Rais Magufuli ampongeza mchimbaji mdogo ndugu Laizer aliyeiuzia Serikali Tanzanite yenye thamani ya sh 7.8 bilioni

Siku hizi huku Jf ni kawaida sana unakuta uzi una replies 200 ukija kuufungua unakuta una replies70. Upo uzi mmoja juzi ulivunja records kwa replies 300 kufutwa.

Mdogo mdogo naona huu unaenda na kurudi kama daladala maana na mimi niliweka kakomenti kangu pendwa hapa naona mods wamekanyakua fastaaa.
Duuu, ndiyo wamekuwa hivyo siku hizi?
 
Wewe kwanza jifunze kuandika Kiswahili kabla ya kujadiliana nami.

Inaonekana una utapiamlo wa elimu.

Neno sahihi la Kiswahili ni "furahi" si "fulahi".

Wewe nawe ni country bumpkin usiyejua tofauti ya "r" na "l" kama Magufuli?

Hiyo ndiyo sababu unajishebedua hapa dhidi yangu?
Brother umepanic kinyama tulia meza mate

Utani kwa mtu mwelewa ni kupotezea

Ndio hivyo tena ameshasema na katania endelea kubishana mitandaoni wakati mmasai kapiga mabilioni yake na ataongeza vichenchede hata rihanna atamuongeza
 
Katika mambo yote ya kuongea rais kaona la kuongeza mke, tena kwa minajili ya ukabila wa kupendelea kabila lake, ndiyo muhimu?
Katika yote umeona hilo nalo ni la muhimu kulikomalia?

Hivi sasa hivi ni miaka 5 ya urais wake bado hamjamjua Magufuli utani wake?
 
Kwani hapo nilipopaona hapako kwenye habari? Magufuli hakusema hayo maneno?

Unataka kunichagulia wapi pa kuchangia?

Rais anatakiwa kuwa na maelezo yaliyonyooka pote.

Yeye ni kiongozi wa nchi.

Akisema maneno 99 yaliyonyooka, halafu neno moja la kipumbavu linalochochea ukabila na ku patronize Watanzania kama watu ambao wakipata hela wanawaza kuongeza wake tu, nitaona hilo neno moja aliloharibu ndilo la kumulika.

Mimi niliamua mapema kwamba sitagombea nafasi ya kisiasa, sasa nitamuonea Magufuli wivu kwa lipi wakati yeye si mshindani wangu?


Nitamuonea wivu nini a country bumpkin?
Kumbe wewe ndio mpumbavu sasa!
 
Rais Magufuli amempigia simu waziri wa madini Mh. Dotto Biteko na kumpongeza mchimbaji mdogo Samimu Laizer aliyeiuzia Serikali kipande kikubwa cha Tanzanite chenye thamani ya sh 7.8 bilioni.

Rais Magufuli amemtania Laizer kwa kusema sasa ataenda kuongeza mke na ikimpendeza aoe mwanamke wa kisukuma

Tukio la makabidhiano ya pande hilo kubwa la kihistoria la Tanzanite lilifanyika wilayani Simanjiro na mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Madini mh Biteko.

Pia alikuwepo Gavana wa benki kuu Prof. Luoga, Naibu Waziri wa Madini, Naibu Waziri wa Fedha, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro na DC wa Simanjiro mh Chaula aliyemwakilisha RC Mnyeti ambaye hakuwepo kwa sababu ya kupata dharura.

Tukio lilirushwa mubashara na TBC.

Pia soma > Mchimbaji aula kwa kupata mawe ya Tanzanite ya thamani ya Tsh Bilioni 7.8

Maendeleo hayana vyama!
Laizer ni meli kuanzia siku mingi tu, na hako kahela wala hakajamstua ,huyu jamaa shimo lake liko white geti pale mererani!
 
Magufuli ni mtu mmoja mshamba limbukeni.

Bado analimbuka.

Watu ambao wana ushamba limbukeni bado, masuala ya kuongezaongeza mke yapo sana mawazoni mwao.

Bado wanalimbuka na some basic things in life.
Mkuu usione wivu wewe ndio utakuwa mke wa pili wa huyo jamaa
 
Unaweza kuchomekea tu halafu hapi hapo ikazalisha mtoto.

Maneno yanaumba.

Maneno ya rais yanaumba mara milioni na milioni.

Magufuli anaelewa hili?

Watu wanamfuatilia kila analosema, dunia nzima. Wanaandika profile ya nchi kutokana na maneno yake.

Tayari kuna maneni huko kwamba Watanzania ni wavivu, wakevi, wakioata hela wanawaza kuongeza wake tu.

Sasa wanaoeneza maneno haya wanaoata nguvu kwa maneno ya Magufuli. Wanasema "Unaona, hata rais wao kasema hili".

Magufuli anaelewa maneno yake yana uzito sana?

Au anafikiri bado anaongea kwenye vijiwe vya Chato?
Naona umepanic kweli kwani wewe ndio mke wa huyo jamaa wa madini?
 
Alimuhonga hawara wake Kabula nyumba ya serikali, wakati Kabula hata hakuwa mfanyakazi stahiki wa serikali.

Siku hizo bado waziri.

Hakuanza leo shobo hizi za kilimbukeni.
Alimuhonga sababu kuna vitu anampa sasa na wewe kampe uhongwe nyumba
 
uyo ana miliki makarasha kibao
Sasa hawa jamaa wanavyotuambia mchimbaji mdogo wakati anamiliki Crushers kibao si wanatuona sie mazwazwa? Usikute kabla hata hajapata ilo jiwe account yake inaweza kuwa na zaidi ya 200m+ halafu wanatuambia mchimbaji mdogo,wachimbaji wadogo ni wale wa geita ambao msukuma aliowapiga maana wanatumia masululu kutafuta mawe.
 
Mkuu we utakuwa na tatizo! Tena kubwa!.. magufuli kalisema hilo kama utani tu then imekuwa ndo mada!!!!!
Ingekuwa kamlazimisha hapo ndio tungesema kakosea lkn kwa hili kweli kazi ipo kuja kumuelewa huyu mtu dah!..
Punguzeni sana kuwa serious kwa kila kitu vitu vyengine ni utani tu wa kikabila.
Huyo jamaa ni Chadema....... Wao hukomalia vitu vidogo vidogo tu!
 
Back
Top Bottom