comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dr John Pombe Magufuli amesema amani ya nchi nyingi duniani imetoweka hasa baada ya nchi hizo kuchanganishwa na makundi mbalimbali, Rais ameyasema hayo leo jumatano wakati wa akitoa hotuba hiyo katika hafla ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa reli ya kisasa yaani Standard Gauge maeneo ya Pugu nje kidogo ya jiji la Daresalaam, Mh Rais amesema utulivu na amani ni kitu bora sana katika kujenga nchi kwani ili ujenge nchi unahitaji amani kwanza, aidha Mh Rais ameasa kwamba amani iliyopo iendelee kuwepo na alitoa mifano mingi sana kwamba kuna vyombo mbalimbali vinaweza hata kuleta uchonganishi na kuvuruga amani "angalia baadhi ya nchi mamilioni ya watu wameuana wenyewe kwa wenyewe aidha kwa kuchonganishana au kuchonganishwa na baadhi ya watu,halafu wanaewachonganisha mkianza kugombana tu wao hukaa pembeni na kuwaangalia tu,"
Hivyo basi watanzania wenzangu mtumie nafasi hii kudumisha amani kwani amani ndio inaleta maendeleo katika ujenzi wa nchi na vurugu zinaleta uharibifu wa mali na maisha ya watu alisema Mh Rais
Hivyo basi watanzania wenzangu mtumie nafasi hii kudumisha amani kwani amani ndio inaleta maendeleo katika ujenzi wa nchi na vurugu zinaleta uharibifu wa mali na maisha ya watu alisema Mh Rais