Rais Magufuli ampongeza Diamond Platnum kwa kuchaguliwa kutumbuiza Kombe la Dunia

tatum

JF-Expert Member
Jan 16, 2018
5,786
4,490
Diamond Platnumz akiongea na Times FM 100.5fm amesema Rais Magufuli alimpigia simu kumpongeza kwa kuchaguliwa kwenda kutumbuiza katika Kombe la Dunia huko Urusi mwezi wa June.

Na yeye Diamond anajipanga kabla ya kuondoka kwenda Ikulu kumuaga Mh Rais Magufuli ili kupata baraka zote za watanzania.
 
Hongera kwake, Kijana anajituma, pamoja na mapungufu aliyonayo Kama Kijana yeyote anayechipukia, akiingia kwenye kazi anaitendea haki. Hili ni funzo kwa wengine badala ya kumponda au kuibua ugomvi Usio na maana, sasa waibue ushindani WA ubora kikazi.
 
Diamond Platnumz akiongea na Times FM 100.5fm amesema Rais Magufuli alimpigia simu kumpongeza kwa kuchaguliwa kwenda kutumbuiza katika Kombe la Dunia huko Urusi mwezi wa June.

Na yeye Diamond anajipanga kabla ya kuondoka kwenda Ikulu kumuaga Mh Rais Magufuli ili kupata baraka zote za watanzania.
Wajanja wanapata fursa Kimataifa, wengine wakikalia siasa na maandamano,
Pongezi nyingi kwako Diamond
 
Mbona na mimi nimegiwa simu na mh. Rais niongozane nae kwenda Urusikuona kombe la dunia lakini niko kimyaaa. Siropoki. Laiti ingekua Mshana jr. JF pangechimbika leo
 
Rais ameona nyimbo mpya ya dimondi au baada ya kusifiwa na dai ataikaushia maana mzee ukimsifia tu bac
 
Usisasahau kuimba wimbo wa Taifa.
Una ujumbe mzuri kwa mataifa ya nje ili waige mambo yetu.
 
hata alikiba leo amepigiwa simu na magufuli ,kumpongeza wimbo wa seduce me, as hit song ,,,sema alikiba hapend show off kama domooo
Sema showoff zinasaidia si unaona mwenzake amealikwa kutumbuiza urusi kombe la dunia
 
Diamond Platnumz akiongea na Times FM 100.5fm amesema Rais Magufuli alimpigia simu kumpongeza kwa kuchaguliwa kwenda kutumbuiza katika Kombe la Dunia huko Urusi mwezi wa June.

Na yeye Diamond anajipanga kabla ya kuondoka kwenda Ikulu kumuaga Mh Rais Magufuli ili kupata baraka zote za watanzania.
Wakati wake mwache atambe na hongera zake sana
 
Back
Top Bottom