Rais Magufuli amlipia Peter Msigwa Tsh. Milioni 38 ili atoke gerezani, CHADEMA wadai wameshamlipia Mil 40

LIMBOMAMBOMA

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
8,094
2,000
Haahaa jpm noma, katuma gari za ikulu kumtoa msigwa, ila chadema nimewavulia kofia.Political strategies Wa chadema nampa big up.Chadema wanapiga mziki huku ccm wakisakata duh...wale walioponda uchangiaji wanajisikiaje sasa.
 
MasterP.

JF-Expert Member
Jun 5, 2013
6,986
2,000
binafsi sioni kama kuna tatizo kwa Joni kumtolea Rev.Msigwa hiyo faini.....tangu mwanzo dada Mange alisema hii michango haina "uchama"!!!yeye Joni kama kaguswa na harakati za raia wema tunaowachangia ndugu zetu sioni ubaya wowote......unafiki wa wa baadhi ya wanaCCM ndio tatizo.
Ni kweli kabisa ila anayeongoza kwa unafiki nchi hii ni huyo aliyetoa hizo 38m...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Oumuamua

JF-Expert Member
Dec 26, 2018
1,018
2,000
Ila kuna baadhi ya binadamu hawana aibu aisee. Yaani wametafuta macamera na wanahabari kututangazia haya! Kokote kwenye harufu ya umaarufu na misifa wanataka wawepo!
Wanataka ku-trend yaani, na wao wasikike hata kama ndio chanzo cha mateso ya wenzao. Kuna waafrika wenzetu wana roho mbaya sana halafu wanafiki.
 
Mr.Junior

JF-Expert Member
Sep 8, 2013
10,340
2,000
😂😂😂ni kujibaraguza huko, nafikiri dhamira inamsuta. Inabidi Rais atueleze hizo fedha zimetoka wapi? Mapenzi hayo ya 'udugu' yametokea wapi? Angeonyesha wema kwa kuwalipia wote bila kubagua...au hata angechangia tu kama wananchi wa kawaida wanavyofanya bila kujali nani atatoka na nani atabaki alimradi nia ikiwa kuwatoa wote. Rejesheni hizo fedha serikalini.
Humu ndani raia mnajitoa ufahamu.

Ndugu wa Msigwa wameenda kuomba wamesaidiwa hao wengine hawajaomba.

Ufuasi wa vyama vya siasa siku hizi unakuwa sumu watu akili zinawatoka.
 
komamgo

JF-Expert Member
Sep 14, 2012
1,658
2,000
Chadema payment time 14hr Magufuli payment time 3hr. Ni wazi Chadema wamechelewa kulipia . waliposikia Pesa imetolewa wakakkurupuka kwenda bank.
 
Trinity

JF-Expert Member
Jul 20, 2017
498
1,000
Upendo ulioje? JPM amlipia Msigwa mil 38 kati ya mil 40.

Taarifa zaidi inakuja

====

Rais wa Tanzania, John Magufuli amemlipia Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa faini ya Sh38 milioni kati ya Tsh 40 milioni anazotakiwa kulipa mbunge huyo ili atoke jela.

Baada ya ndugu kuchangishana na kupata Milioni 2, ikabidi wamfuata rais Magufuli kama mwanafamilia naye achangie. Mtoto wa Dada yake Msigwa(Mpwa wa Msigwa) amemuoa Mtoto wa Rais Magufuli.

Msemaji wa Ikulu Gerson Msigwa amesema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya ndugu kuchanga na kupata milioni mbili tu na hivyo kumtafuta Magufuli kupata msaada.

Ambao bado wapo katika gereza la Segerea ni Mbowe(Mbunge wa Hai), John Heche (Tarime Vijijini), John Mnyika (Kibamba), naibu katibu mkuu wa chama hicho-Zanzibar, Salum Mwalimu na Mchungaji Msigwa.

Wakati huo huo, CHADEMA wanadai wameshamlipia faini Mchungaji Msigwa Milioni Arobaini.

"Sisi kama chama tumelipa Sh100 milioni ya watu watatu ambao ni Peter Msigwa, John Mnyika na Salum Mwalimu na tumewalipia kupitia benki tawi la Azikiwe.

Tumeshapeleka malipo mahakamani, tunasubiri risiti za mahakama. Kama kuna mwingine amemlipia Mchungaji Msigwa hatuna ushahidi na uhakika nao, kama chama mahakama haijaturejeshea fedha za Msigwa kwamba kalipiwa mara mbili.” Amesema John Mrema.
View attachment 1385706
View attachment 1385707
View attachment 1385840 View attachment 1385841
View attachment 1385694

Pia soma:
1). Mahakama ya Kisutu imewatia hatiani Viongozi wa CHADEMA na kuwahukumu kulipa faini ya Tsh. Milioni 350 au kwenda jela, Wapelekwa Segerea

2). Rais Magufuli akizungumza jambo na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wakati akitoka kutoa heshima za mwisho kwa Dada wa Mch. Peter Msigwa
Nimefrai sana kulipiwa jembe letu liludi, jera sio kuzuri by Uncle shivo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
18,915

Haya ndio yale matumizi ya dola aliyosema Bashiru au hamkumuelewa....
 
LIMBOMAMBOMA

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
8,094
2,000
Chadema payment time 14hr Magufuli payment time 3hr. Ni wazi Chadema wamechelewa kulipia . waliposikia Pesa imetolewa wakakkurupuka kwenda bank.
Mkuu, walioanza Ni chadema.Rais kalipa online, Na walitumwa watu Wa ikulu wakiwa Na msemaji wa ikulu mahakamani kuchukua removal order, nani mwenye ubavu Wa kukataa agizo LA rais pale kisutu?
 
Mkongwe Mzoefu

JF-Expert Member
Aug 10, 2018
813
1,000
Walitaka kutumia undugu wa Magufuli na Msigwa kujifanya wanamlipia huku tayari wameshaanza kutangaza kumbe tayari Msigwa na wenzake wawili tayari wameshalipiwa.
Hii ni aibu kubwa sana kwa chama tawala na hata Mwenyekiti wao aliye andaa magari kumfuata Segerea na waandishi wa TV kisha Msigwa kukataa kupanda na kuondoka na wakili wake.
Hakika hii in AIBU KUBWA
IMG_20200312_170759.jpeg
IMG_20200312_175052.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
16,728
2,000
Show ya chama fulani kutumia 'michango' kama ngazi ya kisiasa ya 'buma'. Ha ha haaa! Siasa aisee...!!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom