Gai da seboga
JF-Expert Member
- Apr 19, 2019
- 478
- 962
Habari zenu mabibi na mababu!
Kwanza kabisa ni ukweli usiopingika kuwa kwa sasa kila mtu anapoambiwa au kusikia kuongezewa muda wa kutawala Rais magufuli anashikwa na ghadhabu na kutamani ata kumpiga mtu ngumi kutokana na ugumu wa maisha uliopo.
Sio watumishi wa Serikali, sio wafanyabiashara, machinga, wastaafu, wanachuo, wahitimu wa chuo, mama ntilie, wachuuzi, n.k wote hawa hawataki kusikia ata kidogo msamiati wa Rais magufuli kuongezewa muda wa kutawala, wamemchoka vibaya mnoo kiasi kwamba mpaka wanajuta kwanini walimpa uraisi na bila kupepesa macho wanatamani ata kesho tu Amalize muda wake wa kutawala waangalie ustaarabu wa raisi ajae.
Na wale wanaoshupalia kuwa aongezewe ni wabunge ambao wapo bungeni wakiona hawana cha kupoteza kwamba akitawala milele basi wao wakijipendekeza watakuwa kwenye maisha salama, lakini viongozi ambao wamemwagwa hawapo ata bungeni ukiwafata uwaambie JPM aongezewe Muda usipokuwa makini wanaweza kukupiga makofi mfano mfate lugola alafu mwambie JPM tumpe milele bhana kama hatokutukana, kwahyo wale wanaoshupalia ni wale ambao wananufaika nae tu ila mzee baba hakuna anaempenda watu washamchoka.
^^^^^^^^^^
Mambo ambayo akiyafanya Rais magufuli Watanzania wenyewe bila kushurutishwa watamlilia na kuandamana barabarani kuomba Rais Magufuli aongezewe muda wa kutawala ata milele.
1. Kuongeza nyongeza ya mishahara na kupandisha madaraja kwa watumishi wa umma. (hawa watu wametaabika na wana hali mbaya sana kwa muda wa miaka 6 sasa mpka barabarani wanajiongelesha wenyewe kwa stress, Magu akitaka apate mapambio ya kuongezewa muda wa kutawala basi hawa watu awapandishe mishahara kwa asilimia kubwa % na kuwalipa madeni yao wataongoza kumsifu na kumshinikiza).
2. Kuajiri vijana waliopo mtaani. (siku hizi wahitimu wa vyuo wamejaa mtaani kama njugu vile hawana kazi yoyote ile, sio walimu, sio manesi, madokta, bwana mifugo n.k, hili kundi ni kubwa mnoo na linaongoza kumchukia magufuli vibaya mno adi kutamani Mungu angempenda zaidi mana mtaani wanataabika hatari, vijana hawa hawana ata familia lakini wanaongoza kuwa na msongo wa mawazo).
3. Wastaafu kulipwa pesheni zao. (hapa wazee wengi wanasononeka na kushikwa na hasira mtu amemaliza kutumikia taifa lakini haki yake mwenyewe anazungushwa mpaka anakata tamaa, mzee kastaafu ila ana miaka mitano bado hajapewa pesa zake hayo mapenz yakutaka rais aongezewe muda wa kutawala atayatolea wapi!! Hawa ni wengi mnoo wengine mpaka wanakufa wamekosa stahiki zao.)
4. Wafanyabiashara kupunguziwa kodi za hovyo zinazowapekea kufunga biashara zao.
5. Wakulima wa korosho kulipwa pesa zao. (hawa watu sio tu kuwa wana hasira na huyu bali wana kisasi kikali san na ukitaka kujua machungu yao uwakute wanaongea kikabila, kiasi kwamba wanamuombea majaliwa angalau aje kuwa Raisi ili apunguze machungu ya watu wake wa kusini.)
6. Wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu kupunguziwa riba.
7. Wakulima kutafutiwa masoko ya uhakika na kupunguziwa gharama za pembejeo.
8. Kuzuia mfumuko wa bei kwa bidhaa mbalimbali. Mf. Mafuta, sukar, cement.
9. Mikopo himilivu kwa vijana na wanawake.
10. Bima bora za afya kwa Watanzania.
11. Kuhamasisha Matajiri duniani kuwekeza viwanda mbalimbali Tanzania.
Mh Raisi akiyafanya hayo bila chuki wala roho mbaya Watanzania wenyewe wataamua na kumshinikiza kwa maandamano atawale ata milele hadi afie ikulu.
~Gai da Seboga