Rais Magufuli akataa shule kuitwa jina lake

Hb wa Ilala

JF-Expert Member
Sep 23, 2015
1,161
2,000
Rais John Magufuli amekataa shule ya msingi iliyojengwa hivi karibuni eneo la Bunju, Wilaya ya Kinondoni kuitwa kwa jina lake badala yake ameagiza iitwe kwa jina la Mkuu wa wilaya hiyo, Ally Hapi.

Taarifa ya badiliko la jina haikutolewa na Idara ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu kama ilivyozoeleka bali na mkuu wa wilaya hiyo wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya usafi kwa uongozi wa shule hiyo.

“Shule hii imejengwa kwa fedha zilizopatikana baada ya Serikali Kuu kubana matumizi. Tukaamua iitwe John Magufuli lakini yeye akatoa agizo shule ipewe jina la mkuu wa wilaya sina budi kukubaliana na hilo,” alisema Hapi.

Shule hiyo mpya iliyopo Bunju jijini imejengwa kwa lengo la kupunguza msongamano wa wanafunzi katika Shule ya Msingi Bunju A ambayo ilikuwa na wanafunzi 3,224.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo mpya, Ali Mwakapalila alisema ingawa inatarajiwa kuanza kupokea wanafunzi Januari 9 mwakani inakabiliwa na changamoto mbalimbali.

“Hakuna umeme wala maji, hii inaweza kuleta madhara kwa wanafunzi hasa linapokuja suala la matumizi ya vyoo,” alisema.

Baada ya hafla hiyo, Hapi alikwenda kwenye kiwanda cha saruji cha Twiga Cement ambako alipokea msaada wa mifuko 600 ya saruji kwa ajili ya kufanikisha ujenzi wa madarasa na majengo mengine.

Akipokea msaada huo, Hapi alisema msaada kutoka Twiga Cement unaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano inayoipa sekta ya elimu kipaumbele ili kuhakikisha inatolewa katika mazingira bora.

“Msaada huu umekuja muda muafaka. Tumeshajenga shule ila tunataka kuongeza madarasa, maabara, ofisi ya elimu na kuzungushia uzio ili watoto wawe katika mazingira salama. Lengo ni kuifanya shule hii iwe ya kisasa na itakuwa mfano kwa shule zote za Wilaya ya Kinondoni,” alieleza.

Pia, Hapi alisema wilaya hiyo ipo kwenye mipango ya kujenga maktaba ya kisasa kwa kushirikiana na kampuni hiyo ya saruji.

Mkurugenzi Mtendaji wa Twiga Cement, Alfonso Velez alisema kuchangia katika shughuli za kijamii ni moja ya mambo ambayo wamekuwa wakiyapa kipaumbele zaidi.

“Kushiriki shughuli za maendeleo katika jamii ni jambo ambalo tunalipenda zaidi. Yalipo maendeleo Twiga Cement ipo pia,” alisema Velez.
 

swissme

JF-Expert Member
Aug 15, 2013
13,660
2,000
kwasababu hiyo shule imejengwa na wapinzani na walimuambia kuwa tutatumia jina lako lakini lazima utawala wa wapinzani wawepo mstari wa mbele jana kaitwa kakataa kwasababu yaweza tokea kama yale ya mkuu wa mkoa Arusha.


swissme
 

issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
2,554
2,000
[


“Shule hii imejengwa kwa fedha zilizopatikana baada ya Serikali Kuu kubana matumizi. Tukaamua iitwe John Magufuli lakini yeye akatoa agizo shule ipewe jina la mkuu wa wilaya sina budi kukubaliana na hilo,” alisema Hapi.

Hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, kick zingine hizi za kitoto
 

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
10,048
2,000
Na Magufuli high schoo chato kwanini hakukataa...

Akaipa jina la mke au mtoto?......
 

Transcend

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
20,172
2,000
Hivi huyo mkuu wa wilaya angejataa na yeye aseme iitwe labda Bunju C

Ingekuwa ni dharau kwa mkuu wa kaya...
 

balimar

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
5,041
2,000
The silence ignores for most of the top layer-leaders to call schools for their very own names refer from national examination performance.
Tafiti fulani ilionesha shule nyingi zinazooitwa kwa majina ya viongo.zi kama mukapa, kikweete, leepumba, salmia et. al walikuwa top layer kwa kuleta mayai pale O`level.
Sasa labda watu wanakwepa kadhia hilo
 

Askari Muoga

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
6,129
2,000
Mara imejengwa kwa kubana matumizi mara hapi kapewa saruji na twiga cement ila bora ingeitwa hapa kazi primary school
 

Mr Hero

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
5,550
2,000
Wanasiasa wa kiafrika hawana tofauti na wafalme, Tazama Kabila Congo anayofanya,
 

mwasu

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
10,203
2,000
Kuna mambo mengine yana fanyika mpaka unaona aibu raia, dah! sijui acha tuendelee kuyaona.
 

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
49,521
2,000
Lazima akatae means Hyo shule kwanza haina umeme
Wala maji .....ipo ipo tu

Ova
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom