Rais Magufuli akipata Katiba Mpya tutafika mbali

SHILINDE

Member
Jul 23, 2010
14
6
Tukiacha ushabiki, kila mtu hawezi kubisha kwamba kasi ya usimamizi na utekelezaji wa shughuli na sera anazofanya Mh. JPM kwa sasa, na akipata Katiba Mpya tena ile ya Warioba akaisamia haswaaa, kwa kweli tutafika mbali,
sifa kuu tatu za JPM zinazonifanya niseme haya ni pamoja na
1. Kuweza kuthubutu
2. Kuweza kufanya maamuzi magumu
3. Kusimamia kile anachoamini

Tanzania ya sasa inamuhitaji JPM akiwa na Katiba Mpya.
 
Hii iliyopo anaiheshimu? Kikubwa inatakiwa rais aheshimu na kufuata katiba kama sivyo hata ukileta katiba ya Africa kusini ni kazi bure
 
Hii ya sasa yenyewe imeshindikana kwa mambo kadhaa ambayo yapo na yanakiukwa, hata kama tukikubaliana na wewe kuwa ina udhaifu; je hiyo ya Warioba ndo itawezekana!?

NB: Kutokamilika kwa mwanadamu hakupi uhuru wa yeye kufanya dhambi.
 
Hii iliyopo anaiheshimu? Kikubwa inatakiwa rais aheshimu na kufuata katiba kama sivyo hata ukileta katiba ya Africa kusini ni kazi bure

Katiba inaweza kutokuheshimika kwa sababu hai command respect. Ninaungana na mtoa hoja. Magufuli akipata katiba mpya bila shaka tutafika mbali sana kwa asilimia 200. Nina sababu nyingi sana za kusema hivi.

Kwa sasa anaweza kufanay lolote lile kama wengine walivyofanya bila hofu kwa sababu katiba inampa uhuru wa kufanya lolote bila madhara. Pale katiba itakapopunguza madaraka yake, bila shaka atalazimika kushirkisha vipaji vingine na taaluma zingine katikam maamuzi.

Pale katiba itakapoondoa kinga ya kushitakiwa hata akivurunda, bila shaka atafanya maamuzi kwa ufahamu zaidi.

Katiba itakapoondoa u Mungu mtu wa raisi, itatoa mwanya kwa watu kufanya kazi kwa kujiamini na adabu kwa kujua matokeo ya ujinga wowote wenye uharibifu, ytakuwa juu ya vichwa vyao.

NA HII SI KWA MAGUFULI TU, BALI KWA KILA RAISI WA NCHI KAMA TUNATAKA MAFANIKIO, MAENDELEO, UHURU SAHIHI NA DEMOKRASIA.
 
Hii ya sasa yenyewe imeshindikana kwa mambo kadhaa ambayo yapo na yanakiukwa, hata kama tukikubaliana na wewe kuwa ina udhaifu; je hiyo ya Warioba ndo itawezekana!?

NB: Kutokamilika kwa mwanadamu hakupi uhuru wa yeye kufanya dhambi.

Unaonaje kama katiba ingesema raisi atashitakiwa kwa makosa atakayofanya akiwa madarakani wakati ama baada ya utawala?

Unaonaje kama katiba ingesema mawaziri na teuzi zote za kitaalmu hazitafanywa na raisi bali kutakuwa na vyombo vitatu vya kuchuja majina na vyombo hivyo haviwajibiki kwa raisi?

Unaonaje pale ambapo uchaguz wa viongozi ungesimamiwa na bodi inayojumuisha watu wa mataifa mbalimbali (kwa mfano) ambao hawafungamani na raisi wala viongozi wa siasa?

Katiba inavunjwa kwa sababu haina nguvu na imetoa mianya mingi ya kuvunjwa. Hilo ndilo tunataka tuliondoe. Katiba iwe na meno dhidi ya wahalifu wote bila kuajili vyeo vyao.
 
Mkuu wa kaya alishaweka bayana ya kuwa katiba mpya kwake siyo kipaumbele, kwa hiyo nae amekubali kutumia katiba mbovu ambayo inahararisha uovu, na ndio maana maamuzi mengine yanaenenda kinyume na sheria za nchi
 
Ni kitu gani ambacho umekiona hadi kusema ya kuwa mkuu waa kaya angepata katiba mpya angelifikisha taifa mahali fulani? ni katiba ipi mpya unayoisemea? Maana yeye alishaweka bayana ya kuwa katiba mpya kwake siyo kipaumbele, lakini la kujiuliza ni je, anaheshimu hii iliyopo mbali na ubovu wake?
 
Back
Top Bottom