Rais Magufuli amlipia Tsh milioni 5 mama aliyefiwa na mama mzazi Hospitali ya Muhimbili

Alimtosa jamaa bandari kumpa hela ahahaha never mind

Magu anafanya vizur lkn kwa njia sio nzur kuna watu wanashida tz hii na niwengi kwa pale ningempenda zaid angelitolea swala lile kwa ujumla kuwa wafiwa wasidaiwe hela ya matibabu ya marehemu angesaidia wengi sana ila njia ile alifanya yesu alipokua na msafara na mitume wake
 
Hakuna binadamu asiye na huruma kusema kweli Magufuli ana huruma kwenye mikutano yake yote anayofanya,hakuna mwananchi aliye mlilia shida akamwngusha hayupo.


Lazima afanye hivyo, kwani huoni 2020 hiyoooo inakuja!!🤣
 
sasa gharama zitashuka vipi wakati serikali inachota hela za kwenye bajeti ya afya inaenda kununulia bombardiers hospitals zinaachwa tupu, hivyo inazilazimu kukamuwa wagojwa na ndugu zao ili angarau ziendelea kuwa wazi.
Hivi umeshawahi kujiuliza gharama za hospitali zote za serikali zinatoka wapi? Kuanzia kununua madawa, gharama za kiofisi hadi kulipa mishahara ya wahudumu wote? Au mnadhani hela za hazina hua zinashuka koyoka mpinguni?
 
msisitizo uwe kwenye bima ya afya kwa kila mtu...

Bima ya afya ipo, ila wanaoteseka kwenye matibabu katika hospitali zetu ni hao wenye bima za afya. Ukiwa na bima ya afya hata huduma unapata kwa shida mno. Anayeangaliwa vyema ni mwenye fedha cash kwanza. Kumbuka gharama za matibabu ni kubwa kiasi kwamba hata hiyo bima inavuka. Ila ukisikia kwenye majukwaa ya siasa yaliyojaa propaganda, unaweza ukatamani uumwe ili uende hospitali na ww ukaonje keki ya taifa.

Cha muhimu mbali ya hiyo bima ya afya ambayo ni jambo jema, ni vyema kushusha gharama za matibabu, wangalau kunaweza kusaidia. Maana kwa huu ugumu wa maisha ukipata mgonjwa anayekuhusu inakuwa kama kupaka chumvi kwenye kidonda. Tatizo kubwa kwenye hili jambo, watunga sera hawaishi maisha halisi kwani wengi vipato vyao vinazidi milioni moja kwa mwezi, hivyo wanamudu hata gharama za juu. Kwa vyovyote hawawezi kulipa uzito unaostahili.
 
Hilo la kutengeneza hilo tukio kwa huyo jamaa ni mambo ya kawaida. Zaidi ya 95% ya hao watu wanaojifanya kumlilia huyo jamaa kisha kujifanya anatatua tatizo husika huwa ni mambo ya kupanga.
Hao walinzi walimuacha huyo mama wakati wanajua rais anapita? Kama hawakumpanga basi wana hatarisha usalama wa rais, kama angekuwa amejitoa mhanga je?

CCM B acheni kucheza na akili za watu.
 
Back
Top Bottom