Victor Yohana
Member
- Apr 30, 2013
- 31
- 31
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli mapema leo ameweka jiwe la Msingi katika mradi wa ujenzi wa Barabara ya Mpemba-Isongole na kuweka jiwe la Msingi katika ujenzi wa hospitali ya Mji wa Tunduma ikiwa ni siku ya Pili ya ziara yake Mkoa wa Songwe
Barabara ya Mpemba-Isongole inajengwa Kwa kiwango cha lami Kwa fedha za Serikali bilioni 109 ambapo inatarajiwa kukamilika Septemba 2020 na itaunganisha Mkoa wa Songwe na nchi ya Malawi.
Aidha katika Mradi wa ujenzi wa hospitali ya Mji wa Tunduma yenye hadhi ya Wilaya serikali imekwishatoa bilioni 2.5 huku Mkuu Wa Mkoa Wa Songwe Brig Jen Nicodemus Mwangela amemuomba Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli kiasi cha shilingi bilioni 2.4 ili kukamilisha awamu ya kwanza ya ujenzi Wa hospitali hiyo