MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,975
Rais wa Chad, Idriss Déby awasili nchini kwa ziara ya siku mbili ya kikazi. Rais Deby amepokelewa na mwenyeji wake Rais John Magufuli.
Ikumbukwe kuna tofauti kati ya ziara ya kikazi na ziara ya kiserikali.
Ziara ya kiserikali ni pale Rais wa nchi anapomkaribisha Rais wa nchi nyingine kwa mazungumzo ya kiserikali huku gharama zake zikilipwa na serikali iliyomkaribisha. Dhifa ya taifa hufanyika, wimbo wa taifa huimbwa na mizinga hupigwa.
Ziara ya kikazi mara nyingi Rais anayekuja huwa ameomba kuja au kwa maana nyingine amejikaribisha mwenyewe kwa ajili ya mazungumzo ya kiserikali na gharama za safari anajilipia yeye mwenyewe. Hakuna dhifa ya kitaifa au kupigiwa mizinga.