Rais Magufuli leo tarehe 05 Feb2020 amekutana na Balozi wa Umoja wa Ulaya Mr. Manfred Fanti Ikulu jijini Dar es salaam. Mr. Fanti amesema mazungumzo yake na JPM yamekuwa ya manufaa makubwa ambayo yalijikita katika maendeleo ya Tanzania na kuimarisha ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanazania na EU.
Fanti katika mazungumzo yake amesema hivi karibuni EU wamekamilisha mazungumzo yao juu ya mpango wao wa kuendelea kuchangia katika budget ya maendeleo ya Tanzania ambapo 132 billion zilizokuwa zimezuiliwa sasa zitatolewa kwa ajili ya kuchangia katika budget ya maendeleo ya Tanzania, kwani wamefurahishwa na maendeleo makubwa yanayoendelea hapa nchini.
Wakati huo huo wanaandaa mpango mwingine wa miaka 7 ambao unaanza mwaka huu wa 2020.
Wakati huo Rais Dk. Magufuli amemshukuru Mh. Balozi Fanti kwa kazi nzuri anayofanya ya kudumisha ushirikiano mzuri kati ya Tanzania na Umoja wa Ulaya (EU).
Sent from my iPhone using JamiiForums