Rais Magufuli akutana na Wafungwa na mahabusu katika gereza la Butimba, awaambia yeye ni mfungwa wa baadae

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,512
141,240
Rais Magufuli anawasikiliza wafungwa na mahabusu katika gereza la Butimba.

Hakika huyu ni Rais wa Wanyonge!

=====

Rais John Magufuli leo Julai 16, 2019, amefanya ziara katika bandari ya Mwanza South kukagua ujenzi wa meli mpya na ukarabati wa meli mbili zinazoendelea kutengenezwa, MV Victoria na MV Butiama ambazo zitakamilika mwezi wa tatu mwakani.

"Huyu wa TPA yupo wapi? Njoo hapa, haya jibu haya maswali kwa nini hamuwalipi mishahara vizuri? Mnawabebesha mizigo mingi mpaka huyu baba ameshindwa kununua viatu vizuri na suruali yake ina viraka kwa sababu hamumlipi vizuri?" Rais Magufuli

MWANZA: Rais John Magufuli leo ametembelea Gereza la Butimba mkoani Mwanza ambapo amepata fursa ya kuzungumza na wafungwa na maofisa wa gereza waliotoa kero zao.

“Rais kuna Afisa Usalama yuko huku ndani ana anawapa Wafungwa simu halafu zikikamatwa tunanyan’ganywa vitu vyetu lakini hadi leo hajafanywa kitu chochote" Mfungwa Kalikenya Nyamboge

Mwanza Butimba “Mheshimiwa rais huyu ofisa akupe mihuri na hizo simu uondoke nazo utajua mwenyewe utaenda kufanyia nini na ikibidi ondoka naye kwani ukifanya hivyo utakuwa umetusaidia sana na ukimuacha atanidhuru,” - Mfungwa wa miaka 30

"Hata sisi mnaotuona hapa mbele ni wafungwa wabaadae, mtu ukiwa mahabusu au mfungwa haikuzuii kupata haki za utu wako, mimi ni Rais wa wanyonge ndio maana nimeamua kupita hapa kuwasalimu". Mhe. Rais Dkt Magufuli akiwa katika gereza la Butimba jijini Mwanza leo.

 
Maneno uumba dikteta bashiru alisahau kuyakarabati magereza ya sudani alipotupwa Gerezani akaanza kulalamika gereza baya. Matumizi mabaya ya Madaraka, matumizi mabaya ya fedha za umma, upotevu wa watu wajiandae tu kuyakarabati magereza ili maneno ya Chid benzino yatimie.Wakati mwingine huwa tunayatabiri ya mbeleni Bila kujua.
 
Kuna askari magereza alijifanya anajua kufunguka ,,kakoswakoswa kung'olewa nyota,kam-please ile mbaya Magufuli,alimanusura,ana mungu wake,afanye sana ibada
 
Back
Top Bottom