Rais Magufuli amlipia Tsh milioni 5 mama aliyefiwa na mama mzazi Hospitali ya Muhimbili

Uchumi ukiwekwa vizuri hakutokuwa na haja kusubiri kumwomba raid misaada midogo midogo. Hali ni ngumu na watu wanaamini raid ndiye mwenyepesa za kugawa,mbona kwa kikwete haikukithiri? Nivile alijitahidi kujengea wananchi uwezo wa kumudu gharama zao!!
Kwa miaka mitano hii hakuna tajiri aliyetengenezwa hata mmoja sana tumewapoteza kadhaa...uchumi huchagizwa na matajiri ambamo maskini nao hujipatia riziki humo! Leo viongozi ndiyo watoa misaada? Kina bashite ndio wenyefedha? Hatukosawa
 
Mkuu bima ya afya kwa sasa ni dhahabu haswa kwa hospitali za hapa mjini. Ila huko mikoan ndio watu wa bima hufanyiwa fitina mno
Bima ya afya ipo, ila wanaoteseka kwenye matibabu katika hospitali zetu ni hao wenye bima za afya. Ukiwa na bima ya afya hata huduma unapata kwa shida mno. Anayeangaliwa vyema ni mwenye fedha cash kwanza. Kumbuka gharama za matibabu ni kubwa kiasi kwamba hata hiyo bima inavuka. Ila ukisikia kwenye majukwaa ya siasa yaliyojaa propaganda, unaweza ukatamani uumwe ili uende hospitali na ww ukaonje keki ya taifa.

Cha muhimu mbali ya hiyo bima ya afya ambayo ni jambo jema, ni vyema kushusha gharama za matibabu, wangalau kunaweza kusaidia. Maana kwa huu ugumu wa maisha ukipata mgonjwa anayekuhusu inakuwa kama kupaka chumvi kwenye kidonda. Tatizo kubwa kwenye hili jambo, watunga sera hawaishi maisha halisi kwani wengi vipato vyao vinazidi milioni moja kwa mwezi, hivyo wanamudu hata gharama za juu. Kwa vyovyote hawawezi kulipa uzito unaostahili.
 
Ni kweli,swala ni mfumo mzima uangaliwe upya,kama hiyo ni hospital ya nchi ambayo ni jicho la nchi ipo hivyo ,je huko mikoani?
Hapo mheshimiwa amepata hali halisi,Na bahati amewalipia majeruhi matibabu,wengine wasingetoka kwa kushindwa kulipa gharama
 
Movie ya kisukuma. Wengine wote wameondolewa akabaki huyo mgonjwa wa kuchongwa halafu umati wote umesogea kuconcetrate kwa huyo feki. Haya tengenezeni nyingine . Kosa la Rais wangu ni kuongoza kama anafanya kampeni miaka yote. It’s time to be the President. Yaani demu ushaoa unaendelea kutongoza tuuu badala ya kuchapa mashine.
 
Kweli kabisa, mimi binafsi huwa najiuliza sana hivi unawezaje kumchaji maiti au unataka kuongeza maumivu na majonzi kwa wafiwa? Hili lazima liangaliwe upya na sio maiti tu hata gharama za matibabu zishushwe kabisa mahospitalini maana watu wengi wanafia mahospitalini kwa sababu ya gharama kubwa za matibabu. Serikali ambayo ina dhamana juu ya wananchi wake na inasifika kwa usikivu iliangalie upya hili badala ya kuongeza nguvu katika ujenzi wa miundombinu na vitu vingine nguvu kubwa iwekwe kwenye afya za wananchi na chakula pia na sekta ya elimu.
Kutunza mwili usioze ni gharama kubwa
 
Daah mh Raisi ana wakati mgumu sana Tumuombee sana, shida zooote analiliwa yeye, ningeomba wakuu wa mikoa Na wilaya mjiataidi angalau mumpunguzie baadhi ya majukum.

Pia mh Raisi tufanye maboresho ya gharama kubwa za kukomboa ndugu zetu baada ya kufariki, Huwa Ni gharama sana hususani kwa mgonjwa aliyekaa muda mrefu, inagharrimu hadi familia kuuza mashamba au nyumba kukomboa ndugu zetu,

La mwisho viongozi wanaokwenda mahosipitali Kama akina Jeri muro waige UNYENYEKEVU wa MH RAISI, sio kuenda kisiasa. Wahakikishe wanafuata utaratibu wa namna mkuu wa nchi anavofika, Na kufanya sio kuropokaropoka Na kutishia watoa huduma.
Viongozi Kama jery mtembelee mahosipitali mchana Na sio kuvizia usiku.


TUWAOMBEE VIONGOZI WENYE KUJALI NA KUJUMUIKA NASI KATIKA SHIDA ZA KIBINADAMU TUKIANZA NA MH RAISI.
 
Hao walinzi walimuacha huyo mama wakati wanajua rais anapita? Kama hawakumpanga basi wana hatarisha usalama wa rais, kama angekuwa amejitoa mhanga je?

CCM B acheni kucheza na akili za watu.
Na mm nimewaza hivyo hivyo, wale walinzi mbona wanakuwaga wakali sana hawataki mtu apite mbele ya rais, sasa yule mama alitoka wapi
 
Hali ni mbaya na ngumu sana kila sehemu, hakuna cha kujivunia hapo.
Nilimlipia mgonjwa milion 2. Ambaye hana uwezo hata wa elfu 10 tu. anatokea kijijini kwetu.
Walibaki na mgonjwa kama mfungwa hapo mpaka wapate hela walioitaja. Nilimhurumia sana.
Nchi imekua ya hovyo sana hii kwa sasa.
Sasa unajinadi au
 
Hiki kibabu hakionekanagi kwenye misiba mizito..
non tanzanian's character
I feel shy for a wizard to be called my presideee..
Ngoja nikajifiche wasije wakaniteka sikukuu.
 
Rais wetu na pia ni ' Chief Comforter'. Kutokana na hali anayokutanayo sehemu yoyote ile inampasa pia kuguswa kwa kipekee na baadhi ya mambo. Hata kama hawezi kumfikia kila mtu na kumpa msaada kila mtu, lakini yale yanayomjia mbele ya macho yake, kama binadamu anayeguswa na adha mbalimbali za maisha inampasa pia kuonyesha matendo ya kiutu na huruma.
 
Back
Top Bottom