Rais Magufuli alikataa dili la Kikwete na Mchina ya $7.6 Bilioni kujenga SGR yote na leo hii Dar - Makutopora tumetumia zaidi ya $ 2 Bilioni. Ikoje?

Sitaki kupingana na mtoa maada, japo Kuna video inamuonesha JK Mrisho akihojiwa kuhusiana na Mwenendo mzima wa uongozi wa raisi JPM, Pia akatolea ufafanuzi zaidi juu ya Mradi wa SGR.

Katika maelezo yake yeye alisema "katika uongozi wangu tulipanga tujenge reli ya kisasa ya diesel yaan SGR kama ile ya Kenya, ila namsifu Magufuli kwa kulifanyia utekelezaji wazo letu (Fourth Government) tena kwa kuifanya iwe ya ukisasa zaidi na yenye ufanisi mkubwa kuliko tuliyokua tumepanga siye".

Kwa maelezo hayo unaona jinsi gani JPM kaja na Mradi ule ule ila kivingine. Kwa vyovyote vile kwa kubadili Design ya Mradi ni dhahiri shairi hata viwango vya fedha za uwekezaji zitabadilika tu.

Inawezekana, lakini pia usisahau JK Mrisho hawezi kukosoa hadharani, lazimaaongelee hilo suala positively
 
Ingawa Kuna sintofahamu nyingi za mikataba yetu mbali inayohusu maendeleo ya nchi yetu kwa pamoja.

Ila hata hivyo bandiko/andiko /waraka wa Kabendera hauwezi kuwa uthibitisho tosha kwetu kuweza kujadili suala zima la mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na China kuhusu ujenzi wa reli ya kisasa /SGR.

Hebu tujaribu hata kuangalia kwa majirani zetu hapo kaskazini walivyolizwa na hao hao Chinese, mpaka sasa Majirani zetu wanautamani Mradi wetu japo haujakamilika ile Kuna kitu amazing wanakinusa hayo mbeleni.

Sawa Kuna mapungufu mengi katika awamu hii kama hizo nyingine zilizopita ila isiwe kila Mradi tunataka ufanyike nchi nyingine ndo tuusifu pia tuseme ona kwa akina fulani afu hicho hicho kikifanyika nyumbani kutwa kupigiana kelele.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe na magufuli nani alikua kwenye nafasi nzuri ya kunusa ufisadi?
Wachina watakupa mkopo wa B7,watalazimisha kampuni yao ifanye kazi,mradi ukifika kati mnaambiwa gharama zimeongezeka kwa hamtakua na jinsi mnakopa tena,waulizeni kenya walikopa kwa treni inayotumia mafuta ya taa sasa hivi deni limezidi kwa 100%
Kwa hiyo tatizo lilikuwa mkataba sio ufisadi? Hivyo unavyosema huwa vipo kwenye mkataba. Sasa kama Watanzania tunakuwa mapoyoyo wa kukubali kila kinachopendekezwa kwenye mkataba basi hatuna akili.

Halafu siamini kama hilo ni kweli. Kumbuka mkataba huu ulikuwa ni na serikali ya China, na kampuni ambayo ingejenga ni ya serikali ya China. China huwa wanachukia rushwa kuliko sisi, kwao kosa la rushwa ni kifo.
 
Magufuli hakusema anaupiga chini kwa sababu za masharti, alisema harufu ya ufisadi.

Kauli za Wakubwa hu generalize sana, hapakuwa na haja ya magu kusema pumba zote zilizomo mkatabanini, mikataba ya wachicha mostly huwa ni ya Ki******u sana, jaribu kuchunguzaga, refer mataifa mengi ambayo yalitekelezaga miradi ya kitaifa kupitia Mkopo wa kichina, ni lesson tosha.
 
Inawezekana, lakini pia usisahau JK Mrisho hawezi kukosoa hadharani, lazimaaongelee hilo suala positively
Upo sahihi mkuu, japo kwa jicho la kiinjinia na kibiashara ndo utajua jinsi gani SGR TZ inatishia maisha ya SGR Kenya hata bado haujaisha, ndo maana nao bado wanaweweseka kutafuta mkopo zaid kuibadili kuwa kama yetu kwani yao haitakua na ushindani kibiashara baada ya kukamilika SGR TZ.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kauli za Wakubwa hu generalize sana, hapakuwa na haja ya magu kusema pumba zote zilizomo mkatabanini, mikataba ya wachicha mostly huwa ni ya Ki******u sana, jaribu kuchunguzaga, refer mataifa mengi ambayo yalitekelezaga miradi ya kitaifa kupitia Mkopo wa kichina, ni lesson tosha.
Mkuu mbona kwenye Bandari Bagamoyo alisema wazi kwa nini aliupiga chini? Kwa nini afiche SGR lakini Bandari Bagamoyo amwage kila kitu?

NEW DELHI: Tanzania has suspended the construction of the China funded $10-billion Bagamoyo port project in a major setback for Beijing’s ambitious Belt and Road Initiative (BRI) project.

Magufuli has alleged that the China has presented “exploitative and awkward” terms in exchange for financing. Chinese financiers set “tough conditions that can only be accepted by mad people,” Magufuli told local media.

“They told us once they build the port, there should be no other port to be built all the way from Tanga to Mtwara south,” Magufuli told a delegation of business people at State House in Dar es Salaam on June 14.

Read more at:
Tanzania President terms China's BRI port project exploitative
 
Kwa hiyo tatizo lilikuwa mkataba sio ufisadi? Hivyo unavyosema huwa vipo kwenye mkataba. Sasa kama Watanzania tunakuwa mapoyoyo wa kukubali kila kinachopendekezwa kwenye mkataba basi hatuna akili.

Halafu siamini kama hilo ni kweli. Kumbuka mkataba huu ulikuwa ni na serikali ya China, na kampuni ambayo ingejenga ni ya serikali ya China. China huwa wanachukia rushwa kuliko sisi, kwao kosa la rushwa ni kifo.
Ha ha ha umenifanya nitanue mbavu kwa kicheko mkuu

Ila kumbuka China haitaki kitu inaitwa rushwa ukiwa nchini mwao ila sio nje ya China. Hapo ndo tunakuta makampuni mengi yapo Africa yanapewa Tenda afu yanafanya chini ya Viwango na kwa gharama kubwa kwa manufaa yao na wale wanao wahonga rushwa ili wapate hizo tenda mkuu.

MKuu niliwahi kuwauliza Wachina juu ya hil, kuwa kwa nini kazi zao za Ethiopia na USA ni nzuri sana high standard lakini kwetu wanaboronga?

Wakasema kwamba, wao serikali yao inawaambia jambo moja - wasijiingize kwenye kutoa rushwa kupewa kazi. Ila basi, kama serikali za nchi za nje ndio zinadai rushwa wawakubalie, lakini wachukue sehemu ya hiyo rushwa kwenye gharama za ujenzi bila kuathiri faida ya kampuni au serikali kama kampuni ni ya serikali. Kwa hiyo wanachofanya ni kupunguza quality ya kazi kwa kiwango cha rushwa walichotoa baada ya kudaiwa na mawaziri au hata raisi.

Wakasema Ethiopia hawadai rushwa na hata USA na Ulaya ndio maana utaona kazi wanazofanya huko ni za standard ya juu sana!
 
Huo ndo ukweli, rushwa katika nchi zinazoendelea ni suala mtambuka. Japo ni Muhimu pia kama kiongozi wa nchi kutumia maarifa mengi katika kung'amua upuuzi huo, kwani mwisho wa siku wananchi tutakuangalia wewe /Rais.

Kwa mfano, angalia serikali ya Uganda ilivyo pata tabu kujua ipi reli ya manufaa kwa nchi yake yaan Tanzania, Electric SGR from Diesel SGR Kenya. Pale paliibuka makundi kila mtu na Maelezo yake kumbe kila mtu anampigia chapuo Mteja wake ili 10% iingie na sio nchi kwa Ujumla itanufaikaje na Mradi husika. Hapo ndo utajua waafrika wengi ni viande na wachumia tumbo, uzalendo kushoto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati Magufuli anaingia madarakani alikuta Kikwete ametengeneza makubaliano na Wachina ya Kujenga SGR yote Dar hadi hadi Kigoma, na pia kutoka Uvinza kwenda mgodi wa Musongati wa Burundi na kufika Kaliua. Ilikua iende na Mwanza nadhani, kwa mkopo wa $7.6 Bilioni kupitia benki ya China ya EXIM na Kampuni ya Ujenzi ya Reli za serikali ya China. Magufuli aliitupia hii dili nje kwa madai kuwa ilikuwa na harufu ya ufisadi na kwamba tutajenga SGR kwa fedha zetu za ndani.

Sasa leo hii, zaidi ya fedha ambazo tayari tumezamisha kwenye SGR kipande cha Dar hadi Dodoma tu, tumekopa tena $ 1.46 Bilioni ili kukamilisha ujenzi wa SGR toka Dar hadi Makutopola. Hili linafanyika wakati TRC wanasema hadi sasa kipande kilichojengwa kimeshakula $1.3 Bilioni. Hii inamaanisha kwamba tunakopa $ 1.46 Bilioni kukamilisha sehemu ambayo tayari imekula $1.2 Bilioni. Kwa hiyo basi, hadi sasa kuanzia Dar hadi Makutopola gharama inaweza kufikia zaidi ya $3 Bilioni, ambayo ni karibu nusu (50%) ya mkataba ambao Kikwete na Wachina walikuwa watie sahihi kama gharama ya kujenga SGR yote, na Raisi Magufuli akatuaminisha Watanzania kwamba ule mkataba ulikuwa na harufu ya ufisadi.

Sasa wana JF mie nilishasema kuna mambo huwa simuelewi Magufuli. Kama kuna anaelewa juu ya hili basi naomba anifafanulie.

Usikute Kikwete na Wachina kwa sasa hivi wanacheka kweli kweli, na wanamcheka nani hilo halihitaji PhD kwa wewe kuelewa.

According to the Tanzania Railways Corporation’s latest reports on expenditure the project has so far spent an estimated $1.2 billion for two phases.The corporation’s project manager Machibya Kadogosa confirmed to The EastAfrican in an exclusive interview that, the two phases are currently being constructed by a Turkish firm Yapi Merkezi, in partnership with Portuguese firm Mota-Engil Africa.
Haukuwa na 10%
 
Jiwe anapiga fedha za mkopo!sio zote zinaenda kwenye ujenzi ndo mana fedha nyingi zinatumika bila mradi kukamilika kwa kasi kama inavodhaniwa kwa thamani ya fedha au mkopo husika!!!
 
Mh. Rais Magufuli muda mwingi amewaaminisha watanzania wajinga kuwa watangulizi wake walikuwa ni viongozi wabovu, mafisadi, wasioweza kusimamia, na waliokosa uzalendo. Na kwamba yeye ni nabii Musa. Na kwa vile Watanzania wengi ni wajinga, wanaamini na kushangilia.

Lakini nina hakika Magufuli mambo.mengi amayafanya kwa pupa sana. Na kwa vile kafanya kwa pupa, bila ya kuwashirikisha wataalam, mambo mengi ameyafanya vibaya na kuiingiza nchi kwenye hasara isiyo ya lazima.

Mabweni ya chuo kikuu alifuta kandarasi ya ujenzi iliyokuwa imepitishwa ya gharama ya sh 30 billion, akasema yatajengwa kwa 10 billion. Yakajengwa kwa 57 billion! Unapofikia hapo - nani fisadi, aliyepitisha tenda ya kuyahenga kwa bilioni 30 au wewe uliyesema utajenga kwa bilioni 10 halafu ukajenga kwa bilioni 57?

Ukiwa kiongozi ni vibaya sana kuamini kuwa unajua kila kitu, na wenzako wote hawajui chochote na hawaaminiki.
 
Mkuu mbona kwenye Bandari Bagamoyo alisema wazi kwa nini aliupiga chini? Kwa nini afiche SGR lakini Bandari Bagamoyo amwage kila kitu?

NEW DELHI: Tanzania has suspended the construction of the China funded $10-billion Bagamoyo port project in a major setback for Beijing’s ambitious Belt and Road Initiative (BRI) project.

Magufuli has alleged that the China has presented “exploitative and awkward” terms in exchange for financing. Chinese financiers set “tough conditions that can only be accepted by mad people,” Magufuli told local media.

“They told us once they build the port, there should be no other port to be built all the way from Tanga to Mtwara south,” Magufuli told a delegation of business people at State House in Dar es Salaam on June 14.

Read more at:
Tanzania President terms China's BRI port project exploitative

Mkuu, mtu hashikiwi mdomo na kuelekezwa cha kusema, kutokusema kwake yawezekana yawezekana kuna kulikuwa na mantiki sana kulinganisha na angesema ,
 
Back
Top Bottom