Rais Magufuli aivunja Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala

Sasa hivi EFM & TVE, CLOUDS, ITV, RADIO ONE, EATV, WASAFI, RADIO MARIA, zipo nje kidogo ya jiji la dar es salaam halafu RADIO TUMAINI NA TI FM zipo katikati ya jiji la Dar es salaam pale Tabata Magengeni ambapo wakazi wake wanakula mihogo iliyoiva na mibichi wanasinzia mchana kutwa.
We naye ni mmoja wa wajinga
 
Hapa nipo kwenye panton feri wamefungulia Singeli sauti ya juu balaa, sijui wanashangilia ilala kuwa jiji
Kwa Sasa ni saa 0434 alfajiri
 
Hili suala hata MATAGQ wenyewe hawaelewi chochote
Anyway huku Ubungo kijijini maisha yamekuwa magumu nataka niamie jijini Ilala
 
Tusipotezeane muda na wala tusibishe kwa hili Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli yupo sahihi kwani Ilala ndiyo Dar es Salaam na Tanzania vile vile. Na hata Watoto wa Mjini wote wapo Ilala na siyo Kwingineko ambako kumejaa tu Washamba na Malofa watupu japo wenyewe ( wao ) wanajiona Wajanja.
Umesahau kusema hili, hata wamachinga wote wapo Ilala
 
Dsm ilikuwa inaundwa na manispaa nne kinondoni, Ilala, Ubungo na Kigamboni

Halmashauri ya jiji la dsm ilikuwa inasimamia halmashauri za manispaa zote nne lkn haina eneo lake rasmi la kiutawala, halmashauri ilikuwa na uwezo kuuchukua mradi wowote katika manispaa yyte na kuendeleza na kugawana manispaa inayopatikana mradi kwa utaratibu maalum, hvyo alichokifanya ni sahihi tu.
Umeiweka vizuri mkuu, ninakushukuru lililofanywa lina faida nyingi kwa uchache:-
1. Dar es salaam Jiji lililokuwepo ilikuwa kama kupe tu kunyonya Halmashauri zingine;
2. Ilikuwa inaongeza gharama za uendeshaji bila sababu Mf. Magari, watumishi, n.k
3. Kuweka mgongono wa kimajukumu
Kutaja japo kwa uchache.
 
Ndugu zangu Wachagga hapo Kimara walikuwa wanaaga kila January kuwa wanarudi jijini Dar sasa watakuwa wanaenda Wilaya ya Ubungo wakati ndugu zao pale Moshi watakuwa jijini soon
Moshi kamwe haiwezi kua Jiji hata kama ina vigezo, Jiwe hawezi kubali hilo labda akutoka madarakani
 
Buguruni, Vingunguti, Kivule, Gongolamboto, Chanika, Pugu ndio jiji halafu Masaki, Oysterbay, Msasani, Mbezi beach, Kinondoni, Sinza eti ni Manispaa tu, Maajabu!
 
Tusubiri tu kwa uvumilivu,ipo siku ataibeba dar nzima kama ilivyo na kwenda kuitua chato
 
