Rais Magufuli aizika rasmi BRN, wafanyakazi wahamishiwa idara nyingine za Serikali

Hivi serikali za CCM huwa hazina continuity ya mambo yao? Kila mtu akija lazima aje na kitu kipya na kutupilia mbali cha mtangulizi wake?
 
Kuna wazee pale walikuwa vizuri sana.....Peniel Lyimo na yule. Omari Issa......nao watarudishwa utumishi?? Ahhahahahaah labda wengine wadogo wadogo....wale wanarudi kwao kupumzika!!
 
Kufanya kazi serikali ya Tanzania ni majaribu aiseee....imagine mtu aliapply kazi BRN toka alikotoka Kama private sector..Leo anapangiwa ofisi ya DED Gamboshi! Wallah ngosha utauwa Watu!
 
kila mtu atimize wajibu katika eneo lake la kazi hakuna haja ya mambo kama haya kusimiana kama punda.
 
Angejitokeza mwerevu moja akampinga Kikwete na Linda katika hili la BRN angepigiwa kelele na Lumumba kwa kudai ni usaliti!!

Leo Lumumba hao hao wataandamana Ku support
BRN ilikuwa tatizo kubwa aisee.
Iliingilia 'chain of command' ya wizara nyingi.
Afu ukiangalia matunda yake sasa
 
Bora BRN matokeo yalionekana kuliko hili la nchi ya Viwanda
BRN ilikuwa na matokeo gani mkubwa? BRN was another rubbish! BRN ya kulima miwa, sera ya kiswahili ktk shule kwa ngazi zote! BRN ya kuondoa divisheni na kuingiza GPA sekondari?

Hicho kitengo chenyewe kiliundwa bila sababu. Bungeni opposition walikataa lakini wapi! Nahisi kulikuwa na watu wanatakiwa kupewa madaraka tu au pesa fulani zilitakiwa kuliwa!
 
BRN ilifeli hata kabla haijaanza. Huwezi kutegemea matokeo makubwa wakati hufanyi Kazi inavyotakiwa na kuwa na usimamizi makini. Hii taasisi ya PDB ilikuwa mzigo tu, ni vyema imekaa pembeni maana Kazi zake nyingi wangefanya taasisi kama ya Tume ya Mipango. Ilichukua staff wengi wazuri kutoka private sector na kuwalipa vizuri kuliko walikotoka. Vision yake Ilikuwa sawa ila kwa hali ya nchi yetu hatukuhitaji hii taasisi. JPM hongera kwa hili, Matokeo makubwa yanakuja kwa uthubutu sio kufuatilia miradi.
 
hizi program zinaanzishwaga ili kupata fedha hasa za kampeni...tutaziona tena kwakasi 2019-2020 na zitapongezwa kama siyo hizi zilizofutiliwa mbali.
 
BRN ilileta matokeo gani?
... hayo yalikuwa "maono ya mtu" badala ya maono ya taifa! Aliyeifuta (BRN) naye kaibuka na maono yake binafsi ambayo nayo hayakutufikisha popote yakafia mbali! Tanzania nchi ya majaribio; kichwa cha mwendawazimu kweli kweli!
 
Back
Top Bottom