Rais Magufuli amefanya uamuzi sahihi kwa wakati muafaka

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
SERIKALI ya awamu ya tano ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya Rais Dk. John Magufuli ni serikali iliyoonyesha historia kubwa na ya aina yake ndani ya chama na serikali kwa kufanya magumu mengi kwa masilahi ya watanzania na wanachama wa chama hicho japo wachache wameumia kwa faida ya wengi .

Ni wazi utendaji kazi wa Rais na mwenyekiti wa CCM Taifa Dk. Magufuli umekuwa wa aina yake na wenye kurejesha heshima kubwa kwa watumishi wa umma na viongozi wa CCM na wanachama wake kuona chama ni mali yao na sio mali ya wenye pesa na viongozi wachache kama ilivyokuwa awali kwa wenye pesa kuwa na sauti kuliko wenye chama chao.

Wapo mawaziri na viongozi waliokuwa wakiogopwa ndani ya chama na serikali kwa kusema chochote wakiamini kuwa wataendelea kudumu kwenye nafasi hizo daima na hata baadhi yao kuona wao ni bora zaidi ya wengine ila leo hii chini ya uongozi wa Rais na mwenyekiti wa CCM, Dk. Magufuli mwenye ndoto ya kuona Tanzania inakuwa ya watanzania na chama cha wanachama mwelekeo wa safari umeanza kuonekana na tunaweza sasa kukadilia masaa ya kumaliza safari yetu ndefu iliyoanzishwa na baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Nyerere .

Wengi wetu tumejikita katika maswali magumu kuliko majibu ama kuwa na majibu mepesi zaidi kuliko maswali kwa kuhoji safari yetu hii kuwa kutumbuliwa kwa viongozi mbali mbali CCM na serikali pia wenye vyeti feki na watumishi hewa kuna kwamisha uchaguzi ndani ya CCM ama kutafanikisha safari ya watanzania kuelekea Tanzania ya uchumi wa viwanda kwa kila mmoja kufaidi kipande cha mkate katika Taifa na sio kila mwenye pesa kula mkate mzima wa Taifa?

Maswali haya na mengine yanatokana na hali iliyokuwepo kabla ya Rais Magufuli kuingia Ikulu tulishuhudia hayo kwa matajiri kujaribu kuiyumbisha seriali na hata kujimilikisha chama huku wanyonge wakiwa watanzamaji na wapiga debe kwa wenye pesa zao kiasi hata mchakato wa kumpata mgombea Urais ndani ya CCM ulionekana kuwang’arisha wenye pesa na wasio na pesa walibaki kuvunjika mioyo katika safari hiyo baada ya kila wanapo pita kusaka wadhamini walijikuta wakikosa ushirikiano kwa viongozi wa CCM ama kuulizwa wanakiasi gani cha pesa kwa ajili ya kukutanishwa na wana CCM wa kuwadhamini kwa mkoa wa Iringa Rais Magufuli yeye hakuumiza kichwa baada ya kuona dalili hizo aliomba kupelekwa kata ya Magulilwa jimbo la Kalenga kutafuta udhamini wa wana CCM tofauti na wenye pesa walioandaliwa mjini Iringa .\

Ni wazi siku zote atakaye kusaidia huwezi kumtambua ila pindi utakaposaidiwa wakati wa uhitaji wako hapo ndipo huanza mapenzi ya kweli hakuna haja ya kutafuta majibu kwa maswali mepesi lakini ukweli kila mmoja anao ni nani aliyetegemea kuona watanzania tunaimba wimbo mmoja kama leo kwa kuwa wamoja na kwenye mambo ya kitaifa kama ilivyo leo baada ya mawaziri kutumbuliwa ?

James Mgego ni katibu wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) mkoa wa Iringa katika tamko la vijana juu ya utendaji kazi wa Rais Magufuli kwa kutengua uteuzi wa aliyekuwa waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo baada ya ripoti ya uchunguzi wa mchanga wa makinikia ya dhahabu anasema kuwa uamuzi ni sahihi na kataka mawaziri zaidi watakaohusishwa na ufisadi kutumbuliwa.

