Rais Magufuli amekuza GNI kwa wastani wa USD 80 kwa miaka mitano, mwaka 2005-2010 Kikwete aliikuza kwa wastani wa USD 220!

Sasa kama wewe una ukweli basi tuwekee data kamili ili tumpuuze mleta mada
Wewe ndo mjinga
Kati ya wewe, Magufuli na bank ya Dunia Nani anajua Mambo ya kupanda na kushuka kwa uchumi?

Kwani Rais Magufuli ndo katoa taarifa ya Tanzania kufikia uchumi wa Kati au ka qoute taarifa kutoka kwa WB?

Kijana Acha mihemuko Rais wa nchi hawezi kutweet Uongo Tena kuhusu bank ya Dunia kabisa alichokiandika ndo sahihi nayeye kafanya kuki qoute kutoka kwenye taarifa ya world bank.

Punguza chuki binafsi utakufa mapema.
 
Hizi takwimu zinaonyesha Magufuli ana perform below Standards kulinganisha na Kikwete.

Kikwete kila baada ya Mhula Mmoja alikuwa anaipandisha nchi hatua ndefu zaidi kwenye pato la mtu mmoja mmoja, Wakati Magufuli ndani ya miaka yake mitano kapiga hatua ndogo tu.

Sema kwa sababu Kikwete alikuwa amebakisha hatua ndogo sana ili tuingie uchumi wa kati, huyu kaja kaipiga hiyo hatua fupi tu basi sifa zinamwangukia yeye watu na watu hawakumbuki kuwa ni JK aliyekuza pato la nchi hii takriban mara mbili katika kipindi cha utawala wake hadi kuunyemelea huo uchumi wa kati!
Kumbe ccm inafanya Kaz vizur Sana et mana kikwete alipiga Kaz
 
Duh! World Bank wanazidiwa umakini na SACCOS ya Mbowe?
Watumie hizo data kamanda!
na hii pia ai attach
tapatalk_1593528776616.jpeg
 
Leo akina G Sam wamekalia full kupaparika, kudadadeki, WB hawajawahi kutamka sisi ni nchi ya uchumi wakati hapo kabla, Mwambie DJ Mbowe na muhuni Zitto kuwa WB leo wamesema sisi ni nchi ya uchumi wa 3
tapatalk_1593528776616.jpeg
 
Leo Jamii Forums hawana ujanja, habari ndio hiyo mtaumia sana mwaka huu, ila msitufungie tu mtandao kwa maana habari positive za TZ yetu ndio kwanza zimeanza kumininika, poleni sana, hahaha, we are rich bitch, ...

 
Kwenye siasa facts don't matter, ni emotions tu.

Headline hapo ni "World Bank wamesema tuko uchumi wa kati", mambo mengi hayo wanajua wasomi tu.

Ni kama tunavyoambiwa kila siku SGR tunajenga na hela zetu, mfuatiliaji anajua sio kweli maana tunaona Waziri wa fedha akitia saini mikopo lakini mwanakijiji huko Shinyanga vijijini mambo hayo hayajui.
 
Sisi tunamsifia alietikisa nyavu kwa bao la kideoni,wewe baki na mtu wako alietoa assist
Hii nchi kwa mwaka 2015 2020 hats angepewa MBWA ingefikia hilo pato. Ilikuwa imebaki dola 20 tu na angalia trend inayoenda kutoka mwaka 2000 ndipo utajua kuwa jiwe si lolote.
 
Kwenye siasa facts don't matter, ni emotions tu.

Headline hapo ni "World Bank wamesema tuko uchumi wa kati", mambo mengi hayo wanajua wasomi tu.

Ni kama tunavyoambiwa kila siku SGR tunajenga na hela zetu, mfuatiliaji anajua sio kweli maana tunaona Waziri wa fedha akitia saini mikopo lakini mwanakijiji huko Shinyanga vijijini mambo hayo hayajui.
Unajua tofauti ya mkopo na msaada?
 
Duh....!
Soma report hiyo WB kwanza.
Malengo yetu ni by 2025 tuwe kwenye uchumi wa kati. Hatujafika bado. WB wameiorodhesha TZ kwenye nchi zinazoingia kwenye uchumi mdogo wa kati(lower middle)
Nashangaa hata waziri wetu wa fedha Dr.Mpango ameshindwa kumwambia JPM Kwamba bado hatujafika uchumi wa kati!!
Tuko kwenye hatua nzuri kuelekea uchumi wa kati lakini tusiipotoshe report ya WB.
Bado hatujafika tunakotaka tufike, ndio tumeanza kukanyaga barabara ya kutufikisha huko.
 
Miaka 5 ipi ya Magufuri? maana 1020 ni mwaka 2018 based data, kwanini usiseme miaka mitatu? ukichukua hata data za mwaka 2019 ambapo GNI ni 1172 (Wikipedia) ongezeko ni 172 ukiadd hata hiyo mnayosema 80 or 54 utapata ni 0ngezeko la 226 kwa miaka minne tu ya JPM, punguzeni kupotosha na tutoe pongezi hata kwa hatua kidogo nchi imefikia bila kutafuta sababu ambazo hazina msingi, tuko ndani uchumi wa kati, ndani mbayaw sana hicho no muhimu.
 
Back
Top Bottom