Rais Magufuli aitaka Jumuiya ya Wazazi CCM kuzirejesha shule zake serikalini

FikraPevu

JF-Expert Member
Jan 2, 2010
303
236
Rais wa Tanzania, John Magufuli ameitaka Jumuiya ya Wazazi ya Chama Cha Mapinduzi kuzirejesha serikalini shule za sekondari ambazo imeshindwa kuziendesha ili ziboreshwe na kutoa elimu bora kwa wanafunzi.

Ametoa agizo hilo leo kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Jumuiya ya Wazazi mjini Dodoma ambapo amesema ili kuipunguzia majukumu ya kuhudumia jamii, serikali iko tayari kuzichukua baadhi ya shule ili ziendelee kutoa huduma bora ya elimu kwa wanafunzi wa Tanzania.

“Uongozi utakaokuja na ninyi Jumuiya ya Wazazi kama mtaona inafaa kwa baadhi shule ambazo mmeshindwa kuziendesha na hasa katika shule hizi 54 mkaamua shule 10 au 20 kwamba zichukuliwe na serikali tutazichukua kwa ajili ya kufidia hayo madeni”, amesema rais Magufuli.

Ameibainisha kuwa mpango wa serikali kutoa elimu bure kwa shule zake umeleta changamoto kwa shule zinazomilikiwa na watu binafsi kukosa wanafunzi kwasababu wengi wanakimbilia kwenye shule za serikali ili kukwepa gharama za masomo.

“Ninafahamu bado kuna changamoto kubwa kwenye shule zetu kwasababu ya sera ya elimu ya sasa hivi tunatoa elimu bure. Kwa hiyo unapokuwa na shule nyingi za serikali zinazotoa elimu bure ni vigumu sana kupata wanafunzi watakaoenda kwenye shule ya kulipia”, amesema rais Magufuli.

Jumuiya hiyo ya CCM ambayo inamiliki miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii, pia imewekeza katika sekta ya elimu ambapo ina shule 54 za sekondari na Chuo kimoja cha Ufundi cha Kaole kilichopo mkoa wa Pwani ambacho kinatoa Astashahada ya Kilimo na Mifugo.

Mchakato wa kuzirejesha baadhi ya shule za jumuiya hiyo mikononi mwa serikali umeanza, ambapo shule ya sekondari ya Omumwani iliyoko mkoa wa Kagera imerejeshwa ili kuboresha huduma zake kwa kuwafikia wanafunzi wengi zaidi.

Shule hiyo iliwachukua wanafunzi wa shule mbalimbali mkoani humo ambazo ziliharibiwa na tetemeko la ardhi lililotokea Sepetemba 2016. Kwasababu ilikuwa ni shule ya kulipia serikali imeibadilisha umiliki wake kutoka kwa Jumuiya ya Wazazi kuifanya kuwa ya umma.

“Mwaka jana tulipoenda Kagera baada ya tetemeko nilitembelea shule ya Omumwani na nikaona huduma nzuri ilizokuwa inatoa kwa wanafunzi waliokuwa shule zao zimeanguka. Nikatoa maagizo mlikubali kupokea wanafunzi wa serikali na shule mbalimbali katika mji wa Bukoba na mkaanza kuwahudumia pale”,

“Baadaye nikawaomba kwamba shule sasa tuichukue iwe ya serikali, mlinikubalia tumeichukua, tukabaki namna ya kutafuta fedha za kulipa. Wiki iliyopita tumelipa hizo bilioni 1.7”, amesema rais Magufuli

Hata hivyo, ameitaka Jumuiya hiyo kuendelea kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ajili ya manufaa ya taasisi hiyo muhimu kwa chama tawala, “Jumuiya ya wazazi haitafutwa nikiwa mimi Mwenyekiti wenu. Ni muhimu kwa maendeleo ya chama lakini ni muhimu kwa ustawi wa taifa letu”.

Zaidi, soma hapa => Sera ya Elimu Bure kuzirejesha shule za CCM mikononi mwa serikali | FikraPevu
 
Wanarejesha kwa kuuza au wanatoa bure kwa sababu wameshindwa kuendesha kama vile viwanda walivyo binafsisha?

Msisahau na viwanja vya michezo pia kuvirejesha
 
Hiki ni kichaka cha ccm kujipatia hela za bure kwa kuiuzia Serikali kwa bei ya kifisadi ili kujipatia fedha za bure tumewashitukia
 
Heading yako inakwenda nje ya nilivyokielewa nilichokisikia. Amesema zile zitakazowa shinda kuzihudumia, zipelekwe serikalini. Hakusemam shule tu.
 
Mkulu wakati mwingine anawaza vyema lakini sasa uwakilishi na utekelezaji ndio ipo mineno hapooo
Shule za wazazi zilifundisha tabia njema kwa watoto
Kabla ya kuamua lolote Mkulu atatue shida ya walimu kwanza
 
Back
Top Bottom