Rais Magufuli akerwa na Bilioni 1 kutengeneza Mitaro Igunga

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
1574867733745.png

Rais John Magufuli amemtaka Mkurugenzi wa Igunga kuhakikisha kesho anaitisha kikao cha dharura cha madiwani Igunga kwa ajili ya kubatilisha matumizi ya fedha kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni moja ambazo zilipitishwa na baraza la madiwani kujenga mitaro.

Rais Magufuli amesema amewashangazwa na uamuzi wa madiwani hao kwa kutozipa kipaumbele barabara za mitaa zinazolalamikiwa na wananchi wengi na badala yake wameona mitaro ndiyo kipaumbele chao.

"Sasa madiwani mnaomba fedha kwaajili ya matumizi ya mitaro kweli, kwanini msingepitisha kwaajili ya ujenzi wa barabara, yaani fedha ziletwe kutoka serikali kuu. Mmkurugenzi naomba utekeleze maagizo niliyokupa la sivyo nitaagiza hizo fedha zisiletwe," Rais Magufuli.
 
Ujenge barabara bila mtaro ?
Naomba mnieleweshe wakuu,
Maana mimi nadheni mtaro ndio uanze then barabara ya rami
 
Ujenge barabara bila mtaro ?
Naomba mnieleweshe wakuu,
Maana mimi nadheni mtaro ndio uanze then barabara ya rami
Hata na mimi nilifikiri hivyo, nikaona labda Magu kaona la zaidi.

Tunajenga barabara bila mitaro, halafu kimvua kidogo tu kikinyesha barabara zinafurika, tunalaumiana.

Wataalamu wakitaka kutengeneza mitaro kabla ya barabara, rais anawaingilia.
 
Igunga inasikitisha sana, diwani anajiuma uma tuu halafu mbunge wao kafumu kila ziara ya Rais anajificha yule mzee kabaki kutembea kavaa shuka jeusi sijui kadanganywa na waganga wa wapi msomi mzima. Wananchi wanasema barabara mbovu, hazitengenezwi na maji hakuna.
 
Hata na mimi nilifikiri hivyo, nikaona labda Magu kaona la zaidi.

Tunajenga barabara bila mitaro, halafu kimvua kidogo tu kikinyesha barabara zinafurika, tunalaumiana.

Wataalamu wakitaka kutengeneza mitaro kabla ya barabara, rais anawaingilia.

Mm pia niliwaza kuwa mitaro ikijengwa ndio barabara zitadumu, pia bil 1 itatosha kujenga barabara za mitaa? Au ana maanisha kusawazisha barabara za vumbi, labda ngoja nicheki clip nitaelewa zaidi You Tube
 
Halafu shilingi bilioni moja ya leo kwenye miradi ya umma si hela nyingi hivyo.

Naelewa kunaweza kuwa na wizi, na rais anatakiwa kuudhibiti, lakini shilingi bilioni moja si hela nyingi hivyo katika miradi ya umma.

Inawezekana rais ana kumbukumbu ya shilingi ya zamani iliyokuwa na thamani sana, katika zama ambazo shilingi imeshuka thamani.
 
Bilioni moja inaweza kujenga barabara ya lami YENYE urefu wa km Kama moja tu!
Sitaki KUAMINI Kuwa waliopanga hiyo B1 ijenge mitaro kwanza walikuwa NI malofa,ikizingatiwa mji wa Igunga NI tambarare Sana hivo unahitaji mitaro ya kuyatoa maji....naweza kosolewa!
 
Magufuli anashangaa 1b kutengwa kwa ajili ya mitaro?,au anadhan hiyo pesa ni kama alivyo kuwa waziri wa ujenzi, kwa Igunga ilivyo naona hiyo 1b ni ndogo coz ni tambalare so lazima ichimbwe mitaro yenye kina ili kupeleka maji kirahisi.
 
Hiyo mitaro inajengwa hewani? Sio kwenye barabara?
Barabara bila mitaro zitadumu?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom