G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,596
- 36,018
Hiyo ndiyo hasa maana ya kile rais Magufuli alichofanya kwa wafanya biashara wa sukari nchini. Ingawa ni kweli kuwa rais Magufuli hapendi kabisa kuchezewa na yupo tayari kwa lolote wakati wowote.
Alichokifanya rais Magufuli kinaweza hata kuwatisha wafanya biashara wengine wa ndani na nje. Ingawa hatuungi mkono yale tunayofanyiwa ya ajabu na wafanya biashara hao. Huenda tukapata madhara makubwa mbeleni na uchumi wetu kuendelea kuteketea.
Ni lazima tukae mezani tujiulize ni kwanini wameamua kufanya hivi huku ikiwa siyo hali ya kawaida kabisa. Pengine wafanya biashara hao wana hoja ni kwa nini wamefikia hapa.
Hakuna nchi yoyote duniani iliyoendelea kwa kuanzisha migogoro na wafanya biashara. Marekani inaweza kuanguka kiuchumi na kuwa nchi dhoofu sana kuliko hata Zimbabwe ndani ya muda mfupi sana kama itaamua kuanzisha migogoro na kina Bill gate na wengine! Uingereza imeendelea baada ya kuwekezwa na hao wafanya biashara wakubwa duniani.
Juzi nilimsikia rais Magufuli akisema kuwa "kuichezea serikali yake ni sawa na kuchezea maisha yako" Baada ya hawa wafanya biashara kuingia mgogoro na serikali tusubiri matokeo.