Uchaguzi 2020 Rais Magufuli amebadilika kuelekea kupata ushindi wa kishindo

Mkirindi

JF-Expert Member
Mar 2, 2011
6,750
4,958
Siasa inaonyesha Rais Magufuli, ameanza kuibali siasa, na ameanza kuwa very tolerant na yuko focused kwenya mahitaji ya kudumu ya Wananchi.

POLICAL MATURITY: Rais amezidi kuiva kisiasa, tumeona akiwa hana ushawishi katika Uchaguzi wa Ugombea Ubunge wa wale waliokuwa wakisemekana kuwa ni watu wake wa karibu.

Pia tumeona namna anavyokuwa karibu na Wazee, ambao miaka miwili iliyopita ilionekana kama hawakuwa pamoja, tumeona uhusiano wake na wale viongozi mashuhuri na wenye sifa nzuri, ukirudi kwa nguvu sana. Katika Serikali yake ya miaka 5 ijayo tutaona mabadiliko mengi sana ya kisiasa, Rais ataonekana akianza safari za nje muhimu, na sio bora kusafiri.

ECONOMIC MATURITY: Inaonekana Rais ameanza kuukubali ushauri wa wataalamu wa Uchumi, na tutaona biashara zikipewa kipaumbele mkubwa sana, huenda tukaona kodi zikapunguzwa, ili mzunguko wa biasahara na wafanyi biashara ukawa mkubwa zaidi, na pato la ushuru kuongezeka.

Rais amepewa mfano wa nchi za Falme za Kiarabu (UAE-DUBAI), Custom duty ni 4%, VAT ni 5%, Pato la nchi hizi limekuwa 80% Biashara na 20% petroli. Tanzania ya Miaka 5 ijayo, pato letu la ukusunyaji wa ushuru unaweza panda kwa 20 -30 % ya pato la leo, iwapo ushuru utapinguzwa.

Tukiangalia mabadiliko ya kisiasa tokea Rais ahamie Dodoma, kumekuwa na mabadiliko yanayojitokeza na yenye ishara nzuri sana. huu ni wakati wa wenye busara, Subira, Uvumilifu, Uzoefu na Utekelezaji wa ukweli na sio wa kutafuta sifa.
 
Mkirindi,

Katanga bhana, inaonekena unapiga ramli tu, lini kabadirika? Au baada ya spana za lissu ?? magufuri hawezi kabadirika Kama unavyoota, hata kama ameanza kubadirika kuanzia Jana mwambieni ameshachelewa, yaani kifupi October watanzania wanaimwaga pombe rasmi, mwambieni amechelewaaaa
 
Mkirindi,

Ana wakati mgumu sana kupangua hoja za upinzani. Na hivi amezoea kufoka foka na kulaumu watendaji wake, sijui atajitetea nini kwenye kampeni

Haiwezekani wewe ni mtu wa kiki tu kila siku
 
Katanga bhana, inaonekena unapiga ramli tu .. lini kabadirika? Au baada ya spana za lissu ?? magufuri hawezi kabadirika Kama unavyoota ..hata Kama ameanza kubadirika kuanzia Jana mwambieni ameshachelewa ..yaani kifupi October watanzania wanaimwaga pombe rasmi ..mwambieni amechelewaaaaaaaaaaaa
Watz hii pombe mtainyimwa hadi mvimbiwe, haimwagiki mwaka 2020 wala 2025.
 
Afute na ile kauli ya kibaguzi kwamba amesitisha maendeleo yale maeneo yaliyo kuwa yameendela.
 
Na bado, mwambie safari hii aruke hadi kichura chura na acheze mdako jukwaani, spana atachezea za kutosha tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom