Rais Magufuli alikataa dili la Kikwete na Mchina ya $7.6 Bilioni kujenga SGR yote na leo hii Dar - Makutopora tumetumia zaidi ya $ 2 Bilioni. Ikoje?

Huo ndo ukweli, rushwa katika nchi zinazoendelea ni suala mtambuka. Japo ni Muhimu pia kama kiongozi wa nchi kutumia maarifa mengi katika kung'amua upuuzi huo, kwani mwisho wa siku wananchi tutakuangalia wewe /Rais.

Kwa mfano, angalia serikali ya Uganda ilivyo pata tabu kujua ipi reli ya manufaa kwa nchi yake yaan Tanzania, Electric SGR from Diesel SGR Kenya. Pale paliibuka makundi kila mtu na Maelezo yake kumbe kila mtu anampigia chapuo Mteja wake ili 10% iingie na sio nchi kwa Ujumla itanufaikaje na Mradi husika. Hapo ndo utajua waafrika wengi ni viande na wachumia tumbo, uzalendo kushoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ufukara wa Africa uletwa na mfumo wa uongozi mbaya uliooza yaani MTU mmoja ndio uwaamulia wengi hapa vipaumbele vya watawala huwa sio vipaumbele vya watawaliwa watawala hawajali kuhusu riba bali sifa,uvivu,ubinafsi, ufisadi upigaji na wizi hapa kila MTU mpigaji kuanzia juu hadi Dada wa kazi mtawala uwapiga walipa kodi baba anapiga ofisini analeta nyumbani, mama anapiga anapeleka kwao au kwa mcheps,Dada wa kazi anapiga chenjichenji anapeleka kwao. Halafu utasikia watawala wanawalaumu eti mabeberu awataki tuendelee wamewakaririsha wasomi wetu eti wakawaongopee wanafunzi eti ukoloni mambo Leo ndo kikwazo ili waendelee kupiga.Internal factors ndizo keys za ufukara wetu tuache kuwasingizia wenzetu kwa kushindwa kwetu.Utawala mbovu,rushwa ufisadi na upigaji,ubinafsi, choyo,uvivu,uchawi hivi tumejitengenezea wenyewe tusiwangizie mabeberu, sijui ukoloni mambo Leo mara ohoo mashirika ya kimataifa
 
Mkuu, mtu hashikiwi mdomo na kuelekezwa cha kusema, kutokusema kwake yawezekana yawezekana kuna kulikuwa na mantiki sana kulinganisha na angesema ,
Ndio tatizo. Usiri wa nini? Asiposema sie tutasema with our own conclusions. Kwa hapa tutahisi lilikuwa gubu tu kwa Kikwete. Kwa nini asiwaite Wachina tutakaa tena mezani kama aliona kuna mapungufu? NI wazi alitaka kumkomoa KIkwete. KUmbuka Wachina walikuwa wameshaanza kujenga. Tena walitustahi sana kutokana na uhusiano wetu, lasivyo hata ile Dreamliner isingerudi baada ya kwenda China
 
Huyo jamaa inawezekana kabisa aliamua kuanza mradi upya ili yeye na watu wake wapate nafasi ya kutupiga, na kwahizo gharama zilivyoongezeka, kwanini niamini vinginevyo!.

Hii nchi inageuzwa shamba la bibi na kila serikali inayoingia madarakani.

Kweli CCM ni laana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Inawezekana hela alizotupiga ndo kanunulia kiwanja cha Square meter 728 cha MAKAZI ununuo.
 
Unapolinganisha kuna vitu muhimu ni vizuri ukavichambua pia.
1. Thamani ya Pesa ya Wakati ule na sasa ipo sawa? Usilinganishe tu figure bila kuzama ndani
2. Umekokotoa urefu na miundombinu ambayo inajengwa katika mradi wa sasa kama ni sawa na mkataba wa awali?
3. Mikataba hua inaambatana na Masharti mbalimbali hivyo ungechambua vizuri ili uwe haki ya kutoa lawama zako
Msitetee vitu visivyo na maana. Kwenye mkataba wa kujenga reli toka Dar mpaka Mwanza hakukuwa na masharti yoyote zaidi ya kwamba Serikali ya China ndiyo ingedhamini huko Exim Bank China, na kamouni ya ujenzi ingetoka China.

Hakukuwa na masharti yoyote mengine zaidi. Shida kubwa ya Rais wetu yupo negative naturally, na mtu anayependa kusikiliza majungu.

Hata Rais alipowakataa Wachina hakutoa sababu nyingine yoyote zaidi ya kusema bei iliyokubaliwa ilikuwa kubwa mno, na yeye serikali yake ilikuwa imewapata wajenzi ambao wangeijenga kwa karibia nusu ya bei iliyokubaliwa awali kati ya serikali ya JK na Serikali ya China.
 
Unataka watu wafanyeje wasipojadili yanayotokea katika nchi yao?Akili zenu huwa mnaziazima wapi?
Elimu,Elimu,Elimu!
Elimu Elimu Elimu!
Umenikumbusha enzi za mgombea wetu URAIS.
Sijui alituona makamanda wengi hatuna ELIMU?
2015 hatutaisahau.
 
Ila hata hivyo bandiko/andiko /waraka wa Kabendera hauwezi kuwa uthibitisho tosha kwetu kuweza kujadili suala zima la mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na China kuhusu ujenzi wa reli ya kisasa /SGR.

Hebu tujaribu hata kuangalia kwa majirani zetu hapo kaskazini walivyolizwa na hao hao Chinese, mpaka sasa Majirani zetu wanautamani Mradi wetu japo haujakamilika ile Kuna kitu amazing wanakinusa hayo mbeleni.

Sawa Kuna mapungufu mengi katika awamu hii kama hizo nyingine zilizopita ila isiwe kila Mradi tunataka ufanyike nchi nyingine ndo tuusifu pia tuseme ona kwa akina fulani afu hicho hicho kikifanyika nyumbani kutwa kupigiana kelele.

Watu bwana, ili kutetea jambo basi mtasema lolote. Kwa hiyo huamini alichoandika Kabendera? Hivi unafikiri Kabendera anaandikia haya magazeti yetu ya udaku?

Na nani alisema mkataba wetu ulikuwa sawa na wa Kenya? Kenya wanatuzidi ufisadi hilo liko wazi. Sasa kama waliuza nchi kwa China haina maana na sisi ilikuwa lazima tuuze. Na nimeshasema humu ndani, mkataba wa SGR na China ulikuwa kati yetu na serikali ya China na kampuni ya China ya kujenga SGR ilikuwa ni ya serikali ya China sio kampuni binafsi. Kulingana na uhusiano wetu na China, nini kilimzuia Magufuli kuongea na Raisi wa China na kusema tungependa ku-review mkataba kwanza kwa kuwa tunataka SGR ya umeme sio ya diesel? Entry point ya kureview mkataba ilikuwapo na angekuwa na busara angeitumia - modernization to SGR for electric trains. Lakini Magufuli akapendelea umaarufu wa kisiasa wa kumuumbua KIkwete badala ya kuwa pragmatic na akaishia kukurupuka na sasa tunalia.

Si alisema tutajenga kwa hela yetu. Kiko wapi sasa? Unajua waliomwambia haiwezekani kujenga kwa hela yetu aliwaambia nini? Wapumbavu.

Hebu acheni kutetea upumbavu huu.
 
Msitetee vitu visivyo na maana. Kwenye mkataba wa kujenga reli toka Dar mpaka Mwanza hakukuwa na masharti yoyote zaidi ya kwamba Serikali ya China ndiyo ingedhamini huko Exim Bank China, na kamouni ya ujenzi ingetoka China.

Hakukuwa na masharti yoyote mengine zaidi. Shida kubwa ya Rais wetu yupo negative naturally, na mtu anayependa kusikiliza majungu.

Hata Rais alipowakataa Wachina hakutoa sababu nyingine yoyote zaidi ya kusema bei iliyokubaliwa ilikuwa kubwa mno, na yeye serikali yake ilikuwa imewapata wajenzi ambao wangeijenga kwa karibia nusu ya bei iliyokubaliwa awali kati ya serikali ya JK na Serikali ya China.
Umenena Mkuu. Mie nimesema wazi hapo juu; Kulingana na uhusiano wetu na China, nini kilimzuia Magufuli kuongea na Raisi wa China na kusema tungependa ku-review mkataba kwanza kwa kuwa tunataka SGR ya umeme sio ya diesel? Entry point ya kureview mkataba ilikuwapo na angekuwa na busara angeitumia - modernization to SGR for electric trains. Lakini Magufuli akapendelea umaarufu wa kisiasa wa kumuumbua KIkwete badala ya kuwa pragmatic na akaishia kukurupuka na sasa tunalia.

Si alisema tutajenga kwa hela yetu. Kiko wapi sasa? Unajua waliomwambia haiwezekani kujenga kwa hela yetu aliwaambia nini? Wapumbavu.

Hebu acheni kutetea upumbavu huu.
 
Miradi ambayo Magufuli kavuruga kwa kisingizio cha uzalendo

1. Gesi Mtwara
2. Bandari ya Bagamoyo
3. SGR
4. Nyumba za Dege beach
5. Big Results Now
6. Kilimo Kwanza
7. Korosho
8. Mbaazi

Hivi vyote kavikuta vinakwenda vizuri yeye kaja na mawazo yake tofauti kabisa, Matokeo yake kila anachogusa hakiendi, matokeo yake anakopa tu kuficha udhaifu wa maamuzi yake mabaya
 
Sasa kama Watanzania tunakuwa mapoyoyo wa kukubali kila kinachopendekezwa kwenye mkataba basi hatuna akili.
Ndio mana tukapitisha sheriabya madini kwa ajilibya ile mikataba mibovu
Halafu kama dar dom ni Bilioni mbili,kuanIa hapo kwenda kigoma haitazidi Bilioni tatu kwakua ni mapori matupu hakuna fidia wala kuchoronga miamba
 
Wakati Magufuli anaingia madarakani alikuta Kikwete ametengeneza makubaliano na Wachina ya Kujenga SGR yote Dar hadi hadi Kigoma, na pia kutoka Uvinza kwenda mgodi wa Musongati wa Burundi na kufika Kaliua. Ilikua iende na Mwanza nadhani, kwa mkopo wa $7.6 Bilioni kupitia benki ya China ya EXIM na Kampuni ya Ujenzi ya Reli za serikali ya China. Magufuli aliitupia hii dili nje kwa madai kuwa ilikuwa na harufu ya ufisadi na kwamba tutajenga SGR kwa fedha zetu za ndani.

Sasa leo hii, zaidi ya fedha ambazo tayari tumezamisha kwenye SGR kipande cha Dar hadi Dodoma tu, tumekopa tena $ 1.46 Bilioni ili kukamilisha ujenzi wa SGR toka Dar hadi Makutopola. Hili linafanyika wakati TRC wanasema hadi sasa kipande kilichojengwa kimeshakula $1.3 Bilioni. Hii inamaanisha kwamba tunakopa $ 1.46 Bilioni kukamilisha sehemu ambayo tayari imekula $1.2 Bilioni. Kwa hiyo basi, hadi sasa kuanzia Dar hadi Makutopola gharama inaweza kufikia zaidi ya $3 Bilioni, ambayo ni karibu nusu (50%) ya mkataba ambao Kikwete na Wachina walikuwa watie sahihi kama gharama ya kujenga SGR yote, na Raisi Magufuli akatuaminisha Watanzania kwamba ule mkataba ulikuwa na harufu ya ufisadi.

Sasa wana JF mie nilishasema kuna mambo huwa simuelewi Magufuli. Kama kuna anaelewa juu ya hili basi naomba anifafanulie.

Usikute Kikwete na Wachina kwa sasa hivi wanacheka kweli kweli, na wanamcheka nani hilo halihitaji PhD kwa wewe kuelewa.

According to the Tanzania Railways Corporation’s latest reports on expenditure the project has so far spent an estimated $1.2 billion for two phases.The corporation’s project manager Machibya Kadogosa confirmed to The EastAfrican in an exclusive interview that, the two phases are currently being constructed by a Turkish firm Yapi Merkezi, in partnership with Portuguese firm Mota-Engil Africa.
Mimi nilisoma yale makubaliano hayakuwa na tatizo lolote tena wangejenga reli njia yote dar mpaka mwanza na kipande cha kigoma,lakini serikali ikaona haifai, leo tunajenga vipande vipende gharama lazima iwe kubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa leo hii, zaidi ya fedha ambazo tayari tumezamisha kwenye SGR kipande cha Dar hadi Dodoma tu, tumekopa tena $ 1.46 Bilioni ili kukamilisha ujenzi wa SGR toka Dar hadi Makutopola
Nadhani kibaya zaidi ni kwamba hii bilioni$1.469 ni mkopo wa kibiashara.

Mkopo huu, 'riba' itaanza kulipwa mara tu fedha itakapoingia kwenye 'account' zetu.

Sasa piga mahesabu ya pesa ya ziada inayolipwa kwa mda ambao reli itakuwa inajengwa, kabla hata haijafika huko Makutopora - miaka mingapi, mitatu, minne, mitano?

Hiyo pesa tutakayolipa wakati reli bado inajengwa iongeze kwenye hiyo bilioni $1.469. Katika miaka mitano si ajabu jumla itakuwa imefika kwenye bilioni $3 na ushee!

Yale makubaliano ya Kikwete na Mchina hayawezi yakawa tofauti sana na yale ya Kenya.

Kwa hiyo hiyo bilioni $7.6 (bila shaka ingegawanywa kwenye awamu (vipande vipande kama ilivyo sasa); na kila kipande kingejengwa kwa muda maalum ya makubaliano.

Ndani ya mda huo wa ujenzi pangekuwepo na 'grace period' kabla ya riba haijaanza kulipwa. Kwa mfano, miaka mitano waliyopewa Kenya kwa kipande toka Mombasa hadi Nairobi. Na malipo ya hiyo 'interest' yangeanza kulipwa wakati reli tayari iko kazini, ikizalisha pato, hata kama ni dogo!

Hii reli yetu itakuwa aghali sana

Na bado.tutaendelea kulipia huo mkopo miaka ishirini ijayo!

Tulikuwa tukiwacheka wakenya kwamba reli yao ni ya gharama kubwa kuliko uhalisia (kutokana na ufisadi); lakini yetu itakuwa ni gharama kubwa sana, kutokana na nini? ujinga?, kiburi?' vyote kwa pamoja?
 
Mtoa mada ngoja nikusaidie kitu naona unavimba mishipa ya kichwa kwa jambo dogo....angalia barabara za mitaani za kipindi cha Jk na barabara za mitaani za kipindi cha sasa cha Magu,mjengaji ni yule yule mchina kwa thamani ile ile ya pesa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati Magufuli anaingia madarakani alikuta Kikwete ametengeneza makubaliano na Wachina ya Kujenga SGR yote Dar hadi hadi Kigoma, na pia kutoka Uvinza kwenda mgodi wa Musongati wa Burundi na kufika Kaliua. Ilikua iende na Mwanza nadhani, kwa mkopo wa $7.6 Bilioni kupitia benki ya China ya EXIM na Kampuni ya Ujenzi ya Reli za serikali ya China. Magufuli aliitupia hii dili nje kwa madai kuwa ilikuwa na harufu ya ufisadi na kwamba tutajenga SGR kwa fedha zetu za ndani.

Sasa leo hii, zaidi ya fedha ambazo tayari tumezamisha kwenye SGR kipande cha Dar hadi Dodoma tu, tumekopa tena $ 1.46 Bilioni ili kukamilisha ujenzi wa SGR toka Dar hadi Makutopola. Hili linafanyika wakati TRC wanasema hadi sasa kipande kilichojengwa kimeshakula $1.3 Bilioni. Hii inamaanisha kwamba tunakopa $ 1.46 Bilioni kukamilisha sehemu ambayo tayari imekula $1.2 Bilioni. Kwa hiyo basi, hadi sasa kuanzia Dar hadi Makutopola gharama inaweza kufikia zaidi ya $3 Bilioni, ambayo ni karibu nusu (50%) ya mkataba ambao Kikwete na Wachina walikuwa watie sahihi kama gharama ya kujenga SGR yote, na Raisi Magufuli akatuaminisha Watanzania kwamba ule mkataba ulikuwa na harufu ya ufisadi.

Sasa wana JF mie nilishasema kuna mambo huwa simuelewi Magufuli. Kama kuna anaelewa juu ya hili basi naomba anifafanulie.

Usikute Kikwete na Wachina kwa sasa hivi wanacheka kweli kweli, na wanamcheka nani hilo halihitaji PhD kwa wewe kuelewa.

According to the Tanzania Railways Corporation’s latest reports on expenditure the project has so far spent an estimated $1.2 billion for two phases.The corporation’s project manager Machibya Kadogosa confirmed to The EastAfrican in an exclusive interview that, the two phases are currently being constructed by a Turkish firm Yapi Merkezi, in partnership with Portuguese firm Mota-Engil Africa.

Umekimbilia conclusion kama mtoto

1.mpaka sasa hela ya kikwete haijafikiwa
2.tatizo sio value ni interest na conditions

Mikataba ya wachina dunia nzima ni mibaya

Umeangalia issues hizo?

Maana kwa shallow argument kama hizi, hautakuja kumuelewa JPM
 
Ndio tatizo. Usiri wa nini? Asiposema sie tutasema with our own conclusions. Kwa hapa tutahisi lilikuwa gubu tu kwa Kikwete. Kwa nini asiwaite Wachina tutakaa tena mezani kama aliona kuna mapungufu? NI wazi alitaka kumkomoa KIkwete. KUmbuka Wachina walikuwa wameshaanza kujenga. Tena walitustahi sana kutokana na uhusiano wetu, lasivyo hata ile Dreamliner isingerudi baada ya kwenda China

Sasa hata angesema sisi wanyonge tungefanyeje ?

Kama issue ni kusema ni mangapi alisema na akafanya maamuzi hapo hapo bila kurejea tena mezani ?

Rejea hilo sakata la Bagamoyo Port alisema, na hatukurudi mezani kama utakavyo .
 
Elimu Elimu Elimu!
Umenikumbusha enzi za mgombea wetu URAIS.
Sijui alituona makamanda wengi hatuna ELIMU?
2015 hatutaisahau.
Ujinga bado janga la taifa,hata waliopata elimu wapo wapo tu kama wewe hawajui wajibu wao hasa pale wanapokuwa wanakula keki ya taifa!
 
Back
Top Bottom