Rais Magufuli amewateua aliyekuwa IGP, Mangu kuwa Balozi nchini Rwanda na Meja Jenerai Mstaafu, Mumwi Balozi Urusi

Mkuu ungejua muundo wa serikali ungeona kuwa igp yuko chini ya waziri wa mambo ya ndani,na balozi yupo chini ya waziri wa mambo ya nje.
Hivyo hakuna kilichoharibika hapo.
Zamani kidogo mwalimu nyerere alimshusha cheo mzee kawawa kutoka waziri mkuu na makamu wa pili wa rais,kuwa waziri wa ulinzi,tena kibaya zaidi mwalimu alimwambia kawawa kuwa anataka kumbadilisha,yeye kawawa anaona mtu gani anafaa kwa kazi.
Mzee kawawa bila kinyongo akampendeza sokoine kwenye nafasi yake.Hivyo inategemea wewe unaichukuliaje hiyo changamoto mpya.

Aise. Kawawa kumbe alikuwa jasiri hivyo?Excellent.
 
Akina abdurahman shimbo aliyekuwa mnadhimu mkuu wa jeshi kapewa ubalozi ,vp huyo major jenerali amedhalilishwa nae sembuse igp
.
Unavyoona igp ndio cheo kikubwa ,halafu hawa waliohudumu vyombo vya ulinzi na usalama huteuliwa sana kuwa mabalozi ujasusi unahusika

Hajashushwa hadhi
Shimbo alishastahafu jeshi,ila Mangu bado ajastaafu
 
Kagame alikuwa kwa muda mrefu hamtaki kabisa shushushu mzoefu ALI SIWA
Naona kaamua kumuondolea
Kikwete alipomteuwa SIWA ilichukua miaka miwili kumpitisha haikua kawaida
 
Akina abdurahman shimbo aliyekuwa mnadhimu mkuu wa jeshi kapewa ubalozi ,vp huyo major jenerali amedhalilishwa nae sembuse igp
.
Unavyoona igp ndio cheo kikubwa ,halafu hawa waliohudumu vyombo vya ulinzi na usalama huteuliwa sana kuwa mabalozi ujasusi unahusika

Hajashushwa hadhi

Jeshini IGP anaweza kuwa kama equivalent na Major General kwakua Police kwenye formation ni kama jeshi la akiba na ikitokea vita automatically linakuwa ni COMMAND Chini ya Reserve Force na kimsingi command inaongozwa na major general .. tuna command zifuatazo

Air Force Command
Land Force Command
Navy Command
National Service Command
Reserve Force Command
1.retirees from all forces
2.mgambo
3.vikosi-Znz
4.police ,Magereza , fire , rangers etc
5. Volunteers ( WANANCHI )
Na ndio concept ya JESHI LA WANANCHI Hilo ni neno zito Sana na falsafa ya jeshi ni hotuba ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambayo wanajeshi wote huisoma
Mfano alisema “ ... jeshi hili ninalounda halitatumika kuwakandamiza wananchi , kuwapiga bali ni jeshi lao wenyewe la kupambana na aduii”

Kwa falsafa hiyo ndio maana kuna wakati yalitokea maandamano makubwa Sana Wanasiasa wakamuambia Mkuu wa Majeshi awaingize askari mjini “ alikataaa” na mfumo aliotumia ni kuwaingiza askari bila Sare ili tu kufanya silent monitoring na akawagiza police wasifanye any provocation .. kwenye yale maandamano siku ile kulikua na wnaajeshi kama 5000 wamevaaa kiraia

Pia kuna wakati alilazimishwa kuingiza askari mjini kukabiliana na waislamu kulikua na mgogoro fulani alikubali Kwa Sharti kuwa ataingiza askari wasiokuwa na silaha yeyote na hawatashuka kwenye magari na alifanikiwa walitiii wakaondoka

Kwa falsafa ya TPDF ni Mwiko kwao kuchukua silaha kabisa kupigana na Raia ni kinyume na falsafa yake

Mwalimu alijenga kujenga jeshi la wananchi kwa maana wajisikie wanalimiliki, walipende na wawe tayari muda wowote Kulifia “tuwe na jeshi dogo la makamanda maafisa na wataalamu halafu tutawekeza kwa wananchi , kila mtanzania ni mwanajeshi”
Sera inafanya formation yetu ya kimapigano kuwa na hadi wapiganajiil milioni 10 au zaidi ambao muda wowote wanaweza kuongoZwa na makamanda na maofisa na wakapigana
Hivyo kitendo chochote kinachoweza kufitinisha Jeshi la wananchi na wamiliki wake hao wananchi ni kama uhaini na kinaweza kuhitaji maximum punishment
 
