza au kunasababu za msingi huko .je si ndo atamrudisha kazi na kulipwa siku ambazo alikuwa amesimamishwa, je huo ndo utawala bora
 
Tatizo letu Watz ni kufurahia mwingine kuguswa na misukosuko. Kamwachisha kazi, yeye ndiye kamwajiri?? Mkurugenzi huyo ana haki zake chungu nzima, unamwachisha tu ka Hg!!! Haya tungojee. Alisimamisha Makandarasi wangapi wa barabara bila mjadala. Wakamshinda mahakamani ka mtoto. Akalipa mihela ya kufa mtu. Hasara kwa taifa. Aliizuia meli ya Mvietnam, na samaki zake akagawa bure watu wale. Ati nitawashinda mahakamani. Amelipa meli mpya na samaki wapya kwa Dollar mpya za kimarekani. Hasara kuu kwa taifa.
Haya yoote, mlimsifia. Sitamsema vibaya rais wangu ila, Uongozi bora si hivyo. Yeye ni kiongozi, awaongoze wanaoongoza wafanye kazi ya viwango si kutimuana bila mpangilio. Ila kwa vile huwa hatuambiwi, mngekuja kutujuvya atakacho lipwa huyu mhusika baada ya kumbwaga mahakamani.

ONE MAN SHOW, Jamani hivi hajateua hata washauri? kwa sababu naona ataanza kupata aibu katika utendaji wake kwa asababu siyo level yake hayo anayoyafanya, ana haraka sana mzee wa Push-up.
 
Hii nchi nimegundua kuwa wachawi ni sisi wenyewe WaTanzania. Kuna watu hawapendi kabisa hii kasi ya Magufuli. Kama ni ndugu zenu ndio walikuwa wakiichafua serikali basi imekula kwenu manyang'au nyinyi. CCM ilikuwa ikichafuka kwa makosa ya ndugu zenu ndani ya serikali. Sasa huo ujinga mwisho wake ni sasa.

Wale wanao jiuliza kuhusu uamuzi wa Dkt Magufuli kuifuta bodi ya Muhimbuli pamoja na kumsimamisha kazi mkurugenzi eleweni kuwa kuna vyombo tayari vimempa ushauri mhe rais na hivyo yupo ndani ya sheria kwenye maamuzi yote anayoyafanya. Rais hakurupuki. Huyo mkurugenzi alikuwa ana sabotage serikali. Muhimbili ni moja ya eneo ambalo serikali ilionekana ikiborobga mno kumbe ni kutokana na watu wachache tu....itazameni bajeti ya wizara ya fedha na fungu lililoelekezwa Muhimbili ndio mtaelewa kwanini huyo mkurugenzi katimuliwa. Sio mnatumia hisia zenu za kichoko kuongea pumba hapa.
 
Bila shaka mlifahamu tangu mapema mabadiliko ya kweli yatakuja na maumivu, Magufuli nyoosha wabongo wanachukulia mambo kiutani sana!
 
Muhimbili ikijiendesha kibiashara mimi na wewe au bibi angu kule kijijini hawataweza pata huduma za msingi. Nadhani unajua maana ya public services.

Anyway, umeeleweka mkuu, a word of advise usiwe na mihemuko kwenye post. Take your time and do your home work.
Watu hawana akili, hospitali ijiendeshe kibiashara kama agakani watu masikini watapataje huduma?
 
Kwani waziri mkuu teyari ameshapatikana au Mr Magufuli amehodhi vyeo vyote hivyo kazi zote anafanya yeye?
 
Hah why havifanyi kazi? Taratibu za kuripoti na kurekebisha au kureplace vifaa vibovu zikoje? Isijekuwa taarifa zilitolewa lakini urasimu tu
 
Hii safi sana.Viva comrade JPM.Walidhani wewe ni Kikwete.Hapa kazi tu.Kama mtu huwezi kufanya kazi ondoka.Kwa nini vifaa vya MRI na CT scan vya watu binafsi vifanye kazi vya Muhimbili visifanye kazi tena kwa muda wote huo.Hii ni hujuma.Most likely huyu ana vya kwake kwa hiyo wagonjwa anawaasukumia huko.Enough is enough.Tumechoka.
hii imekaa vibaya
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom