Rais Magufuli akutana na Wilson Masilingi, Philip Marmo na Jenerali George Waitara Ikulu Dar

MLAU

JF-Expert Member
Aug 23, 2007
4,726
3,354
Rais Dkt Magufuli akutana na Mabalozi Wilson Masilingi na Philip Marmo pamoja na mkuu wa Majeshi mstaafu Jenerali George Waitara Ikulu Dar es salaam
ma1.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Wilson Masilingi aliyekutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 12, 2016
ma1a.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Wilson Masilingi aliyekutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 12, 2016.
ma2.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya kitabu kutoka kwa Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali George Waitara aliyekutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 12, 2016.
ma2a.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akiagana na Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali, George Waitara baada ya kukutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 12, 2016
ma4.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani Mhe: Philip Marmo alipokutana naye Ikulu jijini Dar es salaam leo Oktoba 12, 2016
 
Gen. Waitara ameandika kitabu? kinahusu nini?

Kama ameandika, kwa kweli ni suala la kupongeza maana wengi wetu hatuna utaratibu wa kuandika ili kusaidia vizazi vijavyo! Tunakufa na mawazo mazuri, kumbukumbu nzuri etc.

Wengine husema makaburi ndio sehemu pekee yenye utajiri mkubwa. Naweza kukubaliana nao!
 
Nitampongeza sana tena sana kama kaandika kitabu nitakuwa wa kwanza kukinunua na kukisoma.
 
Kama kaandika kitabu brgd mstaafu huyo anastahili PONGEZI,maana maprofesa wetu hatuwasikiagi au kiwaona wakiandika vitabu...kutwa kukimbilia ktk siasa...

OVA
 
Ila nampongeza kwa kuandika kitabu
Maana watu wengi wanaotumia nguvu huwa hawajishughulishi na mambo ya kitaaluma

Ningetamani na mimi nikisome

Ila kwanini alistaafu akiwa kijana sana?
 
Mkuu huyo akiandika kitabu kitaeleweka kweli??nahisi kama naongea point sana.
.nahisi

Gen. Waitara ameandika kitabu? kinahusu nini?

Kama ameandika, kwa kweli ni suala la kupongeza maana wengi wetu hatuna utaratibu wa kuandika ili kusaidia vizazi vijavyo! Tunakufa na mawazo mazuri, kumbukumbu nzuri etc.

Wengine husema makaburi ndio sehemu pekee yenye utajiri mkubwa. Naweza kukubaliana nao!
 
Attachments

  • VID-20160417-WA0006.mp4
    4 MB · Views: 46
Kwahiyo walichoongea katika mkutano huo ni kitabu tu? Tumegeeni kidogo walizungumza juu ya nini?
 
Aliyekuambia hawajishughulishi na mambo ya kitaalamu nenda kamuulize tena leo au akiwa na akili zake timamu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom