peno hasegawa
JF-Expert Member
- Feb 24, 2016
- 12,797
- 21,392
Prof ndalichako,ninakushauri,jitafakari Sana, wizara ya elimu imekushinda, au umuombe mh Rais aigawanye uwe wizara mbili. Kwa hali ilivyo , na kwa Kasi ya Rais wetu na serikali yake unashikwa pabaya. Wazazi walianza kuchangishwa fedha tango December 2017, hadi Rais anakuja kukuambia Jana Ina maana ulikuwa huna habari? Mungy nisamee tulikutarajia utafanya makubwa baada ya kuchaguliwa ILA tumekata tamaa kabisa na utendaji Wako.vyuo vya ualimu vimechoka,idara za elimu kwenye halimashauri zimechoka,walimu wamekata tamaa, majengo ya sule na vyou yamechoka,vyuo vikuu navyo hivyo hivyo.Jembekillo,
Mkuu,
Neno Elimu bure kwa kiswahili nilichosoma darasani miaka mimgi sana ni sentensi zenye maana zaidi ya mbili ila moja chanya ya pili ni hasi.
Hata Elimu bila malipo nayo ni yale yale.
Yaani, zinatoa maana zaidi ya mbili ambapo moja inakinzana moja kwa moja na ile iliyokusudiwa.
Mfano,
Rais, anasema "Elimu Bure"
Kwanza: Elimu pasi kutoa michango.
Pili: Elimu bure ni aina ya Elimu isiyo kuwa na tija au faida kwa mpokeaji.
Waziri. Anasema, Elimu bila malipo,
Kwanza : Hautoi hela kuipata hiyo Elimu.
Pili: Haitakusaidia maana, haina mrejesho chanya kwa anayesoma.
Kwa hiyo, wote wanapambana kutumia neno lenye muonekano na tafsiri chanya tu ila kwa bahati mbaya kiswahili kinawatupa mkono wote wawili katika kuchagua sentence au kauli mbiu sahihi.
Wangeweza kusema "Serikali itagharimia mahitaji yote ya wanafunzi kuanzia ngazi ya darasa la 1 hadi kidato cha 4".