Rais Magufuli amsamehe Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Rufiji aliyetoa taarifa ya uongo kuhusu ubovu wa gari la wagonjwa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
86,395
147,017
Rais Magufuli amemsamehe kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rufiji bwana Kilimba aliyetoa taarifa za uwongo kwa mheshimiwa Rais kwamba gari la wagonjwa ni bovu.

RPC wa Pwani amesema utaratibu wa kumfikisha mahakamani mkurugenzi huyo ulishakamilika ila bwana Kilimba amepata bahati ya mtende ya kusamehewa na Rais Magufuli mwenyewe.

Chanzo: ITV habari.

2020 Hakunaga kama Dkt. Magufuli!
 
Hii ni rushwa. RPC gani mzembe hivi? Yaani misamaha hii ya vichochoroni inawezaje kuwazuia polisi na/au TAKUKURU kufanya kazi yao? CCM ni ile ile!
 
John naomba nijibu tangu lini kumdanganya raisi limekuwa kosa la jinai??? Ni kosa la Jinai chini ya kifungu gani cha sheria???? Hao polisi walikuwa wanampeleka Mahakamani kwa kosa gani???

Unajua Magufuli anatufanyaga watanzania kuwa mazuzu sana!!! Alafu huwezi amini hii Habari imetangazwa kabisa hadi kwenye taarifa ya habari???
 
Kosa la kutoa taarifa za uongo lipo kijinai lipo chini ya kifungu namba 122 cha sheria ya kanuni ya adhabu. Ninavyoelewa mimi kifungu kile ni;

Mf. Polisi wanatafuta jambazi alafu wanakuuliza jambazi yuko wapi wewe unawaambia sijui. Hapo sawa utakuwa umefanya kosa la jinai

Ninavyoamini lile linakuwa ni kosa pale linapofanyika kwa kumzuia mtu aliyeajiliwa kwenye sekta ya umma kutofanya kitu au kufanya kitu ambacho kinahusika na jinai . Sasa suala la gari linazaa jinai gani???
 
Endelea kusoma hicho kifungu utaiona jinai ilipo.

Uwongo ni uhalifu bwashee!
 
Rais Magufuli amemsamehe kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Rufiji bwana Kilimba aliyetoa taarifa za uwongo kwa mheshimiwa Rais kwamba gari la wagonjwa ni bovu.

RPC wa Pwani amesema utaratibu wa kumfikisha mahakamani mkurugenzi huyo ulishakamilika ila bwana Kilimba amepata bahati ya mtende ya kusamehewa na Rais Magufuli mwenyewe.

Source ITV habari.

2020 Hakunaga kama Dr Magufuli!
Blood thirsity monsters
 
Au imebainika kuwa kweli gari ni bovu, lakini ndio hivyo mkubwa hakosei. Hata akikosea yeye ndio anasamehe.
Unacheza na zile spana za mkuu wa wilaya.. Gari la Mkuu wa wilaya bovu, Gari la mkurugenzi linatembea lakini linahiyaji service bab kubwaa maana nalo ni kuu kuu tu, Ambulance nayo ni mbovu.. Sasa unajiuliza wilaya hiyo itakuwa na gari lolote zima??

Wao wanajenga SGR na kununua mandege kwa cash wakati Halmashauri zetu karibia zote ziko hoi..
 
Endelea kusoma hicho kifungu utaiona jinai ilipo.

Uwongo ni uhalifu bwashee!
Uongo kwa mtu aliyeajiliwa kwenye sekta ya umma tu ndo kosa au uwongo wote??? Ndo mana hiki kifungu mie nakirafsili kwenye mazingira ya kijinai zaidi maana hapo ndo kuna logic. Kama uongo wote ni kosa la jinai wasinge specify kwa mtu fulani tu!!
 
Bwashee inaangaliwa " nia" ya kudanganya ni nini?

Hspa nia ingepelekea kutenda kosa la wizi endapo Rais angetoa fedha ya matengenezo ilhali gari ni zima!
 
Back
Top Bottom