Rais Magufuli, akiharibu kwa Lissu na Zanzibar basi Serikali yake itapata tabu sana

Hivi kwa nini SMS zako zote zinaonyesha kuiombea nchi na viongozi wake mabaya, utafikiri machafuko yakitokea wewe utabaki salama?

Ametoa tahadhari nzuri, viongozi wawe makini. Kama wakishindwa kutenda haki kwenye uchaguzi huu na nchi ikadumbukia kwenye lindi la umwagaji damu basi hata wao hawatakuwa salama. Mkono wa sheria utawafikia
 
Hivi kwa nini SMS zako zote zinaonyesha kuiombea nchi na viongozi wake mabaya, utafikiri machafuko yakitokea wewe utabaki salama?
Mpuuzi wewe, hivi anayeiombea mabaya nchi ni nani? Mimi ninayeonya waache maovu au hao wanao ng'ang'ania kutenda maovu bila kusikia kilio cha wanaowatendea au wanao waonya?
Yaani kwa upuuzi wako wewe unaona viongozi kusweka watu ndani kwa kubambika kesi, kuumiza, kunyima Uhuru na kutumia madaraka vibaya ni sawa tuu Ila kuonywa ndio kuitakia mabaya nchi?
Ukiitwa mpuuzi usishangae
 
Kuna hofu kubwa huko Lumumba kuhusu upepo wa Lissu. Hawakuutegemea, walijua Lissu ataufyata kama walivyoufyata wapinzani wengine kutokana na kashkash waliyowatia ndani ya miaka hii mitano, lakini wamekuta ndiyo kwanza Lissu hapepesi macho, ndiyo kwanza anakamua tu bila wasiwasi wowote.

Imefikia hatua wanatamani wamtoe uwanjani ili wafunge magoli bila timu pinzani. Ila sasa tatizo ni moja. Wakimtoa Lissu kwenye kinyang'anyiro kwa staili waliyotumia kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa, dunia nzima inaona!. Lissu ametengeneza marafiki wengi duniani, tena wale ambao ni wa muhimu kwetu kama Taifa. Nchi za umoja wa Ulaya zinafuatilia kwa makini kila hatua katika uchaguzi huu. Iwapo zitafanyika njama za kumuengua Lissu kimagumashi basi Rais Magufuli kama atakuwa yeye ndiye rais kuanzia mwaka 2021 ajiandae kuendesha serikali yenye hali ngumu sana ya kiuchumi kwa sababu wahisani wataondoa mikopo na misaada yao na huenda wakaenda mbali hadi kuwawekea vikwazo baadhi ya viongozi wasisafiri kwenda kwenye nchi zao!

Lakini pia italeta jambo moja ndani ya nchi, wananchi wataichukia na kuipuuza serikali itakayoingia madarakani kwa kucheza faulo kwenye uchaguzi. Zitatumika nguvu nyingi kuipamba serikali hiyo lakini wananchi wataipuuza na huyo mtawala atachukiwa sana na wananchi hata baada ya kumaliza miaka yake mitano!

Ifahamike Lissu anapendwa ndani na nje ya nchi, kwanza ni kielelezo cha maajabu ya kusurvive risasi nyingi, hiyo inampa sympathy kwa wananchi na dunia. Na yeyote atakayejaribu kumdhuru kwa kumchezea hata rafu za kisiasa anaweza kuamsha ghadhabu kali za hawa marafiki wa Lissu!

Lakini pia, Serikali ya awamu hii inajinasibu na kumtegemea Mungu, na imekuwa ikilitumia Jina la Mungu kisiasa na kipropaganda, Hata hivyo Lissu anawanyang'anya karata hii kwa sababu Kusurvive kwake kunanasibishwa na Uweza wa Mungu. Kwa Lissu yeye ni Ushahidi wa Utendaji wa Mungu na hata akisimama jukwaani akataja Muujiza wa Mungu juu ya kusurvive kwake basi watu wa dini wanamsikiliza yeye zaidi kuliko wale wanaopenda kutaja jina la Mungu kisiasa tu!. Yaani Lissu akimtaja Mungu inaclick kwa wananchi zaidi kuliko hawa wanaopenda kulitumia jina la Mungu kisiasa!. Kwa hiyo kumuengua Lissu pia kutawachukiza wapenda Mungu nchini maana itatafsirika kama muendelezo wa shetani kutaka kumuangamiza Lissu!

Kwa upande wa Zanzibar pia hali ni hiyo, Iwapo Maalim Seif atafanyiwa dhulma tena, basi Umma wa Zanzibar utauchukia muungano zaidi na Utaidharau serikali ya Muungano na ya Zanzibar zitakazoundwa. Lakini pia Wahisani hawatatia ushirikiano mzuri kwa serikali ya Muungano ambayo ndiyo lazima iwezeshe figisu huko Zanzibar ili zifanikiwe!.

Lakini Maalim amepata heshima kubwa nchini na kimataifa kutokana na uvumilivu wake, na kupenda kwake amani na kujaribu mara zote kutumia njia za kisiasa kutatua migogoro aliyonayo.
Ifahamike kuwa iwapo serikali itamessup na Zanzibar, ikapelekea wananchi wa Zanzibar kuingia mabarabarani, kutatokea umwagaji wa damu wa kutisha huko Zanzibar, na hii itapelekea wahusika kuingia katika mkono wa sheria huko ICC.

Kibaya zaidi, Misaada na Mikopo kwa serikali inaweza kusitishwa na hata kupelekea vikwazo.

Kwa hiyo, Rais Magufuli ana uchaguzi, ama akubali uchaguzi uendeshwe kimagumashi na yeye ashinde kwa asilimia atakazozitaka yeye, lakini serikali atakayoiunda imdodee kutokana na hali ngumu ya uchumi itakayofuata kutokana na kususwa kimataifa na pia kuacha Legacy ya kuchukiwa na kubezwa na watanzania baada ya kustaafu au akubali kuendesha uchaguzi huru na haki ili apate heshima na kuinusuru nchi isitokee umwagaji damu wa kutisha huko Zanzibar na pia isipate mdororo wa kutisha wa kiuchumi.

Safari hii hakuna choice, bila uchaguzi huru na wa haki kwa pande zote za muungano serikali itakayofuata itapata tabu sana!
Sheria haina mbwembwe ukiizingua inakuzingua
 
Back
Top Bottom