rmdmfaume
Member
- Dec 26, 2017
- 14
- 1
nzuri hiyo ndugu njirembela wew n mwl etiKuna tatizo linalonyemelea taifa. Bahati mbaya kauli ya Rais ni amri..
Sijaona sababu ya kuwaita mawaziri wale wawili Ikulu kuwapa maagizo. Mmoja ni Waziri ndani ya ofisi yake na mwingine wa Elimu. Ningekuwa yeye (lakini siitamani kazi yake hata kwa mabilioni) lingekuwa ni suala la baraza zima la mawaziri, baada ya kupokea ushauri kutoka Wizara zote au Kurugenzi za Elimu. Sio kweli kwamba walimu wanachangisha hela wanafunzi kwa manufaa yao. Hali ni mbaya sana mashuleni, na kile wanachoweza hukitumia mara na wapo wazazi wanaweza kushuhudia hili.
Kinachofanyika sasa ni kufanya zile shule ambazo changamoto yao kubwa ilikuwa ni gharama za kujiendesha- maana ya vitabu na madaftari, na sasa walikuwa wanaelekeza jitihada kwenye kuboresha, kukata tamaa. Wakurugenzi wengi ni wageni- wana majukumu makubwa ya kisekta. Ujuzi wangu mdogo unaashiria katazo jipya hasa kwenye maeneo ambayo shule hazifikiki kiraisi. Ni vigumu kuona mzazi akienda kutoa mchango wa hiari kupitia MKURUGENZI- kwani mwishoni Mwl Mkuu ndiye mtekelezaji.
Naona taifa linanyemelewa na mfumo wa papo kwa papo bila kujali tunakopaswa kuendelea.