Rais Magufuli aitikia wito wa maridhiano wa Mbowe, leo akutana na viongozi waandamizi wa vyama pinzani

M-mbabe

JF-Expert Member
Oct 29, 2009
13,203
23,020
Ni dhahiri kuwa Mbowe na Chadema wamezichanga na kuzicheza karata zao vyema sana. Kitendo cha Mbowe kutamka hadharani umuhimu wa maridhiano kati ya serekali na wapinzani kililenga ku draw attention ya sympathizers wa mustakabali wa mwenendo wa kisiasa na utawala bora hapa nchini.

Sympathizers waliolengwa si wengine bali ni wale tuliowabatiza jina la "mabeberu" ambao siku za hivi karibuni wameonekana (inasemekana as a reaction to ile speech ya Mbowe) kuishupalia vilivyo serekali ya awamu ya 5 kuhusiana na siasa kandamizi na ukiukwaji wa haki za binadamu. Ni kipindi hicho hicho pia tumeshuhudia World Bank wakisitisha mkopo unaosemekana ulikuwa ni kwa ajili ya kuchangia maendeleo kwenye sekta ya elimu.

JPM leo kakutana na baadhi ya viongozi wa vyama andamizi vya kambi ya upinzani, definitely ikiwa ni mkakati wa kuwatuliza munkari "mabeberu" wasiendeleze valangati walilolianzisha hivi karibuni.

Whether JPM atafanikiwa kwa mkakati huu, it remains to be seen.

On the other hand, whether wapinzani watalegeza kamba katika madai yao ya msingi ya katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.... that also remains to be seen.

Nirudie tena kumpongeza Mbowe na Chadema kwa kuchokonoa suala la maridhiano ambapo imepelekea JPM kusalimu amri na leo hii kukutana na viongozi wa opposition camp.

Stay on this page.
 
Mh mbowe angekuwa gari ningemwita FIAT huyu jamaa ni mwanasiasa ngumu na mvumilivu wa misukosuko ya kisiasa, sikuzote yupo straight na kile anachoamini...
Alivunjiwa hotel yake ya billcanass,kunyang'anywa shamba na biashara zake kupigwa stop lakini bado amekomaa na anaendelea kuchanja mbuga
 
Suala la viongoz wa upinzani kuitwa ikulu au kuzungumza na viongoz tawala halijaanza leo,
Si jipyaaa!

Tatizo kubwa hapa je,,vyama pinzani vinakubali kubadiri mtazamo wa kipinzan katika kila jambo tu,hata kama kuna mazur yanafanyika wao ni kukinzana tu!!

Ideology mbaya iliyopo,ukiwa mpinzan basi ndo upinge mabaya kwa mazur!

Lazima wapinzani waje na mtazamo chanya,si kupinga kila jambo,

Siamini kama mbowe na chama chake anashindwa kukaa chini na kuorozesha mapendekezo mazur yenye masrah ya nchi akayafikisha kwa magufur na yasifanyiwe kazi..

kuna vitu vingine ni siasa za anga ila kwa mwananchi mwenye akili na mapenzi ya nchi si ya chama ataona uhalisia wa hizi mambo
 
Ni utaratibu wa mkuu wa nchi tu na sio shinikizo la mbowe, raisi wetu kila siku anasemaga maendeleo hayana vyama

Naona mmeanza kuchukia haya maridhiano..mlitamani uadui uzidi kuota mizizi na kujichimbia chini zaidi.bila shinikizo wala Meko asingepoteza muda kukaa na watesi wake ili tu kupata maridhiano
 
maridhiano ya maana na ya dhati awepo Kamanda Mbowe,Mkubwa Zitto na zaidi Tundu Lissu

ukiacha kidogoo Maalim

Lipumba au Mbatia zaidi wameenda kupiga picha za mandhari ya White House na kuomba kupokelewa uwanja wa Taifa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kila siku unapigana na wazungu, sometimes unawaachia wao na vibaraka wao kidogo..Hivyo ndivyo mwl nyerere / nelson mandela walipata heshima kwa beberu na waafrika..Naona JPM amebadilika anajua sasa kucheza hii game..
Angejifanya kama Mugabe angepoteza heshima kote hadi kwa waafrika
 
Back
Top Bottom