kabingo
Senior Member
- Oct 16, 2015
- 115
- 118
Hivi Mh. Rais mimi ndio sielewi au ni vipi, unaposema huduma hospitalini zitolewe bure unamaanisha nini au ni maneno ya jukwaani. Maana wewe sio mwanasiasa hivyo sipendi kusema ni maneno ya siasa .
Mwanangu ametoka shule anatapika nikaona nimuwahishe zahanati ya serikali nikiamini huduma nitapata bure maana mwezi wa kwanza wenyewe unaniacha hoi. Kwanza nikaambiwa kadi 1000, kupima malaria 1000, mkojo,1000, tyfoid (sina uhakika na spelling) 3000, nikaambiwa ukimwi atapimwa bure.
Baada ya vipimo vyote nikaambiwa hana tatizo lolote, siwafichi nilitamani kuomba wanirudishie 6000 zangu. Sasa kama Raisi unapita humu tunaomba utuambie huduma bure unazosema zinatolewa hospitali gani ndani ya nchi hii!?