Akina abdurahman shimbo aliyekuwa mnadhimu mkuu wa jeshi kapewa ubalozi ,vp huyo major jenerali amedhalilishwa nae sembuse igp
.
Unavyoona igp ndio cheo kikubwa ,halafu hawa waliohudumu vyombo vya ulinzi na usalama huteuliwa sana kuwa mabalozi ujasusi unahusika

Hajashushwa hadhi

Hakuna cha ujasusi wala nini hapo
 
Mh. Dr.Ahmed salim alipewa ubalozi wa Tz huko Misri akiwa na miaka 26,so it is possible mkuu.
Masahihisho kidogo

Dr.salim aliteuliwa kuwa balozi wa misri akiwa kijana mdogo wa miaka 22 tu (1964).

Ila zama na watu wamebadilika vijana wa sasa hivi mtihani kweli tazama tu viongozi wetu hasa vijana wanavyo vurunda na kufanya kazi pasipo na weledi na umakini.
 
Mimi nashindwa kuelewa pale wastaafu kama huyo Meja Jenerali kupata tena ajira ktk utumishi wa umma kama Ubalozi. Tunalia kuwa hakuna ajira na maelfu ya vijana hawana kazi, anachukuliwa mtu aliyefanya kazi miaka 20 na zaidi na kustaafu kwa lazima anapofikisha miaka 60 halafu unamuajiri tena wakati alipaswa kupumzika na kula pensheni yake.

Ktk hali bado watawala wanategemea kuwa vijana wataendelea kuwaunga mkono wakati nafasi zao za ajira wanapewa babu zao?

Vv
.
mkuu kna vitu vingne inabidi tukubali vipo beyond our thinking capacity km haupo ''inside'', leo kijana umpe hicho cheo ni kumtaftia mabalaa na kujtakia kuichafua nchi, hao hawaendi kushnda kusoma magazet km weng wanavyosema, 'intelligence' issue hizi mkuu
 
Ok. Kwa maana hiyo tukubali kuwa hatuwaandai vijana wetu kuwa responsible kwao wenyewe na kwa taifa. Hao wastaafu tunaowang'ang'ania ni wazi kuwa waliandaliwa. Tunawaandaa zaidi vijana kuwa makada na watetezi wa siasa za hovyo za vyama vyetu vya siasa na kuwafanya nyumbu wa kutetea kila jambo hata la kipuuzi kwa sababu tu limesemwa na kiongpzi au limesemwa na chama chao cha siasa.

Ndio maana haishangazi leo ukitoa maoni tofauti na kiongpzi wa chama wanachokiunga mkono, utaandamwa kwa kashfa. Ukitoa maoni dhidi ya Chadema, Bavicha watakuandama, ukitoa maoni dhidi ya CCM, UVCCM watakutolea kashfa za ajabu, na ukisema dhidi ya CUF, UviCUF watakumaliza. Mfumo umewafanya vijana kuwa waumini wa itikadi na maoni ya vyama vyao. Wako tayari kuteka na kuua yeyote anayepinga viongozi wao.

Vv
 
Masahihisho kidogo

Dr.salim aliteuliwa kuwa balozi wa misri akiwa kijana mdogo wa miaka 22 tu (1964).

Ila zama na watu wamebadilika vijana wa sasa hivi mtihani kweli tazama tu viongozi wetu hasa vijana wanavyo vurunda na kufanya kazi pasipo na weledi na umakini.
Daah 22 yrs kwa kijana wa sasa hivi anakua anajua habari za Zari,Mange na kubet full stop.
 
.
mkuu kna vitu vingne inabidi tukubali vipo beyond our thinking capacity km haupo ''inside'', leo kijana umpe hicho cheo ni kumtaftia mabalaa na kujtakia kuichafua nchi, hao hawaendi kushnda kusoma magazet km weng wanavyosema, 'intelligence' issue hizi mkuu
Mbona Dr. Salim alipewa ubalozi akiwa na miaka 22 tu.
 
Back
Top Bottom