Rais Magufuli alijua mchezo wa wale askari waliosindikiza dhahabu lakini hajui Mo alitekwaje, kapatikanaje na mtuhumiwa kunywa chai na Mambosasa!

Jurrasic Park

JF-Expert Member
Sep 13, 2013
3,795
6,769
Habari

Rais Magufuli juzi alipo waapisha mh. Mahiga na mwenzake mh. Kabudi alitoa speech ya kushangaa ambapo alitanabaisha kwamba watanzania sio wajinga. Haina shaka Mo alitekwa na wasiojulikana na akaletwa na wasiojulikana huku IGP Sirro akitoa picha za gari linalosadikika ndo lilimteka Mo na kumrudisha japokuwa picha ya mbele na nyuma zilikuwa zikitofautiana.

Tukaona tena kwenye habari ya ITV ya saa mbili wakati kamanda Mambosasa alipouonyesha umma mtuhumiwa ambaye alikiri mbele ya kamera kwamba aliwapeleka wale wazungu waliomteka Mo stend ya mabasi Ubungo saa kumi usiku. Kwa vile sisi sio wajinga tukahoji inakuwaje mtuhumiwa anahojiwa na waandishi wa habari wakati watuhumiwa wengine wanapigwa makofi mbele ya kamera, huku wengine wakiwa na wasiwasi na uwoga, wengine wakifunika vichwa vyao lakini kwa yule jamaa alikuwa akihojiwa na yupe mwandishi alikuwa akijibu kwa ufasaha bila uwoga. Tushukuru technolojia, yule aliyehojiwa na waandishi wa habari tulimuona akiwa na dk. Shika kwenye show moja ya tv. Tukumbuke sisi sio wajinga.

Turudi Mwanza, Rais Magufuli akiwa ikulu alitoa mfano kwenye speech zake kwamba kuna polisi walifanya mchezo na waalifu ambao walitaka kutorosho dhahabu zaidi ya kilo 300. Alitupa mkasa kama naukumbuka vizuri, Rais Magufuli alisema kwamba wale watuhumiwa walipomkamata yupe mtuhumiwa mwenye dhahabu walimpeleka polisi kisha wakatoka naye. Waliendelea kuongea naye na yule mfanyabiashara mhalifu alitoa pesa akawapa wale askari kisha wakavuka naye kwenda visiwani. Baadaye wakawekewa mtego. Kilichotokea wakati wanajua wameshategwa wakapiga king'ora cha kufukuza mwizi.

Kinachonishangaza Rais Magufuli anakiri kwamba aliijua huo mchezo unaochezwa kule Mwanza ambako ni mbali ni mamia ya kilomita kutoka ikulu. Sasa kinachoshangaza Rais Magufuli hajui kilichotokea kwa Mo pamoja na picha picha za kipumbavu za IGP Sirro. Yaani umbali wa mita chache toka Mo alipotekwa hujui nini kilitokea lakini unajua kilichotokea Mwanza ukiwa umbali wa zaidi ya km 600 toka hapo ulipo. Umesema kweli sisi sio wajinga kisasi hicho.

Naona kamanda Mambosasa amekwisha tumika kama kondomu sasa kazi iliyobaki ni kuitupa chooni. Pamoja na kufunika kombe kwa Mambosasa lakini mnataka kumtoa kafara, wakati kwa shingo upande Mambosasa amefanya kazi yake kwa ueledi lakini kwa upumbavu wa aina yake. Ata kama mfamfukuza kazi au kumshusha cheo sisi sio wajinga tunajua kila kitu.

Naomba nirudie tena sisi watanzania sio wajinga?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unachekesha unajihangaisha na mtu unayejua kabisa ni Tapeli la kisiasa hivi nani hajui kwamba yeye ndio mpanga wa yote badala ya kupata heshima kwa kunyamaza kwake sasa ndio amejiangusha kwa sababu propaganda zake huwa hazina kichwa wala miguu jamaa anajulikana kwa uwongo asikuhangaishe
 
Habari

Rais Magufuli juzi alipo waapisha mh. Mahiga na mwenzake mh. Kabudi alitoa speech ya kushangaa ambapo alitanabaisha kwamba watanzania sio wajinga. Haina shaka Mo alitekwa na wasiojulikana na akaletwa na wasiojulikana huku IGP Sirro akitoa picha za gari linalosadikika ndo lilimteka Mo na kumrudisha japokuwa picha ya mbele na nyuma zilikuwa zikitofautiana.

Tukaona tena kwenye habari ya ITV ya saa mbili wakati kamanda Mambosasa alipouonyesha umma mtuhumiwa ambaye alikiri mbele ya kamera kwamba aliwapeleka wale wazungu waliomteka Mo stend ya mabasi Ubungo saa kumi usiku. Kwa vile sisi sio wajinga tukahoji inakuwaje mtuhumiwa anahojiwa na waandishi wa habari wakati watuhumiwa wengine wanapigwa makofi mbele ya kamera, huku wengine wakiwa na wasiwasi na uwoga, wengine wakifunika vichwa vyao lakini kwa yule jamaa alikuwa akihojiwa na yupe mwandishi alikuwa akijibu kwa ufasaha bila uwoga. Tushukuru technolojia, yule aliyehojiwa na waandishi wa habari tulimuona akiwa na dk. Shika kwenye show moja ya tv. Tukumbuke sisi sio wajinga.

Turudi Mwanza, Rais Magufuli akiwa ikulu alitoa mfano kwenye speech zake kwamba kuna polisi walifanya mchezo na waalifu ambao walitaka kutorosho dhahabu zaidi ya kilo 300. Alitupa mkasa kama naukumbuka vizuri, Rais Magufuli alisema kwamba wale watuhumiwa walipomkamata yupe mtuhumiwa mwenye dhahabu walimpeleka polisi kisha wakatoka naye. Waliendelea kuongea naye na yule mfanyabiashara mhalifu alitoa pesa akawapa wale askari kisha wakavuka naye kwenda visiwani. Baadaye wakawekewa mtego. Kilichotokea wakati wanajua wameshategwa wakapiga king'ora cha kufukuza mwizi.

Kinachonishangaza Rais Magufuli anakiri kwamba aliijua huo mchezo unaochezwa kule Mwanza ambako ni mbali ni mamia ya kilomita kutoka ikulu. Sasa kinachoshangaza Rais Magufuli hajui kilichotokea kwa Mo pamoja na picha picha za kipumbavu za IGP Sirro. Yaani umbali wa mita chache toka Mo alipotekwa hujui nini kilitokea lakini unajua kilichotokea Mwanza ukiwa umbali wa zaidi ya km 600 toka hapo ulipo. Umesema kweli sisi sio wajinga kisasi hicho.

Naona kamanda Mambosasa amekwisha tumika kama kondomu sasa kazi iliyobaki ni kuitupa chooni. Pamoja na kufunika kombe kwa Mambosasa lakini mnataka kumtoa kafara, wakati kwa shingo upande Mambosasa amefanya kazi yake kwa ueledi lakini kwa upumbavu wa aina yake. Ata kama mfamfukuza kazi au kumshusha cheo sisi sio wajinga tunajua kila kitu.

Naomba nirudie tena sisi watanzania sio wajinga?

Sent using Jamii Forums mobile app
Inategemeana na "Intelligence"
 
Ile ni drama tu kama drama ya mafao. Kwamba mswada utungwe, ujadiliwe na baraza la mawaziri ambako yeye ndie chairman, upewe idhini ya kupelekwa bungeni, utangazwe kwenye gazeti la serikali, usomwe bungeni mara kadhaa, wabunge wajadili, wanaharakati wapige kelele usijadiliwe, mswada upitishwe na bunge, upelekwe kwake, ausaini kua sheria, watu waanze kukatwa mafao yao, ipite miezi kadhaa ndio aje kujifanya hakujua, awaite wote pamoja wamwambie nini kinaendelea kisha atumbur mkuu wa mifuko.

Ni ajabu kweli kweli.
 
Naomba nirudie tena sisi watanzania sio wajinga?

Ngoja nikupe mbinu mkuu, kama bado hujapata wazo hili kichwani mwako.

Sisi Waafrika, na hasa waTanzania tunashindwa kuona fursa kila zinapojitokeza.

Hadithi yako hii ina thamani ya mabilioni ya shilingi ukijua kuzichimba. Kama sio wewe, basi yeyote atakayetaka aitumie fursa hii kuokota haya mabilioni miaka michache ijayao.
Kuna bonge la movie hapa. Atakayetaka kuyaweka yote haya kwenye kitabu/sinema, atavuna vyema jasho la juhudi zake.

Jurrasic, umekwishaonyesha mwanzo mzuri, bila shaka wazo hili utalifanyia kazi.
Kwanza jina lako tu 'Jurrasic' Park - lina mwelekeo wa kutoa bonge la movie 'blockburster' kama mwajina wako! Utashindwaje kazi hii rahisi ukilinganisha na hiyo iliyotengeneza movie yako?
 
Ile ni drama tu kama drama ya mafao. Kwamba mswada utungwe, ujadiliwe na baraza la mawaziri ambako yeye ndie chairman, upewe idhini ya kupelekwa bungeni, utangazwe kwenye gazeti la serikali, usomwe bungeni mara kadhaa, wabunge wajadili, wanaharakati wapige kelele usijadiliwe, mswada upitishwe na bunge, upelekwe kwake, ausaini kua sheria, watu waanze kukatwa mafao yao, ipite miezi kadhaa ndio aje kujifanya hakujua, awaite wote pamoja wamwambie nini kinaendelea kisha atumbur mkuu wa mifuko.

Ni ajabu kweli kweli.

Oooh, Aisee nimeshindwa kujizuia kutoa kicheko cha sauti na si tabasamu tu!
 
..hili swala la mo passion si tulishafunika kombe baada ya ku make conclusion zetu kwa yale yalitokea
NIKUKUMBUSHE,SIKU MOJA KABLA YA MO DEWJI KUTEKWA KUNA MTU MMOJA MWENYE CHEO AITWAYE DAUDI BASHITE ALITOA AMRI KESHO YAKE SA KUMI NA MOJA ALFAJIRI VIONGOZI WA U DART WAKUTANE NAYE OFISINI KU DISCUSS USAFIRI WA MWENDOKASI CHANGAMOTO ZAKE,SAA 11 ALFAJIRI????????MUDA HUO HUO MO ALITEKWA NA HUYO JAMAA ALITOA CONTROVERSIAL STATEMENTS HADI KUMTISHA MILARD AYO AFUTE KWENYE WEBSITE YAKE KWAMBA MO KAPATIKANA NA HIYO NI BAADA YA YEYE KUTANGAZA
FAST FOWARD ,JAMAA NI SHABIKI WA SIMBA ILA ALIKOSEKANA KWENYE HIGH PROFILES MECHI ZA SIMBA ZAIDI YA 6 KIKAWAIDA HUWA HAKOSI,WENYE AKILI TUKAJUA NI GUILTY CONSIOUSNESS AMBAYO HATA SHETANI ANAYO SEMBUSE VIJUKUU VYAKE DUNIANI,NIA AIBU YA KUMUANGALIA USONI MO DEWJI
KAIBUKA MECHI YA SIMBA VS YANGA YA MWISHO SABABU JANA YAKE MO NA VANESAA MDEE WALIPOST WAKIWA WANA FLY KWENDA ABROAD
NA M DARE ATOKEE MECHI YA SIMBA NA AS VITA YA CONGO UWANJA WA TAIFA IN FEW DAYS AMBAYO MO DEWJI ATAKUWEPO
ALL THE BEST,MO DEWJI,MUNGU AKUBARIKI,ANZA KU INVEST NA NCHI NYINGINE SAMBAZA HELA YAKO KWINGINE TANZANIA YETU TUNAYOIPENDA MSKINI YA MUNGU NDO HIVYO TENA, HAIELWEKI SASA HIVI.AWAMU YA WANA MWANZA NI HATARI HII.
 
Ogopa sana kuwa na kiongozi anayetoa kafara kwa wasaidizi wake for the sake of popularity

Back
Top Bottom