mnengene
JF-Expert Member
- Nov 21, 2011
- 4,112
- 6,302
ninachotaka ni Serikali kuwa serious na huu ugonjwa ,
Kwanza waje wakiri wamesakosea na waombe radhi,kwa uzembe wa kuchelewa kufunga mipaka ya nchi
na jamaa aliyechimbo chatoga ajitokeze aje aongoze mapambano hii ni vita amiri jeshi kukimbia vita ni hatari kwa nchi
kawaachia nchi akina bashite na dada ya korona kwenye hii ishu ni shida.
Wengine wanatoa matamko ya kipuudhi tu mara wengine wanachapa wananchi fimbo, mwingine anakurupuka anafunga bar kesho anakurupuka tena anazifungua, mwingine anakurupuka bar ziuze kama take away tu hakuna kunywa,
Mwingine anakurupuka eti bar ziuze kama kawaida ila wamiliki wazingatie umbali wa wateja yaani akili fupi kabisa mmiliki gani wa bar asiyetaka wateja wengi auze bia nyingi .
Bashite anatoa maagizo wananichi wote kuanzia tarehe 20 wavae barakoda, Mikoa mingine Je? nani awape order hiyo.
Basite analazimisha hata barakoda za vitambaa, naibu waziri Dr Ndugulile anaibuka na kusema barakoda za vitambaa hazifai na sio madhubuti kuzuia virusi vya ugonjwa huu
Mwingine anakurupuka kuwatangazia watu wake wawatenge watu wote wanaotoka dar es salaam.
Kimsingi ninataka msimamo dhabiti na mmoja wa Serikali kuhusu namna ya kudhibiti huu ugonjwa ,Sio kila kionozi anakurupuka na lake
Hii tume ya huu ugonjwa iliyopo chini ya Waziri Mkuu ivunjwe imeshindwa kazi.
Iundwe nyingine isimamiwe na Rais mwenyewe,
Serikali ifanye mpango wa kuwanunulia wananchi maskini barakoda bure,
Pia wale wote waisiokuwa na kazi maalumu mijini na ni maskini wajulikane wapatiwe chakula bure na serikali na waambiwe watulie majumbani kwao.
Omba omba wote wakusanywe wawekwe sehemu maalumu wapatiwe huduma zote na serikali hadi ugonjwa utakapokwisa.
Ma bar makumbi ya starehe clubs yafungwe kwa muda, sheree kama harusi kitchen part na magettogether yapiwe marufuku.
Maofisini ukiachilia essential services watumishi waende kwa shift kama idara inawatumishi 10 wiki moja waende watano wiki inayofata waende watano ili kupunguza msongamano maofisini, mfano halmashaurini huko idara za Elimu unakuta kuna watumishi kibao wakati shule zimefungwa hao ikiwezekana wapewe tu likizo.
Kwenye vituo vya daladala wapiga debe wote wakusanywe wapewe chakula au fedha waambiwe waisionekane stendi.
Mabasi yote ya abiria yawe yanafanyiwa fumigation kila asubui kabla ya kuanza kwa kazi na milangoni kuwe na dawa za kunawa za chloride muda wote.
Wananchi wote wanapotoka kwenye public wavae barakoda na waimizwe kunawa mikono mara kwa mara.
Serikali iweke sehemu maalumu za kunawia mikono kwenye maeneo yote ya umma.
hospitali ziboreswe wodi za ICU na zenye ventilators ziongezwe ili ikitokea watu wakizidiwa wapate matibabu,
Maeneo ya kutenga watu wanaoisiwa kwa ajili ya quarantine yaongezwe
Hatua za kuchukua kupiga vita ugonjwa huu ni nyini sana nashangaa serikali imeamua kutumia njia ya kukutuma wewe uje huku mtandaoni kuleta blahblah na pumba za kijinga . Pumbavu sana we jamaa.
Fikisha ujumbe kwa namba moja na namba 2 wajitokeze huko walipo waje waongoze haya mapambano wananci waliwapiia kura wao na sio akina bashite na dada ya korona