Rais Magufuli ameahidi kuendeleza mageuzi. Demokrasia Tanzania ipo, kama kuna wanaoona zipo changamoto wazilete

Mgambilwa ni mntu

JF-Expert Member
May 30, 2017
2,869
3,188
Msemaji wa Serikali, Dk. Hassan Abbas yuko live TBC.
Tuungane kufuatilia yanayojiri.

Dk. Abbas anaelezea katika kipindi cha "Tunatekeleza" cha utendaji kazi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kipindi cha miaka yake mitatu ya uongozi.

Abbas ameongelea mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Tano katika kipindi cha miaka mitatu, kuwa ni:
  • Ongezeko la mapato: makusanyo ya kila mwezi kutoka bilioni 850 hadi trilioni 1.3.
  • Mashirika yaliyokuwa hoi kimapato, sasa yako hai: Mfano. TPA kutoka bilioni 743 hadi 830; TRC kutoka bilioni 23 hadi bilioni 36; DAWASCO (DAWASA) kutoka bilioni 32 hadi bilioni 120.
  • Ndoto ya Viwanda sasa ni ya kweli.
  • Mahakama ya Mafisadi: Tanzania sasa ni ya pili nyuma ya Rwanda katika Afrika Mashariki kwa kudhibiti rushwa.
  • Mapinduzi makubwa katika miundombinu: SGR, Dreamliner; Flyovers; meli etc.
Dk. Abbas amewakumbusha waandishi wa habari kutobeza mafanikio haya na kueleza kuwa, ni mambo makubwa sana ambayo yanaweza kufanywa na Serikali iliyo serious tu.

Aidha, Abbas amefafanua namna Miradi inavyowagusa wananchi moja kwa moja.
  • Kupunguza kero za umeme: Miradi ya Kinyerezi; Madaba.
  • Miradi ya Afya: Upatikanaji wa dawa kutoka asilimia 36% hadi sasa asilimia 93%. Vilevile, ujenzi wa Hospitali na vituo vya afya, ikiwa ni pamoja na madawa.
  • Sekta ya maji: Upatikanaji wa maji umefikia asilimia 41% huko vijijini.
  • Sekta ya Elimu: Elimu Msingi bila malipo inatumia bilioni 23 kila mwezi; mikopo ya wanafunzi vyuoni imeongezeka na kwa sasa hakuna migomo kutokana na kutokuwepo ucheleweshwaji.
  • Sekta ya Madini: Mapato yameongezeka bilioni 71 kwa mwezi hadi bilioni 1.2 kwa mwaka.
  • Uanzishwaji wa mifumo ya kisasa ya ukusanyaji mapato.
  • Kudumisha amani, licha ya uwepo wa changamoto ndogondogo za machafuko ya Kibiti.
  • Kujenga na kuenzi misingi ya kuanzishwa kwa Taifa la Tanzania. Misingi hiyo ni uhuru, kujitegemea na maendeleo.
Wengi hawaelewi falsafa ya a Rais Magufuli kuwa, Tanzania itakuwa a donor country. Alisema hiyo inamaanisha watu watakuja Tanzania kupata huduma zinazotolewa hapa Tanzania.

Baada ya mafanikio ya Serikali kuleta ndege nne mpya zinazoendelea kuleta mageuzi katika usafiri wa anga nchini, abiria wanaotumia ndege za ATCL wameongezeka kutoka takribani abiria 4,000 kwa mwezi hadi abiria 30,000 kwa mwezi.

Katika miaka hii mitatu serikali ya awamu ya tano imesimamia misingi ya uchumi wetu ,uchumi unaendelea kukua, unakuwa vizuri, kwa mwaka wa fedha 2017/2018 ambao umeishia mwezi June uchumi wetu umekuwa kwa kiwango cha asilimia 7.1

Kwa ukuaji wetu huo wa asilimia 7.1 Tanzania ni miongoni mwa nchi tisa duniani ambazo uchumi wake unakuwa vizuri

Akijibu maswali ya Waandishi wa habari, Msemaji wa Serikali amekiri kuwa mojawapo ya changamoto za Utawala wa Awamu ya Tano ni kutoeleweka mapema kwa wananchi kwa dhana ya mageuzi. Amesema kuwa, changamoto hiyo imepungua baada ya wananchi kuanza kuyaelewa mabadiliko hayo kutokana na kujionea maendeleo yanayoletwa na Serikali.

Kuhusu malalamiko ya vyuma kukaza, Dk. Abbas alikanusha huu ya uhalali wa hoja hiyo na kueleza kuwa, katika dhana ya mabadiliko lazima wawepo watu walioguswa kwa namna moja katika maslahi yao lakini maslahi ya wengi yamelindwa na mabadiliko.

Demokrasia Tanzania ipo. Kama kuna wanaona zipo changamoto wazilete. Tanzania ni miongoni mwa nchi chache duniani zinazokubali kushtakiwa. Hii inathibitisha kuwa Demokrasia ipo nchini


 
Tanzania ni ya 9 kati ya nchi 10 ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi Duniani.Ya 4 kwa sub sahara na ya 1 Afrika mashariki kwa ukuaji wa uchumi.
Msemaji wa serikali
MyTake:Hizi takwimu ambazo sources zimehodhiwa na serikali kuna ukweli hapo?
 
Tanzania ni ya 9 kati ya nchi 10 ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi Duniani.Ya 4 kwa sub sahara na ya 1 Afrika mashariki kwa ukuaji wa uchumi.
Msemaji wa serikali
MyTake:Hizi takwimu ambazo sources zimehodhiwa na serikali kuna ukweli hapo?
Kuhodhiwa ndio nini mzee, kwa nini asingesema kuwa Tanzania ni ya kwanza badala ya kusema ya tisa?
 
Tanzania ni ya 9 kati ya nchi 10 ambazo uchumi wake unakuwa kwa kasi Duniani.Ya 4 kwa sub sahara na ya 1 Afrika mashariki kwa ukuaji wa uchumi.
Msemaji wa serikali
MyTake:Hizi takwimu ambazo sources zimehodhiwa na serikali kuna ukweli hapo?
Toa za kwako kupinga za serikali
 
Kama mmefungiwa mirija, basi ujue hiyo mirija kwa mwingine imefunguliwa.
Mtasubiri sana but still Rais amesema wazi kuwa, mageuzi yake yako palepale. Kama ulidhani moto unazimwa ni bora utoroke tu.
 
Msemaji wa Serikali, Dk. Hassan Abbas yuko live TBC.
Tuungane kufuatilia yanayojiri.

Dk. Abbas anaelezea katika kipindi cha "Tunatekeleza" cha utendaji kazi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli katika kipindi cha miaka yake mitatu ya uongozi.
Mnaweza kufuatilia hapa:
 
Kichaa kwako na nyumbani kwenu. Kama mmefungiwa mirija, basi ujue hiyo mirija kwa mwingine imefunguliwa.
Mtasubiri sana but still Rais amesema wazi kuwa, mageuzi yake yako palepale. Kama ulidhani moto unazimwa ni bora utoroke tu.
Sasa kinachomfanya anaenda kulilia makanisani kuwa hii kazi ni ngumu nini? jiwe ni jiwe tuu
 
Nani analipa ghalama za kulusha matangazo ya TV Live,maana tuliona tufute matangazo ya bunge ili tuokoe fedha
 
Back
Top Bottom