Rais Magufuli amewateua aliyekuwa IGP, Mangu kuwa Balozi nchini Rwanda na Meja Jenerai Mstaafu, Mumwi Balozi Urusi

Hivi uteuzi huu ni kwa ajili kujiandaa kiulinzi? kufutana machozi au ni kwa ajili ya diplomasia ya uchumi kama wanavyojinadi?

mwenzenu naona nyota tu
 
Daah 22 yrs kwa kijana wa sasa hivi anakua anajua habari za Zari,Mange na kubet full stop.
Kwenye hotuba moja rais Thabo Mbeki aliwahi kusema "......wakati nasikia kijana wa kitanzania wa miaka 22 anateuliwa kuwa balozi nilishangaa sana na kuona jambo lisilofaa na kudharau sana ila siku nilipokutana kwa mara ya kwanza na kijana huyo (dr.salim ahmed salim) wakati huo akiwa akiwa waziri nilijiona mie mjinga na kuona mtazamo wangu haukua sahihi.
Dr salim kwa hakika alistahili kabisa kwa nafasi hiyo ....anamalizia kusema Rais Mbeki......"
 
Very impressive,unadhani nini kinafanya Kijana wa zamami awe na maono kuliko wa sasa?

Wkt kijana wa sasa ana technologia mkononi mwake na anaweza kujua na kupata exposure sana kuliko hata wale wa zamani?
 
Taarifa iliyotolewa leo Jumanne Machi 20, 2018 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi imesema Mkuu wa Jeshi la Polisi wa zamani, IGP Ernest Mangu ataapishwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Rwanda na Meja Jenerali mstaafu Simon Mumwi kuwa balozi wa Tanzania huko Russia.

Hafla ya kuapishwa kwa mabalozi hao wateule itafanyika Ikulu Dar es Salaam kuanzia saa 5 asubuhi.

Jamani. Meja Jenerali Rt Mumwi asisahau kuhangaikia yale Madola ya Mzee wetu Dr. Shika.Anaweza kuwa mwekezaji atakayetutoa kwenye shida.
 
Back
Top Bottom