Rais Magufuli ampa RC Makonda ruhusa ya kwenda Misri leo kuhakikisha Taifa Stars inashinda mechi zilizobaki

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,898
141,829
Rais Magufuli amekubali ombi la RC Makonda kwenda Cairo Misri kuiongezea hamasa Taifa stars.
Dr Magufuli amewataka wachezaji wa timu ya taifa kutokatishwa tamaa na matokeo ya juzi dhidi ya Senegal kwani walicheza na timu namba moja kwa ubora barani Afrika.

Source TBC

My take; Nakubaliana na Rais Magufuli kuwatia moyo wachezaji tofauti na wale akina Nkamia wanaomkejeli Jemedari katikati ya vita!
 
Rais Magufuli amekubali ombi la RC Makonda kwenda Cairo Misri kuiongezea hamasa Taifa stars.

Source TBC
Rubbish, Mungu abariki kazi ya Makonda ????? Huyo Mungu wa Chato si Mungu wa Mbinguni! Inshallah ifungwe tena bao 4-0
Prelude: Inshallah wamefungwa 3-2. Mungu hawezi kubariki matendo ya shetani. Mungu wa mbinguni hayuko na mashetani labda wa Chato!
 
Tusidanganyane Watanzania,wenye wachezaji bora ndio tayari timu zao zimeshinda mie siamini kama Hamasa itafanya maajabu Misri,hata tungeenda nusu ya Watanzania bila uwekezaji mkubwa kwenye Timu zetu tutakuwa Wasindikizaji.Mpira ni Fedha sio Siasa na Makelele.
 
Usiwe na haraka mkuu!
 
Back
Top Bottom