Rais Magufuli akijibu maswali haya atakuwa Rais bora wa Afrika wa karne ya 21

KooZito

JF-Expert Member
Dec 14, 2020
218
1,000
Nawasalimu wanabodi!

Tunaposema haya si kwamba tunamchukia Rais wetu, hapana. Tunampenda sana. Tunampenda afanikiwe maana akifanikiwa Taifa limefanikiwa kwa ujumla. Hivyo basi, hata wapambe wake wajue hivyo.

Aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Marekani Robert Jackson anasema, "Si kazi ya Serikali kuwafanya raia wasianguke kwenye makosa Bali ni kazi ya raia kuifanya Serikali isianguke kwenye makosa" na kwa mantiki hiyo ni jukumu la raia kuifanya Serikali isifanye makosa ni kupitia ukosoaji, ushauri na usifiaji inapostahili.

Kwa mantiki hiyo, ukimya wa raia kuhusu mambo ya hovyo yanayotendwa na Serikali ni kuiangamiza umma, ni kuua watu. Binafsi ninaamini Dk. John Pombe Magufuli akinijibu maswali yafuatayo atakuwa Rais muungwana na wa pekee sana Afrika na duniani kwa ujumla.

(1). Magufuli ni Mkatoliki Safi aliyekataa hata kusaini hati za kunyonga watu. Je, Rais wangu unaamini kwa moyo wa dhati kabisa ulishinda Urais 2015 na 2020?

(2). Rais wangu, tunaimbiwa mapambio ya "uchumi wa viwanda", "hapa kazi tu", "uchumi wa kati", hivi, nini falsafa ya utawala wako?

(3). Rais wangu, kuna vijana Ben Saanane na Azory Gwanda "walipotea". Wapo wanaosema wamejipoteza, wapo wanaoamini walitekwa na wanausalama wako. Wewe unaamini au kudhani vijana hawa wako wapi?

(4). Rais wangu, ni lini uchunguzi au upelelezi kuhusu kushambuliwa kwa mwanasiasa mwenzio Tundu Lissu utakamilika? Je, huoni kuna haja ya kuhusisha wataalamu kutoka nje kwa gharama ya familia kama CIA, Mosad au Scotland Yard kusaidia kuwatambua "wasiojulikana"?

(5). Rais wangu, unadhani uamuzi wa kuwatimua wale wanafunzi 8000 kutoka UDOM na kuwaita vilaza ulikuwa sahihi?

(6). Rais wangu, unadhani uamuzi wa kupora hela za watu katika maduka ya kubadili fedha kwa kutumia JWTZ na kuwafilisi ulikuwa sahihi?

(7). Rais wangu, tumechelewa Maendeleo lakini ulikabidhiwa nchi inayohishimu Sheria. Je, unadhani uamuzi wako wa kununua madege bila kufuata Sheria ya ununuzi kupitia Bunge ulikuwa sahihi? Unajua unadaiwa chenchi?

(8). Rais wangu, ule muswada uliopeleka Bungeni kwa hati ya dharura kwamba wewe, jaji Mkuu na Spika wa Bunge wasishitakiwe kwa makosa yao enzi za uongozi wao ulimaanisha nini? Je, unahisi kuna kosa umetenda ukistaafu ungeweza kushitakiwa kwayo?

(9). Rais wangu mpendwa, hupangiwi kazi, lakini, ni kwa makosa gani walifanya ukawatimua kazi Ernesti Mangu na Kapilimba? (IGP) na DG-TISS?

(10). Rais wangu, unaamini kuwa kuwachukia, kuwabagua na kuwatenga wanaokoaoa utawala wako ni uamuzi sahihi wenye busara na hekima? Unaamini katika kutesa wanasiasa wa upinzani?

(11). Rais wangu, bado unaamini kuwa kila aliyefanikiwa kimaisha ni mpiga dili? Utawapata wapi mabilionea wa kitanzania unayohubiri?

(12). Rais wangu, ulivyoingia madarakani ulikuta kuna shimo la Tanzanite maarufu kama "shimo la Mwarabu" linalotema madini hayo kuliko mashimo yote. Shimo hilo Jakaya alimpa mzungu wa Afrika Kusini aliyemsaidia fedha za kampeni 2005. Umempora mzungu huyo ukajimilikisha wewe kama wewe kupitia kwa kijana wako Dotto Biteko. Umevuna madini ya thamani ya 7T Kagame akakuzima mazima baada ya kumpa akuuzie. Je, ni kweli taarifa hizi?

(13). Rais wangu, ni kweli Rostam Aziz amekutapeli mabilioni za Uchaguzi akatokomea Canada na sasa hamuongei? Kwamba ulimruhusu kuingiza pesa nchini kumsapoti Lissu ili zipigwe akapiga yeye?

(14). Rais wangu, ni kweli Tanzania jakuna janga la Corona? Je, una mpango wa kuagiza chanjo ya ugonjwa huo?

(15). Rais wangu, kelele za kutaka kuifanya Chato kuwa Ulaya badala ya Tanzania unazichukuliaje? Ni kweli au uzushi za wasiokupenda?

(16). Rais wangu, kuna taarifa kuwa baraza lako la Mawaziri umejaza Wakatoliki wa Kanda ya Ziwa, ni kweli mambo haya?

(17). Rais wangu, mtu anayeitwa NAJIM ZUBERI MSENGA ni katika utawala wako? Nani bosi kati yake na Dotto James wa Hazina?

(18). Rais wangu, ni kweli ulimwekea "bambi" Bernard Membe asiwe Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola 2016 licha ya kukubalika na wenzio wote wa EAC na ndio ugomvi wenu uliofikia ngazi ya familia?

(19). Rais wangu, kwa nini unataka kumfukuza kazi Dk. Bashiru Ally? Je, ni kwa sababu amekataa kuondoa ukurasa unaogusa #$@&+ kwenye ripoti ya Mali za chama?

(21). Rais wangu, ni kweli unatumia ripoti hii kama rungu kudhibiti wanaotaka Urais 2025 kwa kuwatishia "tukutane Kisutu" kwa uhujumu uchumi?

(22). Rais wangu, ni kweli wapinzani hawakushinda Ubunge nchi nzima?

(23). Rais wangu, ni kweli umeachana na wazungu kasoro Ufaransa (kuwapa gesi Total) na sasa maisha ni Uchina?

(24). Rais wangu, ni kweli umeteka nyara fedha za mwekezaji kutoka Oman bilioni 480 aliyetaka kuwekeza huko nyumbani Arusha kwenya madawa ya binadamu?

(25). Rais wangu, katika moyo wako wa ndani kama Mkristo, unadhani unaongoza vizuri inavyostahili? Unadhani wananchi wanakufurahia au unashambuliwa na ugonjwa wa. "huwezi kupendwa na wote" ambao ni ndwele ya waliofeli uongozi?

Rais wangu, maswali yako 101. Naomba leo niishie hapo. Unaweza kujibu hadharani au sirini au kwa kutumia washangwena wako.

Ahsante Rais wangu. Ukiyajibu maswali hayo, hakika utakuwa kiongozi wa aina yake Afrika. Tujenge nchi yetu.
 

mcTobby

Senior Member
Feb 16, 2018
157
250
Swali la nyongeza pia. Je, ni kweli wapinzani wanakwamisha maendeleo ya Tanzania kama inavyodaiwa na wewe?

Hivi ni kweli serikali imeshindwa kuajiri watu wengi tokea 2015?

MÊmENtO HoMO
 

Msingida

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
7,083
2,000
Swali lingine;
Walivyoongeza retention ya 6% kwenye rejesho la mikopo ya heslb kwa mwaka alikuwa na lengo la kuwaumiza na kuwadhoofisha kimapato wanaufaika wa mikopo hiyo?
 

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
27,367
2,000
Raisi bora iwe Afrika au popote duniani hapimwi kwa uwezo wa kujibu maswali hupimwa kwa uwezo wa kuletea wananchi maendeleo yanayoonekana

Kazi ya uraisi sio kujibu maswali
 

Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
7,214
2,000
Nawasalimu wanabodi!

Tunaposema haya si kwamba tunamchukia Rais wetu, hapana. Tunampenda sana. Tunampenda afanikiwe maana akifanikiwa Taifa limefanikiwa kwa ujumla. Hivyo basi, hata wapambe wake wajue hivyo....
Huu Uzi nitausoma deile warahiiii Kuna maswali magumu hata quantum physics ikasome.
 

Superbug

JF-Expert Member
Jan 31, 2018
7,214
2,000
Maswali kuhusu lisu Ben azory yanamuondolea sifa ya kuwa mkatoliki mzuri na kumfanya aache legacy yenye doa akistahafu damu zile zitaendelea kumuuliza tulikukosea Nini?
 

pilipili--mbuzi

JF-Expert Member
Dec 2, 2020
774
1,000
Raisi bora iwe Afrika au popote duniani hapimwi kwa uwezo wa kujibu maswali hupimwa kwa uwezo wa kuletea wananchi maendeleo yanayoonekana

Kazi ya uraisi sio kujibu maswali
Kwani Libya ilikuwa haina maendeleo wakati canali Muhammar Gadhafi anapinduliwa? Kuna vigezo lukuki.
Kwani Nani rais Bora Africa?
 

Mtuflani Official

JF-Expert Member
Dec 31, 2019
982
1,000
Swali la nyongeza pia .je ni kweli wapinzani wanakwamisha maendeleo ya Tanzania kama inavyodaiwa na wewe?
Hivi ni kweli serikali imeshindwa kuajiri watu wengi tokea 2015?.

MÊmENtO HoMO

Waliondolewa ili wasiongelee yanayofanyika Chato kama tunavyo ona!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom