Rais Magufuli akabidhiwa rasmi ofisi ya Rais na Rais mstaafu Dr. Kikwete

Pia dallini kulikuwa na kaleee. ..kamtambo toka sumbawanga

Huyu jamaa sijui hata kama pale msoga ayakua anapatikana. Maana ni juzi tu kapanda helcopter kurudi huko, halafu siku mbili baadaye tunaambiwa yupo Ikulu. Yaani hatamani kabisa kustaafu huyu. Jalawii kumwambia Magufuri 'hebu rudi ujenzi mara moja mimi nifanye kakitu fulani japa, maana kuna kakitu nilikasahau'.
Pia msije mkashangaa zinaanza part za kuagana Ikulu zikifanyika mara mbili kwa wiki. Wataanza wafanyakazi wa Ikulu watafanya party ya kumuaga, watafiata makatibu wakuu, wakurugenzi, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya, mabalozi, viongozi wa kijeshi, na wengineo wengi. Hebu tusubirini.
 
Ahaaa, kumbe ndio maana mkulu alikuwa akipiga kazi kitaaa? Kumbe ofisi bado ilikuwa imefungwa. Basi sawa
 
new era,new president,same regime,new tanzania.naimani atatuvusha.jk is history,msimtajetaje tena humu atatutoneshea vidonda vya escrow
 
Naona anakohoa kohoa kizushi huku anacheka. Labda anajua nni kinaendelea!!!

Ukiangalia video clip, kuna kicheko Kikwete amecheka alipozungumzia safari za kushtukiza za Magufuli. " Nimesikia kwenye media kipimo cha MRI kinafanya kazi na watu wana msisimko. Ukifanyafanya namna vile, utasaidia sana kutatua matatizo tkhethe..(anacheka kicheko cha kiaina huku akiangalia chini) yanayowakabili.. yanayowakabili wananchi wa Tanzania.
Binafsi alivyocheka kaniacha na maswali mengi.
Wenye uwezo wa kufanya analysis ya vicheko.; kile ni kicheko cha kupongeza, kukebehi, kubeza au kufurahi ?
 
Atarudi tena na tena kwa kisa cha kutembea, alitaka aendelee kuwepo na kukausha hazina
 
Ndio maana alikuwa anazurura maofisini. Kumbe alikuwa hajakabidhiwa ofisi. Mkwere alikuwa bado ana funguo
 
Sitoshangaa siku nyingine wakisema anakabidhi nyumba ya rais au anakabidhi rasmi bustani ya rais .


Hahahahah nawaza tu
 
Baada ya kukausha hazina.
daud Mchambuzi hebu nisaidie jambo moja. Kama ulisikiliza hafla ile, nilishangazwa sana na JK na sikumwelewa pale aliposema " wananchi wanafurahishwa na unavyoshtukiza maeneo ya kazi, kama ulivyofanya pale MOI na nasikia kwenye media ile mashine inafanya kazi ........"
Kilichonishangaza ni kuwa alimalizia kwa kutoa kicheko cha kejeli ambacho hata Magufuli alionekana kukishtukia. Unadhani JK alikuwa anakejeli hayo mambo ya zimamoto ambayo hata yeye alianza nayo na kufeli au sababu ni nini hasa?
 
Last edited by a moderator:
Khah...sasa alikuwa anakaaje ikulu wakati ilikuwa bado ya kikwete!!!
 
Ukiangalia video clip, kuna kicheko Kikwete amecheka alipozungumzia safari za kushtukiza za Magufuli. " Nimesikia kwenye media kipimo cha MRI kinafanya kazi na watu wana msisimko. Ukifanyafanya namna vile, utasaidia sana kutatua matatizo tkhethe..(anacheka kicheko cha kiaina huku akiangalia chini) yanayowakabili.. yanayowakabili wananchi wa Tanzania.
Binafsi alivyocheka kaniacha na maswali mengi.
Wenye uwezo wa kufanya analysis ya vicheko.; kile ni kicheko cha kupongeza, kukebehi, kubeza au kufurahi ?

Sadoseba, hata mimi ningependa kupata tafsiri ya kile kicheko maana kimeniachia maswali mengi kichwani. Naona kama Magu aliki shtukia
 
Ni maoni yangu kwamba jk angekaa kimya hata miezi sita afanye mambo take binafsi,namuona kila siku Mara aongelee Taifa stars kwenye TV,Mara anakabidhi ofisi,nayo kwenye TV,yaani kwa mwananchi wa kawaida inamchanganya,jk amuache magufuli ajiimarishe kisiasa na kijamii kwa kiasi cha kutosha mpaka ashike mizizi taking into account mwenzie magufuli ndio katoka kwenye uchaguzi na anatakiwa ajenge public confidence in him. Afanye kama alivyofanya mkapa,magufuli ajihisi na awe huru kama rais ili wapinzani tukianza kumpa misumari asiwe na kisingizio
 
Back
Top Bottom