Rais Magufuli aivunja Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala

Bora mana walikua wanakula hela za bure posho kila mwezi mia tatu mia tatu, Mkurugenzi alikua anatembelea bonge la Benz
 
KIUFUPI..mkoa wa DSM utabaki kuwepo na JIJI LA DSM litaendelea kuwepo ila tu kiutendaji, Ilala itakuwa inafanya majukumu ya mkoa mzima ndio maana imepandishwa hadhi kuwa Halmashauri ya Jiji...BINAFSI NIMEMUELEWA RAIS.
Yeye anasema jiji la ILALA wewe unasema jiji la Dar, bado hujamwelewa
 
Hii elimu ya jiji,mji, manispaa na halmashauri mbona ilitolewa shule ya msingi

Ndio shida ya kusema logarithm ilikuwa inasaidia nini matokeo yake mnakuja kutusumbua
Hizo zote ni daraja za Halmashauri kijana:- kijiji, mji mdogo, mji, Wilaya, manispaa na jiji na hiyo ni taaluma inatolewa chuo kikuu tatizo wabongo wajuaji
 
Sio kweli, hujui tafsiri ya local government, na hujui maana ya Area of jurisdiction ' Mkoa mzima ni jukumu la Mkuu wa Mkoa Halmashauri huwa ina jukumu la kuhudumu ndani ya enao lake la kiutawala tu, na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam haikuwa hivyo kama usemavyo isipokuwa ilikuwa ili chukua mapato mfano ya parking, taka ngumu, stend ya Ubungo, soko kuu la kkoo n. K muwe mnauliza kama hamjui si kuropokwa
 
Hapa tunashindwa kuelewa, kwa mfano Mwanza mjini (kati) kuna wilaya mbili ambazo ni Nyamagana na Ilemela.
Ilemela imepewa hadhi ya kuwa manispaa ya Ilemela, lakini hakuna Manispaa ya Nyamagana badala yake Nyamagana imebeba hadhi ya Jiji la Mwanza.
Katika matukio yote ukisikia wanaongea jiji la Mwanza maana yake wanaongelea wilaya ya Nyamagana na sio mkoa wote.
Nimekusoma mkuu
 
Mliokuja Dar es Salaam na Malori ya Ng'ombe pamoja na Treni za Mizigo kutokea Mikoani ( tena Vijijini kabisa ) wala huwa hamjifichi. Washamba wakubwa nyie. Ilala ndiyo Dar es Salaam na Tanzania hutaki tafuta Sumu ya Panya ikoroge, uinywe ili Ufe kabisa.
We endelea kusema washamba akati ndo matajili hapa mjini wewe kazi yako kukaa nyuma ya keyboard unatukana tuu
 
Sio kweli, hujui Tafsiri ya local government, na hujui maana ya Area of jurisdiction ' Mkoa mzima ni jukumu la Mkuu wa Mkoa Halmashauri huwa ina jukumu la kuhudumu ndani ya enao lake la kiutawala tu, na Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam haikuwa hivyo kama usemavyo isipokuwa ilikuwa ili chukua mapato mfano ya parking, taka ngumu, stend ya Ubungo, soko kuu la kkoo n. K muwe mnauliza kama hamjui si kuropokwa
kiazi wewe nani karopokwa...hujasoma hapo mwanzoni nilivyoandika?....'ila ikiwa nimetoa maelezo yasiyo sahihi, mwenye uelewa zaidi atafafanua'...Unakuja unatumia lugha za hasira na kupaniki...kuwa mstaarabu kiazi wewe...
 
Hapa tunashindwa kuelewa, kwa mfano Mwanza mjini (kati) kuna wilaya mbili ambazo ni Nyamagana na Ilemela.
Ilemela imepewa hadhi ya kuwa manispaa ya Ilemela, lakini hakuna Manispaa ya Nyamagana badala yake Nyamagana imebeba hadhi ya Jiji la Mwanza.
Katika matukio yote ukisikia wanaongea jiji la Mwanza maana yake wanaongelea wilaya ya Nyamagana na sio mkoa wote.
Kubwa ni kutofautisha kati ya Tawala za mikoa na serikali za mitaa, na kuirejea article 145 na 146 katika katiba haya unayoyaeleza wewe ni wazi umetumia uelewa binafsi na si wa kitaalam. HALMASHAURI zina kazi zake ndani ya Tawala za mikoa na zenyewe ndizo sauti ya wananchi ni kama mamlaka iliyopewa bunge kutusemea wananchi wote Tanzania kupitia wawakilishi pale Dodoma, ni sawa na kusema Tanzania ni Dodoma maana pale ndipo sheria na Bajeti zetu zinapasishwa
 
