Rais Magufuli, akabidhi gari la kubebea wagonjwa katika hosipitali ya wilaya ya Chalinze

dubu

JF-Expert Member
Oct 18, 2011
3,500
3,481
Cd067Y7WIAAoQWB.jpg

Rais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amekabidhi gari la kubebea wagonjwa kwa hosipitali ya wilaya ya Chalinze, Ikiwa ni utekelezaji wa ilani na ahadi ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwa wananchi ikiwa ni pamoja na wa jimbo la Chalinze.

Gari hilo la kubebea wagonjwa limekabidhiwa kwa niaba ya Rais, na Katibu Mkuu Ikulu Peter Ilomo kwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi gari hilo, Katibu Mkuu Ikulu Ndugu Peter Ilomo amesema gari hilo limetolewa na Mheshimiwa Rais kwa hosipitali hiyo ikiwa ni kuitikia wito na utekelezaji wa ilani na ahadi ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM ya kuboresha huduma ya afya kwa wananchi wake kote nchini.
Aidha, Ndugu Ilomo amewaomba viongozi wa jimbo la Chalinze kulitumia gari hilo kwa matumizi yaliyokusudiwa ya kuwahudumia wananchi wa eneo hilo.

Akipokea gari hilo kwa niaba ya wananchi wa jimbo na Wilaya ya Chalinze, Mbunge wa jimbo la Chalinze Mheshimiwa Ridhiwani Kikwete amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa msaada huo na kuahidi kulitumia gari hilo kwa malengo yaliyokusudiwa, na kusema kuwa, utendaji kazi wa Rais Magufuli umekuwa ukiungwa mkono na wananchi wa kada mbalimbali na kuwaomba watanzania kuzidi kumuombea kwa Mungu.
5(8).jpg

Kwa upande wake Dakta Nasoro Ally Matuzya, amesema gari hilo limekuja kwa wakati muafaka kwa kuwa umezingatia utekelezaji wa malengo ya Milenia hususan lengo namba nne linalosisitiza kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto chini ya miaka mitano.

Naye Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Chalinze Ndugu Saidi Omar Zikatimu amesema gari hilo la kubebea wagonjwa litakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa jimbo hilo la Chalinze hususan katika kusaidia kutoa wagonjwa ambao wako katika maeneo ya vijijini wilayani humo na kuwafikisha katika hospitali ya Chalinze na hivyo kunusuru maisha yao kwa kupata huduma za afya kwa haraka.

Mbali na Wilaya ya Chalinze kupata msaada wa gari hilo la kubebea wagonjwa, tayari magari mengine mawili ya kubebea wagonjwa yameshakabidhiwa katika vituo vya afya vya Kiroka na Kisemu mkoani Morogoro.

Hospitali mpya ya Wilaya ya Chalinze imepanda hadhi kutoka kituo cha Msoga ambayo ilikuwa haina gari la kubebea wagonjwa na hivyo kufanya usafirishaji wa wagonjwa kutoka hospitali hiyo hadi hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Pwani ya Tumbi au kutoka maeneo ya vijijini kuwa mgumu.

Chanzo: ITV
 
Ama kweli uongozi ni dhamana ,juzi tu jamaa alikua anakatiza ikulu kama home kwake, leo hii mwenye Ikulu hata hajaonana naye
 
Hili litakuwa la pili
 
Ndio tunataka
Gari hilo hawatapanda ccm pekee
Wala familia ya Jk pekee
 
Kwanini Chalinze tu
Nadhani umesoma kichwa cha habari pekee na kutoa comment!

Soma habari yote!

**** paragraph inasema hivi;
Mbali na Wilaya ya Chalinze kupata msaada wa gari hilo la kubebea wagonjwa, tayari magari mengine mawili ya kubebea wagonjwa yameshakabidhiwa katika vituo vya afya vya Kiroka na Kisemu mkoani Morogoro.
 
katika habr za leo, mh Rais amemkabidhi gari LA wagonjwa ndg ridhawani. Najiuliza hivi magufuli ameshindwa kukabidh gari kwa wahusika kama vile MKUU wa wilya, au mganga MKUU wa wilaya au mkurugenz au ndo mwendelezo wa siasa!!!"
 
ikatokea jimbo la Arusha mjini wanapelekewa gari ai jimbo lolote lile LA wapinzani atawaita ikulu awakabidhi kama alivyofanya kwa Ridhiwan
 
Kama ulikuwa Unategemea huo msaada imekula kwako.Alishasema hawezi kugawa chakula kwa watoto wa Kambo. Sasa watoto wa Kambo anzeni kutafuta njia mbadala.mpate riziki zenu.
 
Kikwete alishindwa kupeleka ambulance akiwa mbunge, na waziri akashindwa kupeleka akiwa rais, Rizione ameshindwa kupeleka akiwa mbunge mpaka Magufuli kaamua kupeleka wa niaba yao! Kweli Kikwete ni bonge la jipu yeye na familia yake wana chalinze watakuwa na mahaba na hii familia si bure.
 
Back
Top Bottom