Rais Magufuli alivyofanikisha kampeni ya Kiswahili kuwa lugha ya SADC

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
1566460649239.png


“MCHEZA Kwao hutuzwa” ni msemo wa Wahenga wenye ujumbe mzito unaoweza kutumika kuelezea hatua ya mafanikio ya kampeni iliyoanzishwa na Rais John Magufuli ya kupigia debe matumizi ya Lugha ya Kiswahili.

Rais Magufuli ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), amezichanga vyema karata zake katika dhima ya kuhakikisha kwamba Kiswahili kinapata fursa ya kuwa lugha rasmi ya nne kwenye shughuli za jumuiya hiyo.

Agosti 18 mwaka huu akitoa hotuba ya kufunga mkutano wa Wakuu wa SADC, Rais Magufuli alisema kupitishwa rasmi kwa Kiswahili kuwa lugha ya nne katika Jumuiya hiyo ni faraja kwa sababu ndiyo lugha iliyotumika kwenye mafunzo ya harakati za ukombozi.

“Ni heshima kubwa kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambaye aliongoza harakati za ukombozi zilizofanywa na wapigania uhuru barani Afrika,” anasema na kuongeza: “Kutokana na upendo wake kwa watu wa mataifa mengine ya Afrika, alikubali taifa na wananchi wake wateseke ili kufanikisha ukombozi huo.” Akitumia Lugha adhimu ya Kiswahili katika hotuba hiyo, Rais Magufuli anabainisha juhudi kubwa zilizofanywa na Tanzania kuhakikisha amani na utulivu vinapatikana katika ukanda wa SADC na Bara la Afrika kwa ujumla. Anatoa mfano wa namna Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lilikwenda nchini

kiasi kikubwa kukuza ushirikiano na utengamano wa wananchi. “Kiswahili ni Lugha ya Afrika na sisi ni wananchi wa Bara hili, hivyo tunapaswa kuitumia…ni vyema kama viongozi wa nchi za SADC wataiga mfano wa Afrika ya Kusini ambayo itaanza kufundisha Kiswahili katika shule zake kuanzia mwakani,” anasema.

Anabainisha kuwa Tanzania ipo tayari kusaidia kufanikisha malengo ya kufundisha na kutumia Kiswahili katika shughuli mbalimbali kwenye ukanda wa SADC. Awali akifungua mkutano huo, Rais Magufuli alitumia Lugha ya Kiingereza kuwashawishi viongozi wenzake wamruhusu kutoa hotuba yake ya ufunguzi kwa Lugha ya Kiswahili. “Nina imani kwa kufanya hivyo mtashawishika kukubali na kupitisha Kiswahili kuwa lugha rasmi ya SADC, lugha ambayo ilitumika wakati wa harakati za ukombozi,” anasema.

Anabainisha kwamba Kiswahili ni lugha kubwa ambayo tayari inazungumzwa kwenye nchi 34 za Afrika, kati ya hizo sita ziko katika SADC.

HARAKATI ZA KUKIPIGANIA KISWAHILI
Harakati za Rais Magufuli kuipigania lugha hiyo itumike ipasavyo Afrika na katika uga wa kimataifa hazikuanzia kwenye mkutano huo. Amekuwa akisisitiza matumizi ya lugha hiyo kwenye warsha na mikutano mbalimbali nchini na nje ya nchi. Ni vyema kwamba hatimaye azma yake imefanikiwa hasa baada ya kuitumia vyema ardhi yake ya nyumbani na nafasi yake ya uenyekiti wa SADC kuchombeza vionjo, faida na umuhimu wa matumizi ya lugha hiyo.

SEIF KHATIBU
Mohamed Seif Khatib ni mwanasiasa anayetajwa kuwa mwalimu na mpenzi wa lugha ya Kiswahili, anazungumzia hatua hii akimpongeza Rais Magufuli kwa kujitokeza hadharani na kuendesha kampeni ili Kiswahili iwe lugha rasmi SADC. Khatibu ambaye pia ni mwanasiasa mkongwe aliyewahi kushika uongozi ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na uwaziri anabainisha kuwa juhudi zinazofanywa na Rais Magufuli zitakuwa na manufaa iwapo uteketelezaji wake utafanywa kwa mikakati madhubuti.

CHAKUBALIWA AFRIKA
Khatib anabainisha kuwa miaka sita iliyopita Umoja wa Afrika (AU) ulipitisha rasmi kwamba Kiswahili kianze kutumika kama mojawapo ya lugha rasmi Afrika. yamechapishwa kwenye magazeti na majarida tofauti. Miongoni mwa vitabu vyake ni pamoja na ’Pambazuko la Afrika, Utenzi wa Ukombozi wa Zanzibar na ‘Fungate’ ya Uhuru.

Anabainisha kuwa hata Ilani ya CCM Ibara ya 95 inabainishwa kuwa Kiswahili kitakuwa bidhaa. “Kwa hiyo kupitishwa kuwa lugha rasmi ni fursa kubwa kwa Watanzania hasa vijana waliosoma masuala ya lugha na ualimu ambapo watapata ajira za kwenda kufundisha au kutafsiri,” anasema na kuongeza: “Hatua hii imefikiwa kutokana na juhudi binafsi alizozifanya Rais Magufuli, kwani wamepita marais kadhaa nchini tangu uhuru upatikane lakini huyu ndiye wa kwanza aliyejitokeza wazi kupigia kampeni matumizi ya lugha hii,” anasema Khatibu.

ANGALIZO

Khatib anatoa angalizo kwamba iwapo utekelezaji wake hautasimamiwa vizuri basi inaweza kuwa kama maagizo yaliyotolewa kule AU, kuhusiana na matumizi ya lugha hiyo ambapo utekelezaji wake si madhubuti. “Hivyo ni vyema kwa nafasi yake ya uenyekiti Tanzania ijipange vyema kuhakiksha jambo hili linatekelezwa na kuwa na mafanikio yaliyokusudiwa,” anasema na kuongeza: “Tumepata bidhaa nzuri ya kuuza… Kiswahili ni bidhaa…Rais Magufuli amekuwa mfano wa kuhakikisha anafanikisha matumizi ya lugha ya Kiswahili.”

WENGINE

Baadhi ya viongozi wamejitokeza pia kuunga mkono kampeni hizo za Rais Magufuli na miongoni mwao ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki nchini Profesa Palamagamba Kabudi. Prof. Kabudi amehakikisha anasimamia na kuwezesha mapendekezo ya kuifanya lugha hii kuwa rasmi ya SADC yanafka kwenye mkutano wa wakuu wa nchi wanachama uliomalizika karibuni. Akiwa ni Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri la SADC, Profesa Kabudi aliwajulisha waandishi wa habari kuwa Baraza hilo liliwasilisha mapendekezo yake kwenye Mkutano wa 39 wa Wakuu wa nchi na Serikali wanachama wa SADC likiwamo la kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya nne katika nchi 16 wanachama.
 
Huyu anapigania kiswahili kwa masilahi yake binafsi kwakuwa hawezi kuongea kingereza vizuri anataka kuficha udhaifu huo kwenye kichaka cha kiswahili
 
Huyu anapigania kiswahili kwa masilahi yake binafsi kwakuwa hawezi kuongea kingereza vizuri anataka kuficha udhaifu huo kwenye kichaka cha kiswahili

Ni maoni yako hayo. Unafikiri JPM atakuwepo muda wote?
Unajua lugha za SADC zote ni za wazungu?
 
Ni maoni yako hayo. Unafikiri JPM atakuwepo muda wote?
Unajua lugha za SADC zote ni za wazungu?
Unajua tangu kipindi cha JK tunaambiwa kiswahili ni Lugha mojawapo itakayotumika kwny mikutano ya AU?

Vipi hua unasikia AU wakitumia kiswahili?
 
Mwl Nyerere alipata kusema kiingereza ni kiswahili cha Dunia.
 
Back
Top Bottom