Rais Magufuli alimaanisha nini aliposema 'Polisi mnatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya fedha...'?

kindafu

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
1,346
1,678
Kwenye shughuli ya Polisi leo, kati ya mambo mengi aliyoyazungumzia Rais ni pamoja na suala la polisi kutuhumiwa kwa matumizi mabaya ya fedha: "Mheshimiwa IGP, ................., lakini na nyie mnatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya fedha, ha ha ha, ila yaliyopita si ndwele, tugange yajayo"!!

Ina maana hamna kufukua makaburi? Ndio Lugumi keshachomoka Au?
 
Kumbe ? Wewe ulidhani kungetokea nini? Chezea Chichiem wewe? Wacha bwana; hata kama angekuja malaika ni lazima aingie kwenye line tu
 
Kama Magu angekuwa Alipita Jeshini angetambua kuwa hakupaswa kuwaita IGP na Makamanda wa Mikoa "Waheshimiwa". Mara kadhaa alikuwa akirudia Mheshimiwa IGP, Waheshimiwa Makamanda...

,

mheshimiwa rais akubali aandikiwe hotuba otherwise atakua anakosea na kutoa kauli tata kila mara... akubali tuu kwa kipindi hiki mpaka atakapozoea
 
Kwenye shughuli ya Polisi leo, kati ya mambo mengi aliyoyazungumzia Rais ni pamoja na suala la polisi kutuhumiwa kwa matumizi mabaya ya fedha: "Mheshimiwa IGP, ................., lakini na nyie mnatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya fedha, ha ha ha, ila yaliyopita si ndwele, tugange yajayo"!!

Ina maana hamna kufukua makaburi? Ndio Lugumi keshachomoka Au?

Kumbe JPM alishaashiria kwamba skandali ya Lugumi si ndwele, ndo maana bungeni ikakatwa mtama juu kwa juu! HapaKaziTu, hutaki acha!!
 
Back
Top Bottom