Rais Magufuli akumbuka 'viboko' vya Mwalimu Nyerere

diana chumbikino

JF-Expert Member
May 29, 2018
428
368
1571114853625.png


Rais John Pombe Magufuli amesema miongoni mwa vitu ambavyo Mwalimu Nyerere alikuwa akivikemea ni rushwa na kueleza alihakikisha watuhumiwa wa rushwa, walikuwa wakicharazwa bakora 12 wakati wa kuingia jela na kutoka.

Ametoa kauli hiyo mkoani Lindi, wakati akihutubia kwenye kilele cha Mbio za Mwenge nchini, iliyoendana sambamba na kumbukumbu ya miaka 20 ya kifo cha Mwalimu Nyerere.

Aidha Rais Magufuli amesema Serikali yake imemkumbuka kwa kutekeleza masuala mbalimbali ikiwemo kujenga viwanda, kutoa elimu bure.

"Wote mnakumbuka Mwalimu Nyerere alikuwa hapendi rushwa, na yeyote ambaye alijihusisha na vitendo vya rushwa alipigwa bakora kabla ya kutoka na baada ya kutoka jela, kupitia hotuba zake nadhani mnajua hili."amesema Rais Magufuli

Ameendelea kwa kusema, "Naikabidhi hii ripoti kwa TAKUKURU ukaikague, uiangalie wale wanaotakiwa kupelekwa mahakamani na wale ambao unaona huwawezi niletee ripoti zao, nataka Tanzania inyooke.".
 
Hajakumbuka "uhuru wa kutoa maoni"?
Anakumbuka Tu Mawili kati ya mema Mia moja.
Watu hawamtaki na hawajamuelewa hata kidogo. Ushahidi ni Kujiandikisha Kupiga kura, hana Ushawishi anatumia Nguvu kubwa Mpuuzi tu halafu anajilinganisha na Nyerere. Hovyo kabisa huyu Mtu.
 
Yeye kaona “viboko”?

Watu wenye IQ za mashaka hata uwape madaraka makubwa kiasi gani,IQ ni ni shaka tu,hua haibadiliki!
 
Back
Top Bottom