WATU WALIPOKUWA WANAONGELEA DEMOKRASIA WATU HAWAKUELEWA WENGINE , DEMOKRASIA IKIBAKWA KWA WAPINZANI BAADAYE HUHAMIA NDANI YA CHAMA TAWALA .....UAMUZI WA KUFANYA ANAVYOTAKA KWENYE SERIKALI ZA MITAA NDIO ULIOKUWA UNAFANYA ALAZIMISHE MADIWANI WOTE WAWE WA KWAKE ...NI WAZI KUNGEKUWA KUNA MADIWANI WA VYAMA VINGI BARAZANI HANGETHUBUTU KUFANYA HIVYO KWAKUWA MALALAMIKO YANGEKUWA MENGI, KAMA TU WAKATI ULE KUWEKA MEYA WAKE ALIKUWA ANASHINDWA ,KWA KUHOFIA VURUGU ....LEO SASA CCM WAMEONA HUYU MTU ALIVYOKUWA NA DHARAU.....UNAVUNJA HALMASHAURI HATA BILA KUSHAURIANA NA MEYA WAHUSIKA .....DHARAU SANA .,ANAJUA HAWANA LA KUMFANYA NA HAWANA PA KWENDA KULALAMIKA AU KUNGEKUA NA WAPINZANI BARAZANI WANGEUNGANA NAO ,HAWAPO.
NA HUU NI MWANZO TU WA UVUNJAJI WA DEMOKRASIA NDANI YA CHAMA CHAKE MWENYEWE .....HATA MKAPA ALIPOVUNJA HALMASHAURI HAKUKURUPUKA ALIFANYA UTAFITI NA ALIWASHIRIKISHA UN-HABITAT ....
WATU WANASEMA HATA MAMEYA HAWAHESHIMIKI TENA ANAWAONA KAMA MADIWANI TU .. MNAONA HATA ALIVYOMTUKANA MEYA WA MOROGORO HADHARANI .....UNAJUA MTU AKIKUPA KITU BURE LAZIMA AKUSIMANGE ....KAMA PIA WABUNGE WANAVYOSIMANGWA BILA MAGUFULI HAWANGEFIKA BUNGENI HIVYO WAFUNGE MIDOMO
 
Tusipotezeane muda na wala tusibishe kwa hili Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli yupo sahihi kwani Ilala ndiyo Dar es Salaam na Tanzania vile vile. Na hata Watoto wa Mjini wote wapo Ilala na siyo Kwingineko ambako kumejaa tu Washamba na Malofa watupu japo wenyewe ( wao ) wanajiona Wajanja.
Bakhresa anaishi wapi?
Diamond anaishi wapi?
Maraisi wastaafu wanaishi wapi?
Mwamunyange anaishi wapi?
Nyumba za mawaziri ziko wapi?
Mo anaishi wapi?
Acha ushabiki ilala ni ofisi tu Ila madoni wote makazi kinondoni
 
Rais kafanya jambo jema.

Ukisema kwamba Dar hakuna Wilaya inaitwa Dar es Salaam, hata Kilimanjaro, Ruvuma, Rukwa, Mwanza, Mara, Pwani Manyara, Kagera, pia hakuna Wilaya zenye majina ya hiyo mikoa.

Rais kafanya jambo jema kuokoa mapato yaliyokuwa yanaenda Halmashauri ya Jiji isiyokuwa na eneo la kiutawala na isiyo na miradi
 
Hoja siyo ku criticise. Hoja ni kwamba jamaa humu wametoa maelezo yanayoeleweka hadi tusioelewa tumeelewa.

Mimi mmojawapo sikuwa naelewa lakini niliposoma thread hii nimeelewa.

Tabu ni baadhi yenu kama wewe mmeng'ang'ania kilichomo kichwani na ambacho ni wrong.

Kwanza waliotuelewesha hadi hapa inaelekea wamesomea mambo haya na wamefanya kazi nzuri na haikuwa lazima kutuelewesha.

Wametupa elimu ya bure wewe unataka warudierudie. Ni wajibu wako usiyeelewa kurudiarudia usichokielewa.

Hivi wabongo mna shida gani hasa. Why bad blood always towards each other. Nlidhani as country we're truly related in one way or other. Kipi kinakuwa kizito kuchukia mtu ambae anacriticise kitu cha nchi yake aweze elewa. Kipi kinakuumiza kutumia nguvu ya kutukana watu ambao hujui hata kusema wengine ni wakubwa kwako humu au wana nafasi fulani hata kwa Mungu. Unapata faida gani hasa ukimchukia m2 ambae hata ID yake ni fake? 2badilike jamani kuhoji sio kosa kisheria wala dhambi. Kutukana je? Jenga hoja elewesha watu waelewe hata kama hawataelewa jaribu mpaka utakapo ona yafaa.
 
Back
Top Bottom