C4AD171B-3012-4F5F-8A23-F527BCEAA91D.jpeg
Nje ya jiji kwa kwa kwa
 
Tusipotezeane muda na wala tusibishe kwa hili Mheshimiwa Rais Dkt. Magufuli yupo sahihi kwani Ilala ndiyo Dar es Salaam na Tanzania vile vile. Na hata Watoto wa Mjini wote wapo Ilala na siyo Kwingineko ambako kumejaa tu Washamba na Malofa watupu japo wenyewe ( wao ) wanajiona Wajanja.
Jiji la Dar es salaam lote hamna kitu nenda Nairobi kwanza ujionee, Dar es salaam inazidi Mikoa ya Tanzania tu, Dar es Salaam bdo sana
 
Dar es Salaam ni jiji la kawaida Sana Ila nashangaa wazawa wanaishadadia!! Nyie wazawa wa Dar es Salaam tembeeni muone majiji ya wengine yalivojengwa nenda hata hapo Nairobi, kumbe nyie ndyo mpo bize kuicompare Dar na Nairobi pumbafu wazawa wa Dar wasiojielewa
 
Kwenye nchi za wenzetu mambo kama haya huwa yanapelekwa kwanza kwa wananchi wakayajadili halafu wakayapigie kura kabla ya serikali haijafanya uamuzi. Wakazi wenyewe ndiyo wanaamua kubadilisha status ya mji au sehemu yoyote wanayoishi kupitia kura za maoni au referendum. Sisi bado sana.
Mbona sisi tulipigia kura katiba ya Warioba! NA posho juu! Hahahaha!
 
Hivi kwa nini baada ya halmashauri ya manispaa ya Ilala kupanda hadhi isingeitwa halmashauri ya jiji Ilala badala ya Dar es Salaam ili hata halmashauri zingine katika jiji hilo la Dar es Salaam kama Kinondoni, Temeke, Ubungo na Kigamboni nazo siku zikipanda hadhi kuwa jiji zichukue majina yao waliyonayo yaani Halmashauri ya jiji Kinondoni, Temeke n.k?
 
Rais Magufuli ameivunja Halmashauri hiyo na kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuanzia leo Februari 24, 2021

Ameipandisha hadhi Halmashauri hiyo kwa Mamlaka aliyonayo chini ya Kifungu cha 5(1) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura ya 288

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Nchi - TAMISEMI, taratibu nyingine za kisheria ikiwemo kuhamisha shughuli za Halmashauri ya Jiji ya Dar iliyovunjwa zinakamilishwa


View attachment 1711235View attachment 1711236View attachment 1711237View attachment 1711238View attachment 1711239View attachment 1711240
Kwa maoni yangu hapakuwa na sababu ya kuvunja Halmashauri ya Jiji kwa kigezo kuwa haikuwa na eneo la utawala. Mimi ningeshauri kuwa badala ya kuivunja maeneo ya utekelezaji yafuatayo yangeondolewa Manispaa na yangekabidhuwa jiji:
1. Maji safi na maji taka. Halmashauri ingenunua share katika Dawasa ili iweze kuisimamia kiutekeleza. Dawasa ingepewa jukumu la kushughulikia maji ya mvua.
2. Elimu ya sekondari.
3. Barabara kubwa za mjini. Manispaa wangeendelea na barabara za kwenye vitongoji.
4. Mazingira na mabadiliko ya tabia nchi. Hii inahusu mapori, fukwe na mito yote.
5. Usafiri katika barabara kubwa. Mwendokasi uratibiwe na jiji.
6. Usafiri wa mikoani na wa kimataifa ikiwa pamoja na vituo vya basi, treni na ndege pamoja na bandari.
7. Hospitali za rufaa zote.
8. Utalii
Haya ni maeneo ambayo yanahitaji mtazamo wa maendeleo ya jiji, sio manispaa.
Manispaa zingeendelea kusimamia:
1. Elimu kuanzia chekechea hadi praimari.
2. Vituo vya afya.
3. Sehemu za burudani na michezo kwa jamii.
4. Maktaba za jamii.
5. Sehemu za biashara kama masoko.
6. Barabara za kwenye vitongoji.
7. Usafiri katika vitongoji ( bodaboda, bajaj, teksti, daladala n.k.). Hii ikiwa pamoja na vituo husika.
8. Usafi wa taka ngumu.
9. Usalama wa wakazi. Hii ni pamoja na kuweka taa za barabarani.
10. Huduma za zima moto.
11. Kutoa vibali vya ujenzi.
12. Ukusanyaji wa kodi.

Manispaa zitatakiwa kuchangia bajeti ya Jiji kwa kuipa sehemu ya mapato yao.

Kwa kufanya hivi patakuwa na coordination ya maendeleo ya Jiji kwa manufaa ya wakazi wote. Aidha, brand ya jina la Dar es Salaam itabakia palepele.

Meya wa Jiji atokane na kura ya moja kwa moja ya wakazi wa jiji. Aidha, mameya wa manispaa pamoja na wabunge wa jiji ndio wataunda Halmashauri ya Jiji.

Amandla...
 
Back
Top Bottom