Mgego anasema vijana mkoani hapa wamepokea kwa mikono miwili uamuzi huo wa Rais wa kumuondoa waziri Prof Muhongo na kutaka mawaziri na viongozi wengine wa umma kuwajibika kwa faida ya umma na si vinginevyo.
“ Umoja wa vijana mkoa wa Iringa unaungana na kaimu katibu mkuu wa UVCCM Taifa, Shaka Hamdu Shaka kupongeza hatua iliyochukuliwa na Rais John Magufuli kwa hatua alizozichukua za kizalendo kwa maslahi ya watanzania kwa kutengua uteuzi wa waziri wa Nishati na madini ….Rais amefanya jambo zuri ambalo linapongezwa na kila mtanzania kwa faida ya vizazi vilivyopo na vijavyo “

Anasema kuwa Rais Magufuli amechukua uamuzi sahihi wakati sahihi kwani nchi ilikuwa ikipoteza raslimali nyingi kwa ajili ya kuwanufaisha wachache kwa maslahi yao wenyewe na sio jamii ya kitanzania .

Hivyo alisema kuwa umoja wa vijana wa CCM mkoa wa Iringa umeona ni vema kujitokeza mbele ya vyombo vya habari kupinga vikali vitendo vya rushwa na ufisadi ,dhuruma na wizi vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wasio wazalendo na Taifa.

Mgego anasema UVCCM mkoa wa Iringa haitasita kuwafichua wale wote ambao wanaikwamisha serikali kwa kufanya vitendo vya ufisadi ama dhuruma dhidi ya watanzania kwa kutumia nafasi zao za uongozi walizo pewa .
Aidha, alisema kwa kuwa ripoti ya pili ya kiuchunguzi dhidi ya mchanga huo wa madini inakuja ni vizuri wale wote waliohusika kwa namna moja ama nyingine kujitafakari na kuchukua hatua ya kujiuzulu nafasi walizopewa kabla ya kutumbuliwa na Rais.

Pia katibu huyo aliwataka vijana kuendelea kujitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi mbali mbali ndani ya chama hicho na kutowasikiliza mafisadi ambao wapo kuona CCM inakwama katika uchaguzi huo wa ndani ya chama.
Katibu wa UVCCM wilaya ya Iringa mjini Alphonce Muyinga anasema kuwa wanazo taarifa za wote wanaohujumu uchaguzi wa CCM mkoani Iringa na kuwa dawa yao inachemka kwani hawataona haya kuwashugulikia watu hao wanaotaka kukwamisha uchaguzi huo wa CCM.

Anasema baadhi ya viongozi ambao wametumbuliwa ndani ya chama katika wilaya ya Iringa mjini wamekuwa na kampeni kubwa ya kukwamisha zoezi la uchaguzi ndani ya chama kwa ngazi ya mashina na matawi kwa maeneo mengine kuwanunua wagombea wazuri ili wasigombee nafasi hizo japo baada ya kupata taarifa hizo vijana wamejipanga kuona uchaguzi huo unafanikiwa.

Anasema kuwa uchaguzi huo umepangwa kuanza kati ya Tarehe 4 -10 ya mwezi huu wa sita kwa kuanza kutoa fomu kwa wagombea wa kata hivyo wanaamini vijana wengi wenye sifa watajitokeza kuchukua fomu hizo.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Masenza ambae alialikwa katika zoezi hilo la utoaji wa tamko alipongeza hatua ya vijana hao kutambua kazi kubwa inayofanywa na Rais Magufuli na hata kutoa tamko hilo la pongezi .

Masenza anasema kuwa kumekuwepo na maombi kutoka kwa wananchi wa kawaida maeneo mbali mbali ya mkoa wa Iringa kuomba kufanya maandamano makubwa ya kumpongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya na maamuzi mbali mbali yenye lengo la kuwakomboa watanzania na kuwa hakuna kiongozi anaye zuia wao kukutana kutoa pongezi zao kwa Rais ila si kwa kuandamana mitaani.

“Mimi kama mkuu wa mkoa wa Iringa nawapongeza pia wananchi wangu ambao wametambua kazi nzuri inayofanywa na Rais wetu katika Taifa ….nawaomba sana wananchi wenye pongezi kwa rais ruksa kuzitoa ila utaratibu ambao wanapaswa kuutumia ni kukutana katika vikao vya ndani kama walivyofanya vijana wa CCM na sio kufanya maandamano mitaani”

Katibu wa CCM mkoa wa Iringa, Christopher Magala anasema uchaguzi unaendelea pamoja na kuwepo kwa changamoto mbalimbali kwa baadhi ya watu kutaka kuvuruga uchaguzi huo kwa watu ambao wanataka kuvuruga uchaguzi huo.
“Kama inavyojulikana kuwa hivi karibuni kuna baadhi ya viongozi na wachama wa CCM walivuliwa uongozi, kufukuzwa na baadhi yao kusimamishwa uongozi na zipo taarifa kuwa watu hao wanataka kuona uchaguzi huo haufanikiwi ila chama kimejipanga kuwabaini ili kama ni viongozi wa CCM kuchukuliwa hatua “

Magala anasema baadhi yao wameshindwa kukata rufaa kueleza jinsi wasivyo kubaliana na adhabu walizopewa na badala yake wao wanazunguka kwa wanachama kutaka kuvuruga uchaguzi wa Chama jambo ambalo halikubaliki hata kidogo katika mkoa wa Iringa.

Katibu huyo anasema kuwa hali ya uchukuaji wa fomu ndani ya chama linaonyesha kuyumba zaidi katika Wilaya ya Iringa mjini baada ya baadhi ya maeneo kuwa na mgombea mmoja pekee jambo ambalo si kawaida kutokea kwani miaka mingine wana CCM huwa wanajitokeza kwa wingi katika nafasi moja ila kwa sasa si hivyo ila wanaendelea kuhamasisha wana CCM zaidi kujitokeza kugombea nafasi mbali mbali na chama kinapenda kuona upana wa Demokrasia zaidi kwa nafasi moja inagombewa na wanachama zaidi ya watano .

“Tunahisi kuna hujuma inafanywa na hao watu waliotumbuliwa kutaka kuvuruga uchaguzi wetu kwani haiwezekani kasi ya wanachama kugombea nafasi kuwa hivi kama ilivyo “
Akizungumzia utendaji kazi wa Rais Magufuli alisema kuwa anafanya kazi nzuri na anatekeleza vema majukumu yake kwa kufanya wananchi wanyonge kuona wanadhaminiwa hivyo hapaswi kuyumbishwa na hao wanaotumbuliwa na badala yake kusonga mbele zaidi kuwatumikia watanzania .

Magala anawataka mawaziri na wote waliopewa dhamana ya uongozi kuacha kufanya kazi kwa mazoea na wale waliotumbuliwa akiwemo Waziri Prof Muhongo kutulia na kufanya kazi ndani ya chama na kuwatumikia wananchi kwa nafasi yake ya ubunge .

“Hawa wanautumbuliwa wanapaswa kutulia na kuchapa kazi wasigeuke kuwa maadui wa serikali ila wanapaswa kutambua kuwa CCM ni chama cha Kidemokrasia hivyo suala la kukosoana na kusahishana ni jambo la kawaida ndani ya chama ……..Rais wetu anatekeleza ilani ya CCM hivyo lolote analo lifanya chama kipo nyuma yake asiyumbishwe na kelele za waliotumbuliwa “

Chanzo Rai
 
Basi mwambie nae arudishe nyumba za serikali alizoonga.
abbedc5cb7e555c24dbc5f57adf5205e.jpg



Swissme
 
Back
Top Bottom