Rais Magufuli amfananisha Museveni na Mwalimu Nyerere. Je hii ni sawa?

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,330
4,114
Katika pita pita ya hapa na pale nimekutana na twiti ya mtu mmoja akiwa amemnukuu rais wetu JPM akimsifia mseven kuwa kama nyerere baba wa Taifa letu. Heshima aliyo nayo nyerere kwa watanzania walio wengi ni kubwa sana. Sijui kama wana JF tunakubaliana na hoja hii kwamba tukimwona Mseven tuwe kama tumemwona nyerere.

Hii kauli angekua ameongea raia wa kawaida binafsi ningemwambia atuombe radhi watanzania. Nyerere kumfananisha na watu wa ajabu ajabu si sawa. Ila kwa vile kaongea raia namba moja. Ngoja niweke akiba ya maneno ila nimekelwa sana ila sina namna kuwakilisha hisia zangu kwa ninavyo mfahamu Mseven harafu nimfananishe na Mwalimu Nyerere

F94E9EBA-EF6C-4E4C-AB90-DBFC05E56101.jpeg
 
Mara nyingi ukitaka kitu kizuri kutoka hata kwa rafiki yako lazima umpe sifa hata asizokuwa nazo ilimradi ufanikishe lengo lako zuri.
 
Bavicha wanatatizo la kuwa na kumbukumbu fupi. Si ndio nyie mlikua mnatuambia kuwa Lema ni Mandela wa Tanzania au mlikua mnatania??
 
Back
Top